Kwa zaidi ya wiki mbili wabunge wanaojiita UKAWA wamekuwa wakimnyanyapaa mwanamke mdada mdogo Dr. Tulia kwa kumzomea na kumdhihaki huku wakitimka bungeni mithili ya mbuzi wanaofunguliwa bandani kuelekea machungioni.
Mbaya zaidi hata wanawake wenzie nao wameungana na hiyo kadhia bila kujali kufanya hivyo wanamvunja moyo na wanawaogopesha wanawake wengine kuthubutu kushika nafasi za juu za uongozi.
Dr. Tulia ni mgeni katika nafasi za kisiasa na ameinuliwa ili kuwatia hamasa wanawake na vijana kushika nafasi za juu za uongozi na kuharakisha lengo la millenia la 50/50. Cha kushangaza balada ya kumtia moyo na kumsaidia anapokosea ndio kwanza wanamzomea wanamdhihaki na kumkimbia bungeni, mbaya zaidi wamefikia hatua ya kufanya vituko vya hovyo kama kujifunga toilet paper midomoni.
Natoa wito kwa jumuia za akina mama kama umoja wa wanawake wa ccm UWT, na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu na haki za wanawake na watoto na usawa wa kijinsia kama TAMWA TGNP TWAWEZA wajitokeze kukemea na kupinga tabia hii ya kumnyanyapaa mwanamke tena binti mdogo anayejitahidi kushika nafasi za juu za uongozi.
Ipo haja ya kuandaa kongamano tujadili uhalali wa genge haramu la ukawa kumkosea heshima huyu binti. Tena genge hilo likijumuisha wanawake wasomi na watetezi wa haki kama Halima Mdee na wanawake waliojijengea heshima kwa muda mrefu kama mama Ruth Mollel nao wamejichanganya kwenye huo uhuni. Sasa ifike sehemu iwe basi kwa haya yanayojitokeza.