Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 97
- 1,751
UWEZEKANO WA KUBAMBIKIZIWA KESI.
Na Bashir Yakub, Wakili
+255 714 047 241.
Hariri Mohammed Hariri na mke wake Muna Said Omary walikamatwa tarehe 1 Machi 2018 na kushitakiwa kwa kukutwa dawa za kulevya aina Heroin Gram 214.11.
Katika kesi hiyo ya Uhujumu uchumi Namba 2/2020 ushahidi unaonesha kuwa usiku wa tarehe hiyo nyumbani kwao Matitu,Mtaa wa Kisutu, Kinondoni askari wa kawaida na wale wa kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya walizingira nyumba ya watuhumiwa hao kwa ajili ya kazi ya kuwakamata.
Kwamba usiku huo kabla ya kuingia ndani ya nyumba ya watuhumiwa walimtafuta kiongozi wa mtaa ajulikanaye kamaBi Mwajua Ubaya ambaye waliongozana naye hadi kwa watuhumiwa.
Walipofika waligonga hodi na kuingia ndani ya nyumba ambayo watuhumiwa waliwakuta. Kulitokea ubishi kidogo wa kuwazuia maafisa hao kuingia ndani lakini baadae waliingia.
Walipokuwa wameingia walifanya upekuzi wa chumba kwa chumba hadi walipofika chooni na kukuta mfuko wa nailon ambao ndani yake ulikuwa ni kiasi hicho cha dawa za kulevya.Walizuia polisi na baadae mahakamani.
Jaji I.K.Banzi katika ushahidi uliowasilishwa na Jamhuri aligundua yafuatayo.
Kuwa ushahidi wa askari unasema kuwa upekuzi ulianzia kwenye chumba ya baba wa mtuhumiwa, ukaingia chumba ya watoto, ukaingia sebuleni, ukaingia chumba kingine master na mwisho chooni ambako madawa yalikutwa.
Ushahidi wa askari mwingine unasema upekuzi ulianzia kwenye chumba ya baba wa watuhumiwa, kisha chumba ya watoto, sebuleni, jikoni, chooni ambako madawa yalikutwa na mwisho chumba kingine master.
Hawa askari wawili ambao wote walikuwa kwenye tukio, mmoja anasema chooni yalipokuwa madawa palikuwa pa mwisho kupekuliwa na yakakutwa madawa, na mwingine anasema chooni yalipokutwa madawa hapakuwa pa mwisho bali baada ya hapo waliendelea na chumba kingine master ambacho sasa ndo kilikuwa cha mwisho.
Kiongozi wa mtaa Bi Mwajua yeye anakubaliana na askari wa pili na anasema baada ya huko kwingine waliingia chooni ambapo hawakukuta chochote zaidi ya pampers zilizokuwa zimedondoka chini kisha wakaingia chumba master ambacho kilikuwa cha mwisho.
Hata hivyo anasema, wakati wako master askari mmoja akapokea simu ikiwataka warudi tena chooni ambapo walirudi na walipofika wakakuta mfuko wa nailoni wenye madawa ambao mwanzoni wakati wanapita haukuwepo.
Watuhumiwa wote wawili nao wanaungana na Bi Mwajua kuwa chooni walikuta pampers zikiwa zimedondoka chini wakaenda kupekua chumba master ambacho ndo kilikuwa cha mwisho, Wakati wako master askari mmoja waliyekuwa naye akapokea simu ikimtaka warudi chooni, na waliporudi wakakuta mfuko wa nailon wenye madawa ambao mwanzoni walipopita haukuwepo.
Zaidi, baada ya upekuzi huo watuhumiwa wote walikataa kusaini fomu/hati ya upekuzi Cerificate of Seizure kwakuwa waliamini yale madawa hayakukutwa ndani mwao.
Jaji Banzi anasema kutofautiana kwa maelezo ya askari kuhusu series ya upekuzi wa vyumba kunaleta shaka kuwa wanachosema watuhumiwa ni kweli.
Lakini pia Bi Mwajua naye alikuwa shahidi upande wa mashtaka lakini alikubali kuwa mwanzoni chooni hakukuwa na kitu ila baadae waliitwa na waliporudi wakakuta madawa.
Jaji anasema kuna uwezekano wa kupandikiza madawa kwenye nyumba ya watuhumiwa kwani hata wakati upekuzi unaendelea ndani ya nyumba, askari wengine walibaki nje wakizingira nyumba na walioingia ndani hawakuwa wamefunga mlango kutoruhusu mtu mwingine yoyote kutoka nje kuingia.
Kwahiyo kuna uwezekano mtu alitoka nje na mzigo na akauingiza ndani.
Kwa mkanganyiko huo Jaji anasema ushahidi una mashaka makubwa na kuna uwezekano mkubwa kuwa ulipandikizwa, na kwa msingi huo watuhumiwa wote waliachiwa huru tarehe 15/12/2020.
Tunayo ya kujifunza katika Matukio kama haya.