Ni kweli ni uwanja mzuri sana, mimi sio kwa kuona kwa picha tu bali nimefika katika uwanja huu. Lakini, tusijidharau sana kuwa Tanzania hatuna uwanja mzuri kwa kujilinganisha na wenzetu, lugha nzuri iwe 'ni mwanzo mzuri ila tunahitaji kusonga mbele.' Ukiangalia katika Afrika mashariki na kati, uwanja wetu Tanzania bado ni changamoto kwa wengi. Tunawasikia wengi wakisema, 'well done Tanzania, keep up the good work.' Cha muhimu tusijisahau tukafikiri ndo tumefika, tunahitaji kupiga hatua mbele ili tusiachwe na wakati.