Uwanja wa Taifa: Yanga 3 - 1 Stand united, ligi kuu soka Tanzania bara

Abubakar Abdallah

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
281
170
Wanajangwani mpoo? Leo tunaua tena , ili mikia wakija wacheze kwa presha ya juu, maana kwa kawaida ngoma ya watoto haikeshi..... Tukutane taifaa, emmmmyyytaaaa watani hawalali siku hizi naskia ...... Nimalizie kwa kutabiri Yanga 5 stand 0....

Lakini habari mnayo, maana mko macho kodo na roho juu kwa mechi za Yanga, na dua juu..... Mungu hua anampa mwenye akili na maarifa, hata mtokwe na povu vipi ubingwa mshaukosa. Tanbihi.. : Yanga 5 stand 0
Yanga.jpg

Kikosi cha Yanga​
Stand.jpg

Kikosi cha stand United​
Updates.....

34' Yanga 2, Stand United 0

=====

Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Young Africans waliowakaribisha wapiga debe wa Shinyanga Stand United 'chama la wana'

Katika mchezo huo Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam kuanzia saa 16:00 jioni.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Ally Ally aliyejifunga kenye dakika ya 7 kipindi cha kwanza, Ibrahim Ajibu dakika ya 12 na Obrey Chirwa dakika ya 85 ya kipindi cha pili, huku goli la kufutia machozi la Stand likitiwa kimiani na Vitalis Mayanga kwenye dakika ua 83.

Baada ya ushindi huo Yanga sasa wanafikisha alama 46 sawa na vinara Simba wao wakiwa na faida ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Katika chati ya msimamo Simba anaongoza bado akiwa na alama 46 kwa michezo 20 Yanga anafata kwa alama 46 akiwa na michezo 21, huku Azam Fc akiwa na alama 44 kwa michezo 22.
 
wewe unajiita shabiki hata timu hujui kuzitofautisha "Hivi kwa aikiliyako yanga anacheza na Singida leo?
 
. .... Wanajangwani mpoo? Leo tunaua tena , ili mikia wakija wacheze kwa presha ya juu,maana kwa kawaida ngoma ya watoto haikeshi..... Tukutane taifaa, emmmmyyytaaaa watani hawalali siku hizi naskia ...... Nimalizie kwa kutabir yanga 5 singid 0....
Nb: yanga vs stand..... 5 - O
 
. .... Wanajangwani mpoo? Leo tunaua tena , ili mikia wakija wacheze kwa presha ya juu,maana kwa kawaida ngoma ya watoto haikeshi..... Tukutane taifaa, emmmmyyytaaaa watani hawalali siku hizi naskia ...... Nimalizie kwa kutabir yanga 5 stand 0....
Lakini habar mnayo, mana mko macho kodo na roho juu kwa mechi za yanga, na dua juu..... Mungu hua anampa mweny akili na maarifa, mbumbumbu hata mtokwe na povu vipi ubingwa mshaukosa. Tanbihi.. : yanga 5 stand 0
Huu pia nao ni UJINGA. YANGA vs SINGIDA au YANGA vs STAND?
 
Back
Top Bottom