Uwanja wa Ndege Msalato kukamilika Mei

Uwanja wa Ndege Msalato kukamilika Mei

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,895
Reaction score
11,788
DODOMA: Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amewataka wadau wote wanaosimamia ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato kushirikiana ili ujenzi huo ukamilike ifikapo Mei mwaka huu.

Akizungumza jijini Dodoma, leo Januari 14, 2026 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi huo, Prof. Mbarawa amesema hatua ya ukamilishaji wa ujenzi (finishing), inahitaji umakini, kujali thamani ya fedha na ubora wa vifaa unaoendana na mahitaji.

"Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mamalaka ya Viwanja vya ndege (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) pamoja na Zimamoto na Uhamimiaji shirikianeni kikamilifu ili vifaa na mifumo ya uendeshaji isomane na kurahisisha utendaji wa kazi kiwanjani hapo," amesisitiza Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Zuhura Amani amesema wamejipanga kumsimamia kikamilifu mkandarasi anaejenga kiwanja hicho ili kikamilike kwa wakati.

Nae Mkurugenzi wa Kiwanja kiwanja hicho, Clemence Mbaruck amesema watahakikisha ujenzi unakamilika kwa viwango na tayari watumishi 170 tayari wameshahamishiwa Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi kwenye kiwanja hicho mara baada ya kufunguliwa rasmi.

Zaidi ya shillingi bilioni 370 zinatumika kwa ajili wa ujenzi huo na kukamilika kwake kutachochea ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa Dodoma kwani kutaruhusu ndege aina mbalimbali za kitaifa na kimataifa kutua kiwanjani hapo.

Source
#HabarileoUPDATES

________________
Japo sielewi serikali itafanyaje ili kusaidia hii Msalato Airport iwe na flight za kutosha maana watu wengi Tanzania wanatumia mabasi, na wale wanaosafiri kutoka nje mara nyingi wanatua Dar es Salaam, Arusha au Zanzibar. Mikoani safari ni chache ndio maa kunakuwa na viwanja vidogo.
Kwa hiyo serikali inapaswa kuipa sababu jiji la Dodoma kupata safari nyingi za ndege ili uwanja mkubwa kama huu usiwe na flights za kuhesabu, bali iwe one of the busiest airports in the region
1768453079369.jpg
1768453085863.jpg
1768453092198.jpg
1768453099913.jpg
1768453115428.jpg
 
Hizi ndio habari ambazo makonda anataka ziwe zinaripotiwa kwenye media za kimataifa!!! Hahaa
 
Hizi ndio habari ambazo makonda anataka ziwe zinaripotiwa kwenye media za kimataifa!!! Hahaa
Hapana, ni habari tu nimeweka ili watu wajue. Inabidi tujue yanayoendelea nchini kuanzia mazuri mpaka mabaya. Ichukulie kama habari tu ya kinachoendelea nchini kwako, sio part ya siasa
 
Hapana, ni habari tu nimeweka ili watu wajue. Inabidi tujue yanayoendelea nchini kuanzia mazuri mpaka mabaya. Ichukulie kama habari tu ya kinachoendelea nchini kwako, sio part ya siasa
Nimekuelewa, ila nilikuwa nawaza kwa sauti tu kwamba jamaa amesema ataunda kitengo Cha kuhakikisha habari za Tz zinarushwa na vyombo vya kimataifa. Maana CNN, bbc, DW, al Jazeera nk waliporusha mauaji ya mo29 walisema wa wivu na Tz. May be hiyo habari uliyoweka ndio serikali inataka zirushwe CNN.
 
Hahaha sawa nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom