Uwanja wa Ndege JKN - Mambo ya kijinga hayaishi

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
14,660
11,678
Wanabodi jioni ya tarehe 12th Feb 2016 nimefanikiwa kufika uwanja wa Ndege wa DSM kitu kilichonishangaza hakuna sehemu za kuketi kusubiria abiria, ila Madereva wa Taxi wamehodhi Mabenchi yote sijaelewa yale ni kwa ajili yao tu au kwa ajili ya Wanaosubiria Wageni maana wanakaa wao tu.

Tatizo la Viwanja vyetu ratiba za ndege ni mbovu ajabu unaweza fika kumpokea mgeni on time unaambiwa ndege haijatua na muda ushatimia unaambiwa kuna delay yaani ishakuwa kawaida.. Sasa Usumbufu unaupata gharama za Parking zinaongezeka maan kwa lisaa ni 2,000/= na kwa ukisimama na ukachoka ukaamua ukaketi garini kuna Askari wanakataza watu kubakia ndani ya magari hata iwe Dereva... Sehemu ya Kupokelea Abiria hakuna sehemu ya kuketi je mtu asimame kwa zaidi ya masaa hata mawili? na wageni wengine wanatua nchi hawafahamu pa kufikia hadi awepo mwenyeji nao wakifika wasipompata mwenyeji husbiria kwa kusimama hii ishakuwa ni mateso ya lazima kwa wananchi na wasio raia ni aina mojawapo ya kukiuka haki za binadamu,

yapata miezi wiki kadhaa nyuma zilikuwepo sehemu za kusubiria abiria japo ni chache now hakuna hata moja.. Waziri husika naomba uchukue hatua kama unamcha Mungu. Ujinga pale hauishi usipokuta Omba omba basi utakuta vyoo hovyo au chochote tu kile.
IMG_20170212_165526.jpg
IMG_20170212_165253.jpg

Raia kasubiri hadi kachoka kaamua kuchuchumaa... je huu ni Uungwana? Pembeni Mzungu kakalia Air Condition akishangaa nchi ya Vi wonder
IMG_20170212_165246.jpg

Hadi vikidi havina jinsi
IMG_20170212_165239.jpg

Madereva Taxi waliohodhi Mabenchi wakivizia Abiria yeyote
IMG_20170212_165204.jpg

Wenye mabenchi yao japo nayo yamechoka mbaya
IMG_20170212_165155.jpg

Hata kama tunajengewa uwanja mwingine Wekeni sehemu za kukaa hatuingii bure uwanjani kwenu alaa... au hadi Raisi Aseme? mhusika jitume... Tujifunze Rwanda kila mtu anawajibika eneo lake la kazi.
IMG_20170212_165454.jpg

Eneo hili lilikuwa na Benchi karibu na kiduka nalo limetokomea kusiko julikana kwa roho mbaya za baadhi ya watu
 
Sasa yale yaliyokuwepo yamegawanwa kupelekwa mahome kwao?
Wacmamiz hamna kila mtu bize na tumbo lke,unafikiri hawaoni au hawajui mkuu??tz ni zaidi ya uijuavyo acha movie iendelee!! karbu mkuu tupunguze stress!!!
 
Wacmamiz hamna kila mtu bize na tumbo lke,unafikiri hawaoni au hawajui mkuu??tz ni zaidi ya uijuavyo acha movie iendelee!! karbu mkuu tupunguze stress!!!
Mida hii:eek: Asubuhi ni Job Mkuu! hata hivyo thanks mkuu Siku Nyingine mwanzo wa Weekend!
 
Mida hii:eek: Asubuhini Job Mkuu! hata hivyo thanks mkuu Siku Nyingine mwanzo wa Weekend!
pa1 mkuu,naamin wahusika wanapitia hpa na wanaona tatizo ujeuri tyu hdi wafanyiwe ziara ndo wanaamka inakera xana!!uxku mwma mkuu!!
 
Wanabodi jioni ya tarehe 12th Feb 2016 nimefanikiwa kufika uwanja wa Ndege wa DSM kitu kilichonishangaza hakuna sehemu za kuketi kusubiria abiria, ila Madereva wa Taxi wamehodhi Mabenchi yote sijaelewa yale ni kwa ajili yao tu au kwa ajili ya Wanaosubiria Wageni maana wanakaa wao tu.

Tatizo la Viwanja vyetu ratiba za ndege ni mbovu ajabu unaweza fika kumpokea mgeni on time unaambiwa ndege haijatua na muda ushatimia unaambiwa kuna delay yaani ishakuwa kawaida.. Sasa Usumbufu unaupata gharama za Parking zinaongezeka maan kwa lisaa ni 2,000/= na kwa ukisimama na ukachoka ukaamua ukaketi garini kuna Askari wanakataza watu kubakia ndani ya magari hata iwe Dereva... Sehemu ya Kupokelea Abiria hakuna sehemu ya kuketi je mtu asimame kwa zaidi ya masaa hata mawili? na wageni wengine wanatua nchi hawafahamu pa kufikia hadi awepo mwenyeji nao wakifika wasipompata mwenyeji husbiria kwa kusimama hii ishakuwa ni mateso ya lazima kwa wananchi na wasio raia ni aina mojawapo ya kukiuka haki za binadamu,

yapata miezi wiki kadhaa nyuma zilikuwepo sehemu za kusubiria abiria japo ni chache now hakuna hata moja.. Waziri husika naomba uchukue hatua kama unamcha Mungu. Ujinga pale hauishi usipokuta Omba omba basi utakuta vyoo hovyo au chochote tu kile.View attachment 469917 View attachment 469918
Raia kasubiri hadi kachoka kaamua kuchuchumaa... je huu ni Uungwana? Pembeni Mzungu kakalia Air Condition akishangaa nchi ya Vi wonderView attachment 469920
Hadi vikidi havina jinsi View attachment 469921
Madereva Taxi waliohodhi Mabenchi wakivizia Abiria yeyote View attachment 469922
Wenye mabenchi yao japo nayo yamechoka mbaya View attachment 469924
Hata kama tunajengewa uwanja mwingine Wekeni sehemu za kukaa hatuingii bure uwanjani kwenu alaa... au hadi Raisi Aseme? mhusika jitume... Tujifunze Rwanda kila mtu anawajibika eneo lake la kazi.View attachment 469926
Eneo hili lilikuwa na Benchi karibu na kiduka nalo limetokomea kusiko julikana kwa roho mbaya za baadhi ya watu
Wewe ni kati ya wapumba mnaoenda airport kuangalia ndege Kama uko sabasaba. Unalalamika ndege kuchelewa,unajua sababu inayopelekea ndege kuchelewa !? Gari umeazima kwa shemeji unaleta mbwembwe hapa JF.
 
Interesting....
 
Analalamika kukosekana kwa mabenchi ya kukalia watu wanaosubiri wageni wao. Ndege inaweza kuchelewa ila kusubiri umesimama muda mrefu ni mateso. Vitu vingine kukosekana airport ni aibu.
 
Wewe ni kati ya wapumba mnaoenda airport kuangalia ndege Kama uko sabasaba. Unalalamika ndege kuchelewa,unajua sababu inayopelekea ndege kuchelewa !? Gari umeazima kwa shemeji unaleta mbwembwe hapa JF.

Kwa fikra hizi na kwa kutokusoma na kuelewa hakika bado tuna safari ndefu sana kutoka hapa tulipo. Mleta uzi anaongelea vitu vya kujenga wewe umeona ni upuuzi!
 
Wewe ni kati ya wapumba mnaoenda airport kuangalia ndege Kama uko sabasaba. Unalalamika ndege kuchelewa,unajua sababu inayopelekea ndege kuchelewa !? Gari umeazima kwa shemeji unaleta mbwembwe hapa JF.
Acha ushamba dogo
 
Naam Mkuu Adharusi sikuwa nimeona kama umeniita,nimeamka kuwahi kiti cha mbele kwenye list ya Makonda huku Chimala Street.
Kwanza nimsahihishe kidogo mkuu Mlaleo ,uwanja wetu hauitwi JKN (nafikiri alimaanisha JULIUS KAMBARAGE NYERERE) bali uwanja wetu unaitwa JNIA (JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT)

Kuhusu suala la mahali pa kukaa,si tu kwa wanaosubiria abiria,bali hata kwa wale wanaosindikza wageni au wale abiria wanaotakiwa kuondoka wakiwa bado eneo la Landside wanakuwa hawana pa kukaa.Pale eneo la kusindikiza abairia,kuna vibenchi vya kukaa watu kama 25 tu,sasa jiulize abiria wanaoondoka wako wangapi?sio rahisi wote wakae...lkn wapunguze tatizo kidogo.

Tatizo mkuu ni ufinyu wa kiwanja,lkn pia tatizo la pili ni management!Pale wapo watu wapigaji tu,ndio maana tumekuwa tunamwambia Prof Mbarawa afanye mabadiliko makubwa pale,wale watu wa juu ni wizi mtupu.Eneo lote la kupumzikia badala ya kuweka mabenchi wamegawa kama vizimba kwa rushwa na kujinufaisha.

Wale madereva tax ni deal ile,wanalipa mamlaka ada za kuwa na tax pale,ni mradi wa watu ule.Eneo la mapumziko lilipaswa kuwekwa mabenchi ndio hiyo wamejenga kimgahawa cha yule Mama wa Kichina,eneo lote lile liliotakiwa kuwa wazi kwa mabenchi na mapumziko ndio imewekwa ile famasi,duka la kubadili fedha,supermarket ya mhindi,kiduka cha vifanyago na Stationery!!Hii haipo hata kwenye ramani ya jengo,ni ufisadi na wizi.

Usiishie hapo nje,panda kule International Lounge ukiwa unasafiri,watu wamegawiwa vizimba vya biashara mpaka sehemu za kukaa abiria,matokeo yake ni kubanana na joto juu!!Juzi nimepita naenda South nakuta eti wameweka na huduma ya massage mahali ambapo palikuwa na mabebchi,matokeo yake,wakati wa "peak hours" abiria wanakosa pa kukaa wanasimama....Management ni hovyo sana hapo JNIA

We angalia hapo pembeni ya Mzungu,hilo bango lilipaswa kuwa juu limetundikwa lkn limelazwa chini,na watu wanapita tu bila kuchukua hatua na wanaona kawaida!Pembeni ya hilo bango kuna kidumu cha lita 5 kimewekewa mrija toka kwenye AC...Kinajaa maji kinaanza kumwaga eneo lote linakuwa na maji tepetepe!!Hii ni aibu sana!!
 
Labda Terminal III watalifanyia kazi. Ni jambo la ajabu sana. Ma Taxi driver wamehodhi ile sehemu.

Ukizidiwa lazima uende sehemu ya departure ujifanye na wewe ni msafiri ili ukae hapo ili kuvuta muda
 
Back
Top Bottom