Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,356
Kuna haja kubwa kwa Shirikisho la soka Tanzania, TFF kuuchunguza upya uwanja wa Mabatini unaotumiwa na timu ya Ruvu Shooting ya mkoni Pwani kufuatia unyanyasaji mkubwa kwa raia unaofanywa na askari wa kambi iliyopo uwanjani hapo.
Mashabiki zaidi ya 90 wa Mbeya City waliokuwa uwanjani hapo kwa ajili ya kuishangilia timu yao kama wanavyofanya kwenye michezo mingine inayoihusisha timu yaojana walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kundi kubwa la askari kuwavamia na kuanza kuwashushia kipigo pasipo sababu ya msingi.
Tukio lilianza pale mashabiki hao wa City waliokuwa wakishangilia kwa nguvu muda wote ili kuchagiza ushindi kwa timu yao walipoamua kwenda kwenye goli ambalo mlinda mlango wao David Buruhani alikuwepo kwa lengo la kumhamasisha kufuatia mara kwa mara kuwa akibughudhiwa na mashabiki wa Ruvu ambao ni askari waliokuwa wamevaa kiraia ndipo wanajeshi wengine waliokuwa na sare walipokimbia haraka upande huo na kuanza kutoa kipigo kwa mashabiki wa City.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mashabiki hao wamesema kuwa hawaelewi sababu ya askari hao kuanza kuwashambulia alhali hakukuwa na fujo yoyote iliyoashiria uvunjifu wa amani zaidi ili ni nguvu ya kushangilia waliyoitoa wao kwa lengo la kuhamasisha ushindi na kumlinda kipa wao aliyekuwa akisumbuliwa na askari waliokuwa wamevaa kiraia.
Huu uwanja siyo sehemu salama tena kwa soka wanajeshi wanatumia nguvu kubwa kuwanyanyasa raia, kuna haja TFF kuutazama upaya uwanja huu, timu inayocheza hapa ni ya jeshi hivyo kwa vyovyote lazima raia watanyanyasika. walisema mashabiki wa City.
Hakika ni jambo la hatari kwenye soka letu kwani linaweza kusababisha uwepo wa kuliziana kisasi kwa mashabiki kila timu inakuwa kwenye uwanja wa nyumbani hivyo kuchafua sura nzima ya mpira wa Tanzania.
Tovuti Rasmi ya Mbeya City