Uvutaji wa Sigara Tanzania na Kansa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvutaji wa Sigara Tanzania na Kansa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sipo, Nov 12, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwanini Tanzania tusiwe serious katika kuhakikisha kuwa wavuta sigara hawafanyi hivyo katika public places? Kwa mujibu wa takwimu wa ongezeko la Kansa Tanzania zilizotolewa na Dr. Ngoma sababu kubwa ni uvutaji wa sigara ambako asiyevuta lakini hukutana na moshi wa sigara ndie mwathirika mkubwa na aweza kupata kansa kwa urahisi zaidi.
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kuna sheria ya uvutaji nafikiri! Maana kwenye public transport, na Maofisini hakuna uvutaji na kama upo kuna vyumba maalum vimetengwa kwa matumizi ya uvutaji. Kwenye kumbi za starehe pia kuna smoking rooms! Mikakati ipo ila labda ufuatiliaji upo usingizini
   
 3. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Niliweka hii thread makusudi kutokana na aina ya maisha tuyoishi huku kwenye mitaa yetu. Tunasema tuna sheria ya kuzuia uvutaji kwenye public lakini ni wangapi wanafahamu kuhusiana na hii sheria kwa maana ile ile ya wavutaji na wasiovuta. Je ni vyombo gani vinahusika mtu anapovunja sheria hii makusudi kwa kuvuta sigara kwenye basi/hiace au sehemu nyingine yoyote yenye watu wengi au hata wachache lakini wanaathirika na uvutaji huo.
  La pili ni kama alivyoandika Kimbweka kuhusiana na kuwepo sehemu za kuvutia sigara kwa mfano sehemu za starehe. Lakini swali langu ni kuwa ni sehemu gani hizo zenye hivyo vijumba vya kuvutia sigara? Si sehemu zile ambazo ni kubwa na wanazokwenda watu wenye uwezo mkubwa tu? Je kwenye bar hizi za mtaani ambazo umekaa kiti cha nyuma mtu anakuja anakaa kiti cha mbele yako anaanza kuvuta sigara kwa madaha na ukimwambia tafadhali sio vizuri kuvuta hapa manake huu moshi una athari kwangu na wengine wasiovuta yeye kwa kiburi anakujibu anakwambia nenda popote unapotaka mimi naendelea kuvuta.
  Sasa ukijaribu ku-link mambo yote haya unaona kabisa kuwa kuna tatizo sehemu hasa kwenye upande wa enforcement ya sheria zinazotungwa. Lakini hali hii ni tofauti na wenzetu a nchi zinazoendelea kama ya kwetu ambao wana sheria kama hizi na watu wameelezwa vya kutosha kuhusiana na sheria hii na waende wapi anapotokea mtu kuivunja sheria hii. Mfano mzuri ni hapo Kenya kwenye Jiji la Nairobi ambako hii sheria kwa kiasi fulani wamejaribu kuitekeleza. Kwa mfano hivi vibanda vya kuvuta vimewekwa sehemu mbali mbali Jijini ili yule anayetaka kuvuta aingie mule avute na kuondoka zake. Kule ni kosa hata kuvuta ukiwa unatembea mwenyewe barabarani na ukikutwa sheria inachukuwa mkondo wake hapo hapo.
  Sasa hapa kwetu mambo ni tofauti kabisa tunaogopana wenyewe kwa wenyewe hata wale wanaovuta wanaona ni sawa tu.
  Tujrekebishe jamani ndugu zangu tuache ujinga na upumbavu kwa wale wanaovuta sigara ovyo. Na naitaka serikali na asasi za kiraia kuhakikisah kuwa wananchi wanaifahamu hii sheria kwa undani na kuweza kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya kansa na mengineyo yanayotokana na uvutaji wa sigara.
  NB: Binafsi nachukizwa sana na uvutaji wa sigara hasa kwa wale wanaovuta sigara pasipo kuangalia sehemu walipo na wanathiri vipi wengine. Kama wewe ni mwanaJF na mvutaji wa sigara husiyefuata sheria na kuheshimu afya za wengine ni mbaya sana na inabidi ulaaniwe na jamii ya Kitanzania na Kimataifa. Vuta sigara kwa faida yako na uheshimu afya za wengine nawe utaheshimika siku zote.
   
Loading...