Uvutaji wa sigara kwenye umati wa watu ungepigwa marufuku na adhabu kali itolewe kwa wakiukaji

Still88

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
351
228
Habari zenu wana jamii forum!
Kuna suala moja mie linanikera sana ambalo nimeona kupitia jamii forum wenda ikafikia wahusika na maisha yakawa yenye furaha.

Suala lenyewe ni hili la uvutaji wa sigara, siku hizi ishakuwa kero. Unakuta mtu ananunua kwa raha zake ili kujipa raha mwenyewe lakini kinachonikera hapa ni kuvuta bidhaa hiyo ya hatari hadharani na muda mwingine mbele za watu ambao hawapendi SIGARA. Binafsi naona sio ustaarabu na ni kuharibu raha ya wengine.

Ikumbukwe kuwa sigara inatokana na zao la tumbaku ambalo lina nicotine. Kemikali hiyo inahusianishwa na usababishaji wa kansa ya aina yeyote mwilini kitaalamu. Kwa kuvuta hadharani katikati ya umati wa watu ina maana mtumiaji anaweka idadi ya watu maelfu na elfu katika hatari ya kupata kansa na madhara mengine yatokanayo na uvutaji wa moshi wa sigara.

Binafsi nlikuwa naziomba mamlaka husika za serikali kuliangalia hili kwa upana wake ili kunusuru idadi kubwa ya wanajamii kutoka kwenye madhara ya sigara. Inabidi kama wanapenda kuuza sigara basi wajenge sehemu maalumu ambamo wavuta sigara watakuwa wakikutania humo ili kufanya yao bila kuathiri afya zawengine wasio na hatia. Uwe mvuta tumbaku pia ni humo humo. Na iwekwe sheria kali kwa yeyote atayekamatwa akivuta sigara kwenye umati wa watu ama barabarani ili tuheshimiane.
Kwa kweli sigara ina madhara makubwa ambayo siwezi kueleza yote hasa hili la kansa maana kansa haiponi kirahisi na matibabu yake ni ya ghali na idadi kubwa ya watanzania hawawezi kumudu.

Kwa yeyote anayehusika afikirie juu ujumbe huu kwa manufaa ya Taifa lenye afya njema.
Mungu awabariki.
 
Back
Top Bottom