Jamaa baada ya kuona anapata shida kusali kila ukifika mda wa kulala maana sala yake ilikuwa ndefu akaona ni bora aiandike kisha akaibandika ukutani, ikiwa ikifika mda wa kusali anasema ''Eeeh Mungu Kama kawaida Hapo ukutani'' Ameen.
Mkuu,ile kujitoa kumuomba Mungu wako ina umuhimu sana"ombeni bila kukoma" na hata kukata usingizi mara nyingine mfano usiku wa manane au alfajiri sana ni muhimu kwani umeutesa mwili wako kwa ajili ya Muumba wako,ndio maana wengine wanafunga,hakika kwa kufanya hayo Mwenyenzi Mungu atajibu uyaombayo,Ila pia IMANI ni muhimu iambatane na maombi hayo.