UVCCM Wamjibu Zitto Kabwe

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1-16.jpg

Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji, Sera, Utafiti na Mawasiliano, Abubakar D. Asenga

Nimeona taarifa ya Kaka Zitto kabwe akielezea hoja zake kwa msingi wa kukana kumhujumu Rais Magufuli na kuwa waliotoa taarifa hizo wanatumiwa na mmoja wa Mawaziri ( ) wa Serikali ya awamu ya tano.

Kaka Zitto ameenda mbali zaidi akiandika,namnukuu

“Maneno hayo yanaenezwa na watu wanaotumwa na Waziri(anamtaja jina) nina ushahidi usio na mashaka wa waziri ( ) kupanga vijana wanaojiita wa UVCCM kufanya Mikutano na waandishi wa habari na anawalipa fedha kufanya hivyo” mwisho wa nukuu.

Mosi, nimpongeze Mh. Zitto Kabwe kukana kwa sauti ya juu kabisa kuwa hampingi Rais Magufuli na anamuunga mkono katika Ujenzi wa Nchi kama alivyofanya kwa Serikali ya awamu ya nne. Kama ni kweli na lipo kwa matendo Ni jambo jema sana kwa maslahi ya nchi yetu ambalo wapinzani wengine wanapaswa kuliiga.

Pili, Nimthibitishie pasi na shaka ndugu Zitto Kabwe kuwa Vijana hao kama alivyosema (wanajiita wa UVCCM) ni wanajiita tu.

Vijana wa CCM kama Jumuiya imara ya Vijana wa Tanzania haiwezi kutumika na kulipwa pesa na mtu ili kutumika kwa maslahi binafsi.

Na kwa kuwa ndugu Zitto amelisema jambo hili kwenye umma na kuwa anao ushahidi wa hao wanaojiita wa UVCCM, tupo tayari kushirikiana nae na ikithibitika kuchukua hatua zaidi kwa mujibu wa Kanuni yetu, vinginevyo tunaona jina la Jumuiya yetu linatumika kama Nyanya kwenye mboga za watu, na hatutakubali hilo.

Tatu. UVCCM inaimani kubwa na Rais Magufuli kuwa hawezi kuwa mtetezi wa Majipu ata kama mwenye jipu kwa madai yako ni rafiki yake, na UVCCM ni kisu cha kumsaidia Rais kutumbua majipu hayo.

Lakini tunajua kuwa Rais Magufuli ni Rais makini katika atua anazochukua pasi na kumuonea mtu, kwa kuwa kutumbuliwa jipu kunamaumivu makali sana yanayoweza kuvumiliwa tu na mwenye jipu, asiekuwa na jipu hawezi kutumbuliwa.

Hivyo kama kweli tuhuma hizo zinazotolewa kwa Waziri huyo zina ukweli na zinahusu rushwa na ufisadi Rais angeshamtumbua waziri ama atakuja kumtumbua tu ikishathibitika, tusiwe na haraka,"haraka haraka haina baraka"

MWISHO.
Ushauri kwa kaka Zitto Kabwe, kwa kuwa yeye ni Mbunge na Waziri anaemtuhumu anaingia Bungeni basi ni vizuri akatumia jukwaa hilo kuweka ushahidi wa hoja zake ili zipate majibu ya kina na anaetuhumiwa, kwani naye atakuwa na fursa ya kujibu kwa hoja na ushahidi.

UVCCM tunachotaka ni mazingatio ya maslahi ya watanzania hasa wengi ambao bado ni masikini.

Tumeendelea mara zote kuwaomba kupata habari sahihi za jumuiya na kuepuka uzushi unaofanywa mara kwa mara kuichafua jumuiya yetu,

UVCCM hutoa taarifa zake kwa utaratibu wake wa kanuni chini ya Mwenyekiti SADIFA JUMA HAMIS kama msemaji Mkuu ama Makamo Mwenyekiti wake Bi.MBONI MHITA ama Kaimu Katibu mkuu SHAKA HAMDU SHAKA au Kaimu katibu wa Idara ya Uhamasishaji,Sera, Utafiti na Mawasiliano Mr Abubakar Asenga, pia Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu MFAUME KIZIGO

Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ndugu ABDUGHAFAR IDRISSA ama itakavyoelekezwa vinginevyo


Kwa lolote wasiliana nasi kwa

email.uvccm1978@gmail.com

simu - 0627 968 722 AU 0222150743.


imetolewa na.

Abubakar D. Asenga

Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji, Sera, Utafiti na Mawasiliano

UVCCM MAKAO MAKUU

S.L.P 19989

DAR ES SALAAM

April 20,2016
 
Haka kahamaa kanaandika lugha ya wale watoto wa gazeti la sani .tena huyu dogo olevwake asije akakutana na mzee kifimbo cheza
 
Wale wa lumumba jana walikuja na povu kuuubwa kukosoa taarifa ya meya wa Dar kuwa andiko halina mashiko, arudi shul, leo kimyaaaa, wapo kama wamenyeshewa , CCM kweli kama nia ni kuelimishana na upande wenu ukikosea mkosoane pia,.
 
Acha kutudanganya Asenga. Inakuwaje mtu atumie jina la jumuiya ya chama tawala kutoa tamko kali linalowataja kwa majina wabunge 3, halafu akaachwa tu. Kama ndivyo basi hiki chama tawala kina shida kubwa sana, hakifai.
Kosa kubwa kama hilo unasubiri mpk Mbunge alalamike ndipo ukanushe. Tena unatoa kanusho pasipo kuonyesha ni kwa jinsi gani umeguswa ama kuudhiwa na kitendo dhalimu kama hicho kinachopaka matope chama chako.
Tafsiri yake ni kwamba, hao wanaojiita uvccm, ni uvccm halisi. Kuna mchezo unachezwa ndiyo maana hata chama chako hakijawachukulia hatua za kisheria. Asenga kajipange tena.
 
'Rais hatatoka kaskazini' ... Ndugu Asenga kuliko uwepo huko CCM bora uache siasa ukafanye biashara. Tayari hapo ulipo ni first disqualification.
 
Nimeshangaa sana tamko la umoja wenye hadhi hii hawajui kuandika maneno simple ya kiswahili kama hatua (anaandika atua), hata (anaandika ata.)
Sio hawa peke yao, humu JF haya maandishi ya aina hii ni mengi mpaka kuna siku najihisi kuwa labda nimepitwa na wakati. Ndio maaana kuna siku mtu aliandika "muhandisi" badala ya "muandishi" na uzi ukawa mrefu bila sababu ya msingi. Hili sasa limekuwa gonjwa.
 
Acha kutudanganya Asenga. Inakuwaje mtu atumie jina la jumuiya ya chama tawala kutoa tamko kali linalowataja kwa majina wabunge 3, halafu akaachwa tu. Kama ndivyo basi hiki chama tawala kina shida kubwa sana, hakifai.
Kosa kubwa kama hilo unasubiri mpk Mbunge alalamike ndipo ukanushe. Tena unatoa kanusho pasipo kuonyesha ni kwa jinsi gani umeguswa ama kuudhiwa na kitendo dhalimu kama hicho kinachopaka matope chama chako.
Tafsiri yake ni kwamba, hao wanaojiita uvccm, ni uvccm halisi. Kuna mchezo unachezwa ndiyo maana hata chama chako hakijawachukulia hatua za kisheria. Asenga kajipange tena.
Project ZZK
 
Haka kahamaa kanaandika lugha ya wale watoto wa gazeti la sani .tena huyu dogo olevwake asije akakutana na mzee kifimbo cheza
sasa na wewe hapa unakosoa kitu gani wakati na wewe ni walewale mliokunywa uji wa mgonjwa?
 
sasa na wewe hapa unakosoa kitu gani wakati na wewe ni walewale mliokunywa uji wa mgonjwa?
Hawa jamaa sio ndio walimu wetu wa viswahili wa bongo.....anamsahihisha mtu na huku yeye anakosea....haya mambo nayooo

Sent from my HUAWEI Y330-U01 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo hilo tamko lina hiyo picha? Au ni njia ya kumfanya JPM avute taswira ya mtoa tamko ili akunbuke kuwa waliwahi kukutana somewhere? Ukuu wa wilaya buana!
 
View attachment 341378
Nimeona taarifa ya Kaka Zitto kabwe akielezea hoja zake kwa msingi wa ....
----------------------------------------------------------------------------------------------
Kaka Zitto ameenda mbali zaidi akiandika,namnukuu ...
-----------------------------------------------------------------------------------------------
Ushauri kwa kaka Zitto Kabwe, kwa kuwa yeye ni Mbunge na Waziri anaemtuhumu anaingia Bungeni basi ni vizuri
Tamko gani la taasisi linaweza kuonyesha uhusiano binafsi kwa kuandika 'kaka' badala ya formal 'Mheshimiwa'? Tamko gani la taasisi linaweza kubandikwa picha ya mtoa tamko? nadhani Asenga angeweza kumuandkia tu Zitto kwenye instagram
 
Back
Top Bottom