UVCCM walaani wanasiasa kuhamasisha uvunjaji wa sheria

R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,294
Points
2,000
R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,294 2,000
[h=2][/h] UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mwanza kimelaani tabia ya wanasiasa kuhamasisha wananchi kutotii sheria. Akizungumza mjini hapa jana, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Elias Mpanda, alisema wamesikitishwa na tukio la mauaji lililotokea katika vurugu zilizoibuka katikati ya Jiji la Mwanza baina ya Wamachinga na mgambo wa Jiji na kusababisha kifo cha mtu mmoja pamoja na majeruhi watatu.

Alisema vurugu za namna hiyo zimekuwa zikitumiwa na wanasiasa kujitafutia umaarufu kwa kuchochea wananchi kutotii sheria zilizopo, pamoja na mamlaka halali hali inayojenga chuki baina ya wananchi na Serikali yao.

“Vurugu zilizotokea na kusababisha kifo ni sehemu ya uchochezi ambao umekuwa ukifanywa na wanasiasa kwa malengo binafsi, katika hili muda mfupi mtawasikia wamejitokeza kwa ajili ya kusaka umaarufu.

“Nchi inaongozwa na utaratibu wa sheria hivyo naomba ndugu zangu Wamachinga kufuata utaratibu uliwekwa na jiji waweze kufanyia biashara zao katika maeneo yaliyoruhusiwa na si vinginevyo,” alisema Mpanda.

Alisema UVCCM imesikitishwa na vurugu hizo zilizosababisha kifo cha mpiga debe aliyepigwa risasi kwa bahati mbaya na kueleza kuwa mtaji wa mwanasiasa makini ni watu.

Kuhusu mgambo wa jiji kuhusika katika tukio hilo, alisema UVCCM haitaki kuona mgambo wasio waaminifu wanaendelea kuwa chini ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutaka waondolewe mara moja kwa kuwa hawafai.

Alisema baadhi yao wamekuwa vinara wa kupokea rushwa na kukamata mali za Wamachinga na kuziuza na wakati mwingine wamekuwa wakizichukua na kuzipeleka nyumbani kwao kwa matumizi yao.

“Tunajua wanachofanya sio maagizo ya wakubwa wao kikazi, bali ni tamaa binafsi, kuna mgambo mmoja wa jiji ambaye amekuwa akichukua mali za Wamachinga na kuzipeleka kwake na kuna wakati alikamata blanketi za Mmachinga na walipofuatilia nyumbani kwake walizikuta zikitumiwa,” alisema Mpanda.
 
S

Savannah

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
239
Points
0
Age
67
S

Savannah

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
239 0
UVCCM hawana cha kusema. JK amekiri jinsi CCM na Serikali yake walivyokuwa wakitumia Polisi kuzibiti wapinzani na matokeo tumeyaona.
 
Ciril

Ciril

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Messages
6,913
Points
2,000
Ciril

Ciril

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2011
6,913 2,000
[h=2][/h] UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mwanza kimelaani tabia ya wanasiasa kuhamasisha wananchi kutotii sheria. Akizungumza mjini hapa jana, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Elias Mpanda, alisema wamesikitishwa na tukio la mauaji lililotokea katika vurugu zilizoibuka katikati ya Jiji la Mwanza baina ya Wamachinga na mgambo wa Jiji na kusababisha kifo cha mtu mmoja pamoja na majeruhi watatu.

Alisema vurugu za namna hiyo zimekuwa zikitumiwa na wanasiasa kujitafutia umaarufu kwa kuchochea wananchi kutotii sheria zilizopo, pamoja na mamlaka halali hali inayojenga chuki baina ya wananchi na Serikali yao.

“Vurugu zilizotokea na kusababisha kifo ni sehemu ya uchochezi ambao umekuwa ukifanywa na wanasiasa kwa malengo binafsi, katika hili muda mfupi mtawasikia wamejitokeza kwa ajili ya kusaka umaarufu.

“Nchi inaongozwa na utaratibu wa sheria hivyo naomba ndugu zangu Wamachinga kufuata utaratibu uliwekwa na jiji waweze kufanyia biashara zao katika maeneo yaliyoruhusiwa na si vinginevyo,” alisema Mpanda.

Alisema UVCCM imesikitishwa na vurugu hizo zilizosababisha kifo cha mpiga debe aliyepigwa risasi kwa bahati mbaya na kueleza kuwa mtaji wa mwanasiasa makini ni watu.

Kuhusu mgambo wa jiji kuhusika katika tukio hilo, alisema UVCCM haitaki kuona mgambo wasio waaminifu wanaendelea kuwa chini ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutaka waondolewe mara moja kwa kuwa hawafai.

Alisema baadhi yao wamekuwa vinara wa kupokea rushwa na kukamata mali za Wamachinga na kuziuza na wakati mwingine wamekuwa wakizichukua na kuzipeleka nyumbani kwao kwa matumizi yao.

“Tunajua wanachofanya sio maagizo ya wakubwa wao kikazi, bali ni tamaa binafsi, kuna mgambo mmoja wa jiji ambaye amekuwa akichukua mali za Wamachinga na kuzipeleka kwake na kuna wakati alikamata blanketi za Mmachinga na walipofuatilia nyumbani kwake walizikuta zikitumiwa,” alisema Mpanda.
Wamesema tu ili na wao waonekane wapo kazini,mauaji ya kikatili yanayofanywa kila siku na jeshi la polisi yanabakia kukemewa kwa maneno unafikiri hiyo ndio njia sahihi ya uwajibikaji?Tutashuhudia mauaji mengi zaidi hakuna jipya,umesikia juu ya operesheni iliyoanzishwa ya "okoa mazingira"inavyoleta madhara kwa maovu yanayofanywa na polisi dhidi ya wananchi wa Tanzania?
 
Forum statistics

Threads 1,296,014
Members 498,494
Posts 31,230,721
Top