UVCCM waivaa UKAWA

ray jay

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
1,084
Reaction score
485
"Demokrasiabila mipaka ni ukichaa na demokrasia bila nidhamu ni uwendawazimu"Mwl Jk Nyerere


Ndugu zangu Watanzania, naomba mfahamu kuwa miongoni mwa wajumbe wote wabunge la katiba takriban 600, wajumbe waliofanya maamuzi haramu yakugomea ni 79 ambao ni pungufu ya asilimia 15% ya wajumbe wote, nasio kweli kuwa wao pekee ndio wenye tafsiri sahihi ya rasimu. Wajumbe wa makundi mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa vyama vyote vya siasa takriban 18 kati ya 22 bado wamo kwenye bunge, kati ya wajumbe wakundi la 201 walioasi ni 15 ambapo bara ni 9 na zanzibar 6 lakini piakatika wanaojiita UKAWA wapo wabunge ambao wameendelea kurudi bungeni kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa. Takwimu hizizinatuthibitishia kuwa UKAWA ni kikundi kidogo cha watu waliojipangakuvuruga AMANI ya nchi, watu ambao hawataki KATIBA wala hawatakiMUUNGANO.

Nduguzangu Watanzania, naomba leo niwape picha na kilichopo nyuma ya pazia ya kikundi hiki kiitwacho UKAWA ambacho kinaratibiwa na viongoziwachache na maslahi yake kujulikana kwa wachache zaidi tena yaliyojikita katika misingi ya kibinafsi. Mfano, ndoa ya CUF naCHADEMA inayopelekea NCCR mageuzi kuwa bendera fuata upepo imejengwakatika misingi ya kuvunja muungano, kwa makubaliano kuwa CUF kubaki na Zanzibar na CHADEMA kubaki na Tanganyika. CUF inataka inufaike namkakati dhalimu wa kunyonya rasilimali za wazanzibar yakiwemo mafuta bila kushurutishwa na sheria za muungano kwani wakiamini kubaki na muungano imara CUF na viongozi hao wachache katika chama hichowanakosa fursa za kupora rasilimali za wazanzibar.

IkubumbukweMuungano ndio unalinda mipaka na usalama wa raia katika kujiendelezana kujinufaisha bila ubaguzi wa kikundi cha watu wachache ambachokinaenda kinyume na utawala wa sheria.

Ikumbukwekuwa rasimu ya CUF walioipeleka kwa Mhe. Raisi mwaka 2011,mapendekezo yao ni tofauti na madai yao sasa ya serikali 3, hapa inatosha kutupa picha kuwa nia yao ni kuvunja muungano ili watuache katika mfarakano kama nchi nyingine zinazoteseka kwa sababu yawanasiasa uchwara.

Ifahamike ajenda ya CHADEMA ni kuvunja muungano ndio maana CHADEMA hawahangaiki kuimarisha chama Zanzibar, nia yao ni kubaki na Tanganyika ili waigawe Tanganyika katika vipande vipande kwa lugha ya majimbo iliadhima yao ya ukanda na ukabila itimie. Moja ya kanda yao ambayowametangaza katika kanda 8 walizo nazo ni Kilimanjaro, Tanga, Arushana Manyara. CHADEMA ina amini kanda hii inajitosheleza kwani ina bandari, mbuga za wanyama, madini, milima . Na hii imepelekea mbunge mmoja wapo wa CHADEMA kulazimika kusema kaskazini ni nchi huru huku mwenyekiti wao Mbowe akiendelea kudai mapato ya mlima Kilimanjaro yabaki Kilimanjaro.

Katikakipindi hiki ambacho wenzetu wamegomea bunge la katiba ambalo lipo kisheria na madai yao yakibadilika kila kunapokucha tena yakiwa na upotoshaji mkubwa kwa kufanya siasa chafu ili mradi watimize azma yakuisambaratisha Tanzania wakiwa makuwadi wazuri wa soko huria.Ukihoji leo sababu iliyowafanya watoke bungeni ni tofauti kabisa na sababu waliyoitoa siku wanatoka bungeni, eti msingi wao mkuu wao ni watetezi wa wananchi. Lakini tumesikia katika vyombo mbalimbali wananchi hao wakiwaasa na wakiwataka warejee bungeni ili kukamilisha kazi ya kisheria na tumaini la watanzania la kuwapatia katiba mpya. UKAWA hawa bila haya wamekataa. Swali? wanamtumikia nani. Mpaka sasa imepelekea wananchi hao wanaosema wanawawakilisha wameamua wenyewe kuja Dodoma kuendelea kusema kero zao na shida zao ili katiba hii iweze kutoa majawabu, mfano tumeshuhudia makundi ya wakulima, jukwaa la wahariri wa vyombo vya habari, wafugaji na makundi kadha wakadha yameendelea kutiririka Dodoma.
Hii ni picha tosha kuwa UKAWAhawawatumikii Watanzania na wameamua kuwahadaa Watanzania kwa mgongo wa kuwatetea huku ajenda yao ikiwa maslahi binafsi.

Nduguzangu Watanzania tunapowaunga mkono watu wanaoendelea kuligomea bunge la katiba wakati tunajua nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria, na wao ndio wamevunja sheria, tujue kabisa kuwa tunaenda kinyume na utawala bora, ambao umejengwa kwenye msingi wa sheria na demokrasia.Msingi wa demokrasia sio kususa baada ya kushindwa hoja, UKAWAhawataki hoja za wengine na wanalazimisha hoja zao pekee ndizozikubalike kinyume na msingi wa demokrasia. Na bila haya watu hao wasiojua demokrasia wameendelea kuwashawishi watanzania waingie barabarani huku wakijua kuwa Katiba haipatikani barabarani kama wanahoja kwanini wanaikimbia Dodoma? Mchakato huu ulianza kisheriana utahitimishwa kisheria, sio matamko ya makuwadi wa soko huria.

Miongonimwa madai yao matatu, (i) Rais avunje bunge (2) kinachojadiliwaDodoma sio rasimu ya warioba (3) Serikali tatu ndio maendeleo
Kwaujumla wake, UKAWA wanajua mamlaka ya Rais kwa mujibu wa sheria yamabadiliko ya katiba ya mwaka 2011, sura namba 83 imempa Rais mamlaka ya kuunda tume, kuchagua wajumbe 201, kutangaza na kuitisha bunge nakuzindua bunge la katiba, kupokea katiba inayopendekezwa na kuitangaza kwenye gazeti la serikali.,kwanini wanataka kumlazimishaRais kuvunja Sheria kwani hayo niliyoyataja ndio ambayo Rais anayo mamlaka ya kisheria kuyafanya katika mchakato huu wa Bunge la Katiba,na ndio maana hata wale wajumbe aliowateua ambao wamegomea Rais hajawatengua.,kinachojadiliwa bungeni ni Rasimu ya jaji warioba na kiko wazi, kwa sababu msingi mkuu wa majadiliano ni Rasimu inayotokana na tume tena kwa mujibu wa Sura namba 83 kifungu cha sheria namba 25/26 na kwa mujibu wa kanuni za bunge kifungu namba 33(8). Wanajua mamlaka ya bunge na waliohusika kutengeneza sheria hizi pamoja na kanuni waache kuwahadaa watanzania.

Jambola mwisho lenye kusikitisha zaidi ni kung'ang'ania Serikali tatu kana kwamba ndio kilio kikubwa cha watanzania, naomba niulize swali kati ya Muungano na migogoro ya ardhi ni jambo lipi limepoteza maishaya watanzania wengi na ambalo tunatakiwa kulifanyia kazi ili Watanzania wasiendelee kumwaga damu. Kati ya tatizo la ajira na muungano, kati ya afya na muungano, kati ya maji salama na safi na muungano, kati ya elimu bora na muungano, kati ya haki za binadamu na muungano eti watu hawa wanaojiita UKAWA kwao muhimu muungano kuliko chochote kile.
Watanzania naomba tupime kama ni kweli kuwa hawa ni watetezi wetu au ni makuwadiwa soko huria.


Kwaniaba ya watanzania wazalendo, napenda kuiomba serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuwatupia UKAWA jicho la pekee katika kuangalia na kufuatilia kwa ukaribu zaidi nyendo za UKAWA nahata kutuambia ni nani wako nyuma yao kiasi cha kuwa na kiburi cha kupindukia. Wito wa watanzania kwa vyombo vya ulinzi na usalama nikuwa amani, umoja na uhai wa nchi hii uko mikononi mwao, kwani nia yaUKAWA sio nzuri kwa mustakabali wa taifa hili na lazima wakumbuke USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA na pia MAJUTO NI MJUKUU NA HUJA BAADAE. UKAWA wanataka kutengeneza Misri, Afrika ya Kati, Libya, Syria,Sudani Kusini nyingine hapa Tanzania.


MunguIbariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika




PAUL MAKONDA
Katibu, idara ya Hamasa na chipukizi
Jumuiaya vijana chama cha mapinduzi (UVCCM)
 

Attachments

  • 0D6A4862.JPG
    600.4 KB · Views: 347
  • 0D6A4891.JPG
    503.2 KB · Views: 330
  • 0D6A4896.JPG
    611 KB · Views: 306
ukawa ni kikundi kinachoenda na upepo unakovuma, kesho kutwa wanakuja na lingine wanasahu ya nyuma
 
Kati ya mke wako na Muungano nani zaidi? Hoja zingine bwana! Kati ya baba yako na mkeo nani zaidi?
 
Huyu Makonda huwa simkubali sana, hasa alipoanza ule mtindo wake wa kukashifu wazee aliowakuta kwenye chama.

Wakati mwingine kuna watu waliopumbazwa ama kudumazwa kwa masilahi mpito ila uhalisia wao hufikia mahali ukajionesha kwa uwazi. Ulichoandika ndugu MSALANI hakina tofauti na kauli ya watu kama Nchemba anazozitoa kwa sasa mbali na kauli na matendo dhalili aliyowahi kutenda siku za nyuma.

MWENYEZI MUNGU AZIDI KUTULINDA KAMA WATANZANIA KWA UJUMLA WETU NA ATUJALIE FURSA YA KUMSHUKURU KWA KUTUMIA KARAMA NA VIPAWA VYETU KUSIMAMIA NA KUTENDA KWA MUJIBU WA HAKI NA MATAKWA YAKE.
 
Usiponde tena huu uzi safi sasa tunataka kuona nani ukawa nani ccm sio kelele zisizo na maendeleo............mfano unataka changia mada sema mimi ukawa :endelea............ Tena mimi ccm:endelea.........
Vijana tunahitaji maendeleo sio kelele duni hapa.........
Usiseme vibaya chama chako kipende banaaa....
 
we KONDA, sasa si muendelee kujadi na kupitisha hiyo katiba yenu unawataka UKAWA wa nini? AU mnajua ni maji marefu?
 
Yaani mchakachue maoni yetu mtake tukae kimya!!!!!!! patachimbika anzisha maandamano, tunasubiri tamko la viongozi wetu hatuwezi kutoa maoni yetu mkayachakachua eti tusiongee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Peoplesssssssssssssssssszzzzzzzzzziiiiiiiiiiiiiiiii SHITIIIIIIIIII
 
Bora angekuwa mtu mwingine,lakini makonda!huyo kichwani hazimo.na mwakani atakimbia nchi.
 
ccm wote wapumbavu sana. Majitu majinga majinga tu, hayana hoja zaidi ya makelele na mauaji halafu yatusumbue hapa. Mwisho wa ccm umefika.
 
Makonda mchumia tumbo, si muda mrefu utasutwa na maneno yenu. Sikilizeni sauti za wananchi. Kama mnajadili oja toeni tamko lingine kuhusu tume ya Warioba na kauli za maaskofu pia na taasisi nyingine za kiraia. Sauti za kulalamikia mnachokifanya ni nyingi hata ndani ya ccm tatizo lenu hamna uchungu na wananchi wa nchi hii hasa watanganyka. Nchi hii ni yetu sote hakuna anayetumika hapa bali nyinyi mnaogopa kivuli chenu kwa kuona kuwa mabadiliko ya katiba yanaweza kuing'oa ccm madarakani. Mkumbuke kuwa hata ndani ya ilani yenu hamkuwa na mpango wa katiba mpya.

Mngekuwa smart enough mngemwondoa JK madarakani kwa kushindwa kuilinda katiba ya muungano alipoona inavunjwa na Wazanzibar kwa mabadiliko ya katiba yao ya 2010. Kumbuka jinsi Nyerere alivyo fanya kwa Jumbe mwaka 1984, Ulikuwa mdogo soma historia. Baada ya mabadiliko ya 2010 hakuna tena muungano mmebaki kuabudu sanamu. Rasimu ya katiba mpya kwa pendekezo la serikali 3 inajaribu kuurudisha muungano kwani hakuna muungano wa nchi 2 na bado zikabaki kuwa nchi ni lazima iwe nchi moja na serikali 1 au 3 na kuendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…