UVCCM: Wafuasi, wasaliti au wasanii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM: Wafuasi, wasaliti au wasanii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfu Lela Ulela, Apr 4, 2011.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa siku za karibuni Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM), umekuwa ukitoa kauli zenye utata kati ya viongozi wake. Baada ya kikao cha Bagamoyo, wakaibuka wengine Tabora na kauli tofauti. Mara akaibuka Beno Malisa na kauli zake tata. muda si muda wakaibuka UVCCM Kilimanjaro na kauli zilizozidi kuwachanganya wanachama wake na kuonekana kweli zinakigawa chama.

  Lakini zipo tetesi kuwa kinachoendeleas UVCCM SI UHALISIA bali vijana wanafanya MAZINGAOMBWE. Kwa maana kuwa ni mkakati maalumu wa kuwachanganya wananchi ili waache kucocentrate kwenye mambo ya msingi na kubaki kushabikia ugomvi "wa kupikwa" ndani ya UVCCM.

  Je, ni kweli UVCCM wanatumiwa, je ni wasaliti wa chama chao, au ni wasanii tu? wanaJF mnasemaje?
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kutokuwepo kwa JKT kutaathiri utendaji makini wa taasisi nyingi za umma na jamii. UVCCM sasa hivi inaongozwa na vijana wa kuokota mitaani tu.
   
 3. n

  ndutu Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Brother JKT pekee haisaidii na wala maadili hayakuwa yanajengwa JKT. Kule tulifundishwa ukakamavu na uwezo wa kupambana na mazingira lakini somo la uzalendo lingekuwepo hawa mafisadi wa leo wasingekuwepo maana nao walipita huko huko.

  Suala lililo wazi hapa ni kwamba uzalendo unakosekana na sasa ni wakati wa kukuna kichwa nini kifanyike kurejesha uzalendo na woga kwa mali za umma. Linalonijia akilini kwa haraka haraka ni kuhakikisha kwamba wale waliohusika na wanajulikana wawe mfano kwa wengine wa namna sheria inavyoweza kumbabua mtu. Kwa kufanya hivyo hata hawa mafisadi chipukizi watajiuliza mara mbili mbili kama waendelee kurithi hiyo mikoba au la. Kwa hakika UVCCM wamechanganyikiwa na kilicho bayana ni kutumiwa kwao, tena na watu wawili watatu ambao ni sumu kwa taifa hili.
   
Loading...