UVCCM ni wazalendo au wahalifu wa Taifa hili?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,273
Unaweza kuwa mzalendo kwa taifa lako kupitia vyama vya siasa?
Huu ndio mjadala unaoumiza vichwa jamii nyingi hasa za kiafrika katika ulimwengu wa leo.

Ukiwaangalia makada wa chama tawala wanajiona wao ni wazalendo wa taifa hili kuliko mtu yeyote yule na wamejipa hakimiliki ya taifa kwa kila kitu, ikitokea uwe upande wa upinzani unaonekana wewe sio mtanzania na ni mhalifu kabisa....

Pia kwenye vyama vya upinzani kumejengwa mtazamo huo kuwa wao ni bora zaidi mbele yauso wa Taifa, na kwamba wale wa Chama tawala ni wahalifu na wasaliti kwa taifa hili (huo ni kweli).

Hii ndio mitazamo ya watu wote katika siasa, na kwa bahati mbaya kila kitu nchini kinaendeshwa kisiasa na rais wa nchi ndiye kiongozi wa mitazamo hii kuwaona wasio wanaccm kama wahalifu na sio wazalendo kwa Taifa letu.

Hebu fuatana nami tujifunze mambo machache juu ya haya...

Kwanza tujiulize, Siasa ni nini?

Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni njia azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani.

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa yake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa. Mpaka hapo tumeshafahamu mwanasiasa ni mtu wa aina gani katika taifa,

Je Itikadi ni nini?

Itikadi ni mkusanyiko wa imani unaoshirikiwa na kikundi cha watu fulani. Kuna aina kuu mbili za itikadi: Itikadi za kisiasa, na itikadi za kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo). Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa. Itikadi za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi. Kwakuwa dhamira yetu ipo kwenye mkondo wa siasa, hivyo tujikite kuangazia itikadi ya kisiasa zaidi katika mukthada huu.

Ulishawahi kujiuliza kwanini vyama vya siasa Marekani, Israel, Italia, Urusi nk, havitumii bendera wala nembo zao ktk mikutano ya hadhara?

Na sio kwamba havina nembo na bendera, bali havizitumii kama ilivyo kwa siasa za Afrika.

Kwa taarifa yako wenzetu ili kulinda uzalendo wa watu kwa taifa lao, huendesha siasa kwakuzingatia viashiria vya ukuu wa uzalendo na utaifa.......Hili kwa Tanzania Mwalimu Nyerere alikosea sana pale alipotilia mkazo kujenga kunguvu ya chama badala ya kujenga nguvu ya misingi ya utaifa wetu, badala ya kujenga nidhamu ya taifa, yeye akajenga nidhamu ya chama kilichoshika hatamu, Yaani chama kilikuwa na nguvu kuliko serikali na taifa... Hali inayopelekea kuwa chama kikianguka na taifa linaanguka.

Mwanafalsafa Plato anasema, "Serikali ya kidemokrasia ya watu wapumbavu ni hatari zaidi kuliko serikali ya kidikteta ya watu wapumbavu"...

Tafsiri sahihi ya uzalendo ni kuilinda nchi yako dhidi ya maadui wa ndani ambao kwa namna moja kuu ni serikali, na maadui wa nje. That's obvious.

Nawaomba someni vitabu na nyaraka hizi hapa chini kwa faida yenu marafiki zangu...

National identity
National identity - Wikipedia

Do we need nationalism today? Why?
http://postnito.cz/do-we-need-nationalism-today-why/#What_is_nationalism_and_why_is_it_important

What Is The Meaning And Importance Of Nationalism Politics Essay

Nationalism in the 21st Century
Nationalism in the 21st Century

The New Age of Nationalism
The New Age of Nationalism

Na Yericko Nyerere
 
heading na uliyoandika ndani hayaendani mkuu.
nilitegemea chadema kuonyesha uzalendo unaouhubiri, wangeacha kutumia Bendera za chama.
au lingekuwa pendekezo katika hitimisho lako
Tatizo umakini umeupeleka CCM ukasahau matiki ya unachoandika
 
29418379e7036c196b4ee162fcc4dddb.jpg

Ngoja nimalize mazoezi ntarudi
 
Yuvisisimizi walikuwa na akili timamu enzi zile wanamiliki bendi ya Air Pambamoto, angalau walikuwa wanatoa ajira na burudani. Hivi sasa kazi yao ni matusi na ukuwadi wa wagombea urais.
 
Unaweza kuwa mzalendo kwa taifa lako kupitia vyama vya siasa?
Huu ndio mjadala unaoumiza vichwa jamii nyingi hasa za kiafrika katika ulimwengu wa leo.

Ukiwaangalia makada wa chama tawala wanajiona wao ni wazalendo wa taifa hili kuliko mtu yeyote yule na wamejipa hakimiliki ya taifa kwa kila kitu, ikitokea uwe upande wa upinzani unaonekana wewe sio mtanzania na ni mhalifu kabisa....

Pia kwenye vyama vya upinzani kumejengwa mtazamo huo kuwa wao ni bora zaidi mbele yauso wa Taifa, na kwamba wale wa Chama tawala ni wahalifu na wasaliti kwa taifa hili (huo ni kweli).

Hii ndio mitazamo ya watu wote katika siasa, na kwa bahati mbaya kila kitu nchini kinaendeshwa kisiasa na rais wa nchi ndiye kiongozi wa mitazamo hii kuwaona wasio wanaccm kama wahalifu na sio wazalendo kwa Taifa letu.

Hebu fuatana nami tujifunze mambo machache juu ya haya...

Kwanza tujiulize, Siasa ni nini?

Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni njia azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani.

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa yake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa. Mpaka hapo tumeshafahamu mwanasiasa ni mtu wa aina gani katika taifa,

Je Itikadi ni nini?

Itikadi ni mkusanyiko wa imani unaoshirikiwa na kikundi cha watu fulani. Kuna aina kuu mbili za itikadi: Itikadi za kisiasa, na itikadi za kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo). Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa. Itikadi za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi. Kwakuwa dhamira yetu ipo kwenye mkondo wa siasa, hivyo tujikite kuangazia itikadi ya kisiasa zaidi katika mukthada huu.

Ulishawahi kujiuliza kwanini vyama vya siasa Marekani, Israel, Italia, Urusi nk, havitumii bendera wala nembo zao ktk mikutano ya hadhara?

Na sio kwamba havina nembo na bendera, bali havizitumii kama ilivyo kwa siasa za Afrika.

Kwa taarifa yako wenzetu ili kulinda uzalendo wa watu kwa taifa lao, huendesha siasa kwakuzingatia viashiria vya ukuu wa uzalendo na utaifa.......Hili kwa Tanzania Mwalimu Nyerere alikosea sana pale alipotilia mkazo kujenga kunguvu ya chama badala ya kujenga nguvu ya misingi ya utaifa wetu, badala ya kujenga nidhamu ya taifa, yeye akajenga nidhamu ya chama kilichoshika hatamu, Yaani chama kilikuwa na nguvu kuliko serikali na taifa... Hali inayopelekea kuwa chama kikianguka na taifa linaanguka.

Mwanafalsafa Plato anasema, "Serikali ya kidemokrasia ya watu wapumbavu ni hatari zaidi kuliko serikali ya kidikteta ya watu wapumbavu"...

Tafsiri sahihi ya uzalendo ni kuilinda nchi yako dhidi ya maadui wa ndani ambao kwa namna moja kuu ni serikali, na maadui wa nje. That's obvious.

Nawaomba someni vitabu na nyaraka hizi hapa chini kwa faida yenu marafiki zangu...

National identity
National identity - Wikipedia

Do we need nationalism today? Why?
Do we need nationalism today? Why? | POST

What Is The Meaning And Importance Of Nationalism Politics Essay
What Is The Meaning And Importance Of Nationalism Politics Essay

Nationalism in the 21st Century
Nationalism in the 21st Century

The New Age of Nationalism
The New Age of Nationalism

Na Yericko Nyerere
Nina Imani majibu ya Ndug Shaka wa UVCCM kwenye Magazeti ya leo yamekutoa pangoni
Hivi BAVICHA wapo wapi?
IMG-20170515-WA0004.jpg
 
Yuvisisimizi walikuwa na akili timamu enzi zile wanamiliki bendi ya Air Pambamoto, angalau walikuwa wanatoa ajira na burudani. Hivi sasa kazi yao ni matusi na ukuwadi wa wagombea urais.
BAVICHA wamepotelea wapi???mbona sijawasikia hata kidogo au Chama chao kimekosa miundombinu kwa vijana?
Chadema wamefail kweli maana wao ndio walitakiwa kuwa washindani wa UVCCM katika kutengeneza Vijana wazalendo, sasa kazi ya kutengeneza Vijana wazalendo imekuwa ya UVCCM pakee.
 
Ogopa sana kusanyiko la watu wengi na mbaya zaidi kusanyiko hilo likawa na WAJINGA wengi..

Ndio ivyo ilivyo CCM.

Nani atabisha hapa kwamba CCM wengi sio wajinga??
Mojawapo ni hili hapa chini.
Kusanyiko CHAFU kuwahi kutokea ulimwenguni
Wazalendo

Kimsingi Mabandiko/thread zako Kijana huwa zina Hoja Za Kitoto sana bora wale wadaku akina Malisa G na Mange Kimambi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom