UVCCM Jitokezeni kumjibu Zitto

UVCCM Jitokezeni kumjibu Zitto

Tulime

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
248
Reaction score
104
"UVCCM MMEFITINISHWA NA SERIKALI YENU!"


Zitto Zuberi Kabwe, kiongozi mkuu katika chama chake cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini ameifitinisha UVCCM na Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi-CCM.

Mh. Zitto ameandika taarifa yake juu ya mzozo wake na Waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga. Amesema kuwa katika kile kinachoitwa hujuma dhidi ya Rais Magufuli,Jumuiya ya Vijana wa CCM imenunuliwa na Waziri Kitwanga kukinga na kutetea uhalifu.
Katika taarifa yake ndefu Zitto amesema kuwa Waziri Kitwanga ni mkosefu,yako madhambi anafanya katika Serikali na hivyo hayo ndio yatakayomuondoa madarakani na sio yeye kwa kuwa sio size yake.

Kwa muktadha huo,kwa mujibu wa maneno ya Zitto inawezekana kabisa kufikirika kuwa vijana wa UVCCM wamenunuliwa na Waziri Kitwanga kuficha madhambi ambayo ni makosa ama uhalifu dhidi ya Serikali ambayo inaongozwa na CCM. Niliwahi kusema mahala kuwa "Vijana wa nchi hii tunao wajibu mkubwa kabisa kumsaidia Rais kutafsiri mambo haya sawasawa ikiwa tunataka nchi yetu isonge mbele"

Leo natumia kalam hii kusema kuwa UVCCM chukueni tahadhari mapema, mmefitinishwa na Serikali yenu tayari. Jitokezeni hadharani Viongozi mseme kama mlituma vijana kuwasemea Infosy mbele ya waandishi wa habari. Kama hakuna mnachojua juu ya hilo kwa sababu yoyote ile, semeni kuwa hatujui lolote ila tunashangaa UVCCM kuingizwa katika mzozo usioihusu jumuiya yetu. Kwisha kusema hivyo endeleeni na shughuli zenu,hiyo itakuwa ni kinga tosha kwa jumuiya na chama chenu.

Kimya ni jibu.
Mtapokaa kimya,kisha ikafahamika kuwa uko uhusiano mkubwa kati ya Waziri Kitwanga(Infosy) na mkataba tata wa Lugumi mtakuwa mmejitukanisha wenyewe kwa Rais wenu. Madhara ya kuendelea kukaa kimya wakati mmekwisha ingizwa tayari katika mzozo ni makubwa mno maana tuko tutakaodhani kuwa ni kweli mmenunuliwa kutetea uhalifu kama asemavyo Kabwe. Mkikanusha taarifa hii kwa sehem yanu haina madhara hata ikithibitika kuwa Waziri anaonewa!
Uungwana ni vitendo, jitokezeni sasa!

Rais anapigana vita vikubwa!
Hakuna kipindi kingine zaidi muhimu ambacho Rais Magufuli anahitaji msaada mkubwa kutoka katika chama chake kama kipindi hiki. Ni kipindi hiki ambapo chama kikiteleza na kujitenga Rais atapata dhiki kubwa katika kushinda vita hii ambayo sio lelemama.

Rais ameambiwa kuwa UVCCM mnatumika kulinda na kutetea hujuma,nyie mnakaa kimya mnataka Rais ajue nini? Mnataka aamini anachoambiwa? Baada ya kuamini kisha iweje? Kwani hamjui kuwa huyu ndie Mwenyekiti wa chama hapo baadae? (Bahati haimfanyi mpumbavu kuwa na busara)

Zitto Zuberi Kabwe amesema Viongozi huwa wana mawasiliano yao ambayo amekua akiwasiliana na mkuu wa nchi kushaulina juu ya mambo ya nchi. Yamkini atakau kamwambia mengi kuhusu uhusika wenu katika hili. Kasema ana ushahidi usio na mashaka,isiwatishe!
Huyu ni mwanasiasa,anajibiwa kisiasa,semeni HATUJUI,HATUHUSIKI NA HATUTAHUSIKA hivyo TUSIHUSISHWE kwa namna yoyote, kisha mnamalizia kuwa ushahidi alionao Kabwe ni wa uongo,ametengeneza kwani technology imekua sana.
Si basi? Hapo si itawaondoa katika hisia kuwa mmenunuliwa?
UVCCM amkeni,nyinyi ndio walinzi wa chama,chama kimeanza kumeguka!

Ikumbukwe kuwa yote haya yanayoendelea yametokana na uwepo wa kashfa ya mkataba tata wa Lugumi. Tunasikia yote haya katika jitihada za watu kujinasua na utata huu wa mkataba. Mzozo huu umekuja baada ya kubainika dosari katika mkataba huo ambao tayari umeundiwa kamati maalum ya Bunge kuchunguza usafi na udharimu wake.
Ni wazi kuwa tayari UVCCM mmehusishwa katika kashfa ambayo ikithibitika itakuwa ya kifisadi. Baada ya kuthibitika tafsiri ya moja kwa moja itakuwa kwamba mlitumika kuzuia mbio za Rais katika kupinga ufisadi ndani ya Taasisi za Serikali. Aibu kubwa ilioje!
UVCCM zinduka.

Mh. Zitto Zuberi Kabwe"kumradhi sana"
Iondoe UVCCM katika mikakati yako ya kifedhuri,unakumbukwa kwa kuiangusha serikali ya awamu ya nne mara kadhaa.
STOP!
Inatosha..
 
Back
Top Bottom