UVCCM Dodoma wazindua mbio maalum za pikipiki zenye lengo la kuhamasisha uzalendo!

Paul Makonda

Member
Jul 8, 2011
97
186
DSC01160.JPG DSC01166.JPG IMG_8342.JPG IMG_8350.JPG IMG_8360.JPG DSC01163.JPG IMG_8360.JPG IMG_8369.JPG
Leo Tarehe 22/03/2014 katika Manispaa ya Dodoma, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), tumezindua mbio maalum za pikipiki zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa vijana na kuibua fursa zinazopatikana maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Mbio hizi maalum zimezinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, katika hafla fupi ya kufana iliyofanyika katika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Dodoma.

Mbio maalum za pikipiki zitazunguka nchi nzima na zitahitimishwa rasmi kwa matembezi ya miguu kuanzia Kibaha Mkoani Pwani hadi Dar es Salaam tarehe 25/04/2014 yatakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Mrisho kikwete katika ukumbi wa Nyerere Convention.

Kauli Mbiu Yetu
"MIAKA 50 YA MUUNGANO; VIJANA TUDUMISHE MUUNGANO WETU NA TUTUMIE FURSA ZILIZOPO KULETA MAENDELEO YETU"
TANZANIA KWANZA, MENGINE BAADAYE

Imetolewa na;
Paul C. Makonda
Katibu wa Hamasa uhamasishaji UVCCM
 
safi sana ikiwezekana tengenezeni cd za kutosha za hutuba ya karne ya mheshimiwa rais ya kuzindua bunge maalamu la katiba ambazo zitasambazwa maeneo yote mtakayopita hili wananchi waweze kusikiliza busara za hali ya juu za mpendwa rais wetu
 
Hivi nitakuwa mzalendo kweli, wakati wachache wanafaidi keki ya taifa???
 
Huu utumbo nao ni wa kupost humu?si kila kitu nikupost JF,mbona hutuletei wazee wa madawa ya kulevya na meno ya tembo namna mnavyowakamata na kuwafunga vifungo vya maisha?kwa yanayoendelea tanzania bado kuna uzalendo kweli?Ninachofahamu uzalendo kwa nchi hii ulisha tangu Nyerere atoke madarakani,mengine yote yanayoendelea ni usanii mtupu.
 
wamekosa kazi si wakalime zabibu au msimu umepita!
 
Kila mwenye akili atajiuliza atajiuliza bunge la katiba linaendelea kufanya nini Dodoma ikiwa hata wajumbe wa bunge hilo wanatoka nje ya ukumbi kuandaa maandamano ya kuunga mkono serikali mbili.

Bunge lisitishwe wajumbe waache kukaa kula hela za uma wakati wanafanya mtihani wakiwa wameshapewa majibu tayari. Au hoja ya muundo wa muungano itolewe kwenye rasimu zibakizwe hoja zisizo na shinikizo la ccm.
 
View attachment 146448View attachment 146449View attachment 146450View attachment 146451View attachment 146453View attachment 146454View attachment 146453View attachment 146455
Leo Tarehe 22/03/2014 katika Manispaa ya Dodoma, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), tumezindua mbio maalum za pikipiki zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa vijana na kuibua fursa zinazopatikana maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Mbio hizi maalum zimezinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, katika hafla fupi ya kufana iliyofanyika katika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Dodoma.

Mbio maalum za pikipiki zitazunguka nchi nzima na zitahitimishwa rasmi kwa matembezi ya miguu kuanzia Kibaha Mkoani Pwani hadi Dar es Salaam tarehe 25/04/2014 yatakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Mrisho kikwete katika ukumbi wa Nyerere Convention.

Kauli Mbiu Yetu
"MIAKA 50 YA MUUNGANO; VIJANA TUDUMISHE MUUNGANO WETU NA TUTUMIE FURSA ZILIZOPO KULETA MAENDELEO YETU"
TANZANIA KWANZA, MENGINE BAADAYE

Imetolewa na;
Paul C. Makonda
Katibu wa Hamasa uhamasishaji UVCCM

Ni ujinga na kutokufikiri vyema kama mtu mwenye akili timamu ataamini kwamba uzarendo unapatkana kwa kuhamasishwa kama mnavyowaaminisha watz,uzarendo unapatkana kwenye mioyo ya watu na sio kutembea kwa mapik pik.
 
View attachment 146448View attachment 146449View attachment 146450View attachment 146451View attachment 146453View attachment 146454View attachment 146453View attachment 146455
Leo Tarehe 22/03/2014 katika Manispaa ya Dodoma, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), tumezindua mbio maalum za pikipiki zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa vijana na kuibua fursa zinazopatikana maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Mbio hizi maalum zimezinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, katika hafla fupi ya kufana iliyofanyika katika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Dodoma.

Mbio maalum za pikipiki zitazunguka nchi nzima na zitahitimishwa rasmi kwa matembezi ya miguu kuanzia Kibaha Mkoani Pwani hadi Dar es Salaam tarehe 25/04/2014 yatakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Mrisho kikwete katika ukumbi wa Nyerere Convention.

Kauli Mbiu Yetu
"MIAKA 50 YA MUUNGANO; VIJANA TUDUMISHE MUUNGANO WETU NA TUTUMIE FURSA ZILIZOPO KULETA MAENDELEO YETU"
TANZANIA KWANZA, MENGINE BAADAYE

Imetolewa na;
Paul C. Makonda
Katibu wa Hamasa uhamasishaji UVCCM
Mafisadi nyie nendeni pemba
 
Mkuu, swali kubwa watu wanalojiuliza, ilikuwaje CCM wakaunda tume iliyotumia gharama kubwa,ili kukusanya maoni ya wananchi, wakati wao CCM wanataka mambo yao yote wanayopenda yapite kwa lazima!?, kwa nini wasingeitisha kamati kuu ya CCM wakakaa na kutunga katiba wanayotaka kuliko kutupotezea muda na fedha wakati wao tayari wana katiba yao?

CCM ni watu wa ajabu sana.
 
Kikwete kashindwa kujua maana ya simple majority anadai kama wanaotaka Tanganyika ni wengi basi tume ilitakiwa kuhoji watanzania milioni 20! Hii ni hajabu ya yeye kuwa rais wa watanzania milioni 45 wakati alichaguliwa na asilimia ndogo ya watanzania hawa!
 
Back
Top Bottom