Uvaaji wa magauni mafupi, vimini, kikaptula

Bitoz

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
30,823
Reaction score
126,642
Mko poa walimbwende,

Ngoja niwape darasa kidogo, kimsingi uvaaji wa nguo fupi kwa wanawake pia ni fasheni ya mjini nazungumzia gauni fupi,kimini au kikaptula(kichupi) ila nazungumzia zaidi vimini na magauni mafupi.

1/Mazingira yanaruhusu?
Kabla hujavaa kimini au gauni fupi jiulize kwanza unaenda ofisini,sehemu ya ibada,starehe au kitaani tu au utapanda daladala? Ukijiridhisha wewe jipigie tu kimini chako.

2/Una miguu?
Kuvaa tu kinguo kifupi wakati una miguu mibaya ni sawa na kujidhalilisha tu kama unajijua unatembelea mikono usivae vazi hili.

3/Kiatu kirefu ndio mwake
Ili utoke bomba na gauni fupi au kimini hakikisha unavaa kiatu kirefu, lakini kimini pia kinaweza kuvaliwa na flat shoes kikaeleweka utaonekana wa kijanja.

4/Epuka kuinamainama
Ukivaa vazi fupi kamwe usitake kuinama unaweza kujikuta mali zako zinabaki nje.Njia bora wakati unaokota/kuchukua kitu ni kuchuchumaa tu.

5/Kaa kwa staha
Wakati wa kukaa hakikisha unapishanisha miguu badala ya kuachanisha au kuitanua, utakaa uchi !!!!!

6/Uvaaji wa kaptula fupi/kichupi
* Huvaliwa chumbani au sehemu ya starehe
* Inapendeza ukivalia top au blauzi
* Hakikisha miguu yako ipo soft


The Bitoz
 
Yaani hapo jamaa amegusa penyewe,unakuta mwanamke miguu myembamba kama antenna halafu anavaa kasketi kafupi na anaringa yaani hadi kinyaa kumtazama,si bora ajivarie tu nguo ndefu kwa heshima.
Sio kosa lake....hajui atoke vipi
 
Kwanini uvae nguo fupi unamuonyesha nani?nguo fupi ni kujidhalilisha tu kwa watu wanaojiheshimu.mimi ninapomuona mwanamke kavaa skirt fupi nahisi ni biashara tu maana hakuna mantiki yoyote.
 
Kwanini uvae nguo fupi unamuonyesha nani?nguo fupi ni kujidhalilisha tu kwa watu wanaojiheshimu.mimi ninapomuona mwanamke kavaa skirt fupi nahisi ni biashara tu maana hakuna mantiki yoyote.

Ni fasheni ya mjini....sharti ivaliwe sehemu za starehe
Huwezi kuvaa hijab disco !!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…