Jumuiya hii inahitaji kumulikwa upya. Kauli zao zimekuwa zikiibuwa mashaka kwa mustawa wa nchi nzima. Hazijaanza leo wala jana.
jumuiya hii imepewa viongozi wasiojuwa wajibu wao kwa nchi. Hawajuwi maslahi ya nchi wao wanajuwa maslahi ya chama hata ikibidi kwa kuvunja katiba na sheria za nchi.
Jumuiya hii imethubutu kusema Viongozi wanaotokana na vizazi vya kisultani hawatatawala nchi, labda watawale mikarafuu na minazi. Dola iko kimya hivi watu hawa wako juu ya Katiba na sheria.
Wanaapishana kulinda mapinduzi kwa njia yoyote ile hadi tone la mwisho la DAMU mbele ya viongozi wao wa kitaifa.
wanapinga mabadiliko kwa kisingizio cha kulinda mapinduzi. Wanasema na wanatenda hakuna wa kuwauliza. Wana makamanda wao, wanatoa amri na kutekelezwa.
Napata wasiwasi wanamtandao hadi katika vikosi vya ulinzi ambapo hutumika kwa maslahi yao. Wana uthubutu wa kutoa maagizo na kutekelezwa na yasipotekelezwa kunaandaliwa fitina ili malengo yao yatimie.
Jumuiya hii imetumika kuvunja maridhiano ya Zanzibar yalitengenezwa na Amani Karume. Wameiyumbisha GNU na Zanzibar. Wanapigwa mbeleko na baadhi ya viongozi wakubwa kwa maslahi yao sio ya CCM nzima na nchi.
Ziko habari mtandao umeanzia kwenye jumuiya yenyewe, vikosi vya SMZ hasa KVZ, Baadhi ya vyombo vya dola vya Jamuhuri, Mahkama, na taasisi nyengine za SMZ. Wanajiamini wanachokisema wakiaminbi vyombo vyote viko mikononi mwao. wamejengeka kiburi .
Sasa hivi nchi iko katika mkwamo hawaisaidii wanaizamisha wenyewe wanaona wanakisaidia chama, wakubwa wamepiga kimya.Wameleta fitina kwa wanachama wenye mtazamo chanya juu ya mshikamano wa wananchi na maendeleo ya wote.
Walifanya fitina katika uchaguzi wa viongozi ngazi za mikoa na wilaya wakawekwa makanjanja ambao hawakisaidii chama hasa Zanzibar. Wamepelekea chama kukimbiwa na vijana wengi, wameendeleleza visasi kwa wenye mtazamo tofauti na wao. Hawana maono. Wanafanya siasa chafu.
Wanafanya siasa na chafu za kiharakati za ukombozi sasa wanafikiri wanapata sifa kumbe wanaipoteza taswira ya nchi iliyojengwa kwa nidhamu. Katika hili CCM taifa wana la kujibu. Wamewaacha vijana wao wafanye watakavyo, Hili linaloendelea Zanzibar halistahamiliki.
Muulize kiongozi yoyote wa CCM Zanzibar uone anavyowaogopa Uv- CCM Zanzibar. Wamekuwa malaika wa kutoa masindikizo hata ya kuhatarisha amani na umoja wa wananchi. Hawawezi kuonywa. Wamelelewa hivyo wamekuwa na sasa wamekuwa wakubwa.
Hawajuwi zaidi ya kujtekelezewa masindikizo yao kinyume na hivyo unafanyiwa fitina ndani ya chama na seriukali na mwishowe unalala mchangani. Katika hali kama hio unalazimika ufuate matakwa yao ili uwepo katika nafasi yako iwe serikalini, mahakama au bungeni,
Jumuiya hii inaiyumbisha Zanzibar na Tanzania, IMULIKWE kwa mustakbali wa nchi.
Mungu ibariki Tanzania.