Utumwa makampuni ya madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumwa makampuni ya madini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by masomo, Oct 28, 2012.

 1. m

  masomo JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania bado wapo watu wanaotumikishwa kama watumwa chini ya ukandamizaji wa watanzania na siyo wawekezaji hasa kwenye sekta ya madini.Kwenye makampuni ya drilling/uchorangaji kwa asilimia kubwa ni sehemu ambayo wafanyakazi wake hufanya kazi ngumu na za hatari sana na ni moja ya maeneo ya kinyonyaji ambapo utakuta makampuni haya hayawafanyishi kazi kwa taratibu na sheria za kazi.eneo hili limekuwa halina mtetezi kwa muda mrefu sasa kutokana pia na waajiriwa wengi maeneo haya ni vijana ambao wengi hawana elimu kubwa.

  Katika kutembea maeneo mbali mbali ya uwekezaji katika sekta ya madini sikuwahi kuona kiongozi wa serikali akitetea maslahi ya watanzania ingawa wawekezaji wengi wamekuwa wakipitia kwa viongozi wa serikali na kuwaomba ushauri juu ya maslahi ya watakao waajiri,kwa mfano wakuu wa wilaya,wengi wamekuwa wakishauri viwango vidogo vya mishahara kiasi cha baadhi ya wawekezaji kuwashangaa na hata wengine kusema hawaitetei serikali yao kwani kwa kushauri viwango vidogo kiasi hicho wanainyima serikali yao mapato ya kodi.Hali hii kwa mtizamo pia inasababishwa na ubinafsi,mbunge,mkuu wa wilaya au afisa fulani asingependa kusikia malipo yanayomzidi kwani yupo mkuu wa wilaya fulani alidiriki kusema mishahara ya magiologisti ni mikubwa kuliko mkuu wa wilaya kwa maana ya kutaka ipunguzwe.

  Nawaomba mjirekebishe wenye hizi tabia na tuwatetee watanzania bila ubinafsi na wanaohusika chukueni hatua.
   
 2. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Kwa taarifa yako viongozi hao ndio ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwatetea hao wanaoitwa wawekezaji badala ya kuwatetea wakesha hoi. Nakumbuka wakati migodi ya Geita inaanza mkuu wa wilaya wa wakati ule ndiye alikuwa wa kwanza kushauri kuwa wafanyakazi wa wasilipwe mishahara mikubwa kwa madai kuwa watakuwa hawaendi kazini mwisho wa mwezi.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Na ili suala huwa nashikwaga na butwaa mwekezaji anakuja na scale yake ya mishahara alafu anatokea mpuuzi fulani anaslash!
  alafu anaomba cha juu kwa kuslash,ivi apounakuwa na akili timamu kweli si unajishushia laana wewe na ukoo wako
  kinachotokea sasa mwekezaji ana adopt ushauri wa uyu kenge as a result kazi zinakuwa full wizi mtu anahandle vitu vya mpaka 300mil kwa mwezi unaishia kumpa mshahara wa laki 8
  Nina ushahidi wa makampuni kama mawili ivi moja la ujenzi na lingine lahusika na na mikopo
  tuache ubinafsi tuwe wazalendo
   
 4. w

  wikolo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wanakwambia wewe mtanzania ukilipwa mshahara mkubwa eti utasababisha 'inflation'!! Kazi kweli kweli nchi hii.
   
 5. SHOSHOLOZA

  SHOSHOLOZA Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hapo ndipo umetugusa sisi wafanyakazi wa migodini. Kwa mfano mimi kwa kazi yangu natakiwa kufanya kazi na watu wawili. Nafanya kazi na wacanada wawili mmoja ambaye ni kiongozi analipwa dola 18,500 kama milion 29, usafiri wa bure hadi kwake wakati wa mapumuziko, anaishi amp bureee. Wapili naye analipwa dola 14,000 zaidi ya milioni 20 na vitu vyote kama kiongozi. Mimi mubongo nalipwa tshs. 842,500. Hiyo ndiyo nile na familia na nauli pia wakati wa mapumziko. Hapo tunafanya kazi ileile hadi mwisho kila siku, tofauti tu ni kuwa wao ni ma expart. Jamani hali siyo nzuri. Ukilalamika viongozi wakibongo wanakwambia acha kazi.

  Sijuwi inji hii inatupeleka wapi. Tuna waghana hapa wao wanalipwa milioni 15, na hela ya kujikimu kila wiki laki 8 ya maji na sigara. Shiiiida
   
 6. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  na hela ya mafao inayokatwa kila mwezi nayo SSRA wanaitaka eti mpaka ufikishe miaka 55 hapo ndipo natamani kujilipua kama gaidi
   
 7. m

  masomo JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Shida kubwa ni ubinafsi kwa viongozi wivu wa viongozi wengi kufikiri hakuna anayestahili kulipwa zaidi yao ni hilo tu.wazungu wawekezaji wengi wamekuwa wakiwashangaa sana hawa viongozi.wawekezaji waliona basi ni afadhali walipe kwa dola angalau mtanzania apate angalau kidogo, wakaamua kuondoa na kudai kulipwa kwa dola kunaleta mfumuko wa bei.
  Jamani,hawa watanzania wenzetu wakilipwa vizuri si ndiyo mwanzo na wafanyakazi wa serikalini kulipwa vizuri kwa ongezeko la kodi hii ya wafanyakazi wa migodini.
  Ukweli ni kwamba tanzania ni nchi ambayo ingeweza katika kampuni nyingi watu kulipwa si chini ya kima cha chini cha milioni mbili kwa mwezi,tatizo ni uchoyo,wivu na ubinafsi,madhalani makampuni ya simu ambayo yanaingiza faida ya mabilioni ya pesa,makampuni ya pombe,makampuni ya sigara,makampuni ya madini na uchorongaji/drilling companies,bima ,makampuni ya ujenzi wa barabara,mabenki nk.shida nyingine ni kujipendekeza viongozi wetu kwa wawekezaji pamoja na ufisadi ambapo kuna makampuni kama vile voda nk ambayo wakubwa weingi ni wazamini.
  Nini cha kufanya ni juu yetu kutafuta mustakabali wetu.
   
 8. S

  Simba Yuda Member

  #8
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna urazima wa kufanya maandano kama SA
   
Loading...