Utumwa huu wa fikra utakoma lini!

Utumwa huu wa fikra utakoma lini!

mashaka-jr

Member
Joined
Apr 28, 2012
Posts
26
Reaction score
2
Ndio kwanza nimemaliza kusikiliza kipindi cha "THIS WEEK IN PERSPECTIVE " kinachorushwa na TBC1. Kipindi kimejadili mambo mengi mazuri, lakini la kusikitisha ni lugha iliyotumika ambayo ni Kiingereza, kisichofahamika kwa Watanzania walio wengi.
Hivi kweli vyombo vyetu vya habari vinafanya kazi kwa maslahi ya nani?
Kipindi hiki muhimu kilipaswa kuwa na manufaa kwa Watanzania wote. Kilipaswa kurushwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili inayofahamika na wananchi walio wengi.
Rai yangu kwa TBC na vituo vingine virushavyo vipindi muhimu vyenye taarifa muhimu kwa umma virushe vipindi hivyo kwa kutumia lugha adhimu ya Kiswahili.
Nadhani
ni muda muafaka wa kuondokana na utumwa wa fikra kwamba Kiingereza ndiyo lugha ya wasomi kutolea mada.
Wana jf naomba mchango wenu kuhusu hili.
 
Mkuu,wewe hujui kuwa bado tuna tawaliwa kiaina?.nadhni bado kazi ipo.Pia hata shule zetu watoto wanafundiswa kwa lugha isiyo yao.walimu hawaiwezi vyema je?watoto wetu wataelewa kwa kiasi gani?.
 
Back
Top Bottom