Posho City
JF-Expert Member
- Mar 15, 2012
- 648
- 416
Kwanza nianze kumshukuru Mungu kwa kuendelea kutupa uhai...
Mheshimiwa raisi wa Tanzania na waziri wa UTUMISHI najua huku mitandaoni mnapitia sana....Leo naleta kilio hiki cha sisi baadhi ya watumishi walimu wa shirika hili la umma la elimu Kibaha..
Hili shirika lina idara mbalimbali ikiwemo idara ya elimu ambayo inaendesha shule tatu za Kibaha wavulana...Tumbi sekondari na Kibaha wasichana...
Katika shule hizi za shirika baadhi ya walimu na walio wengi tuna kilio cha muda mrefu kabisa na ni kama sasa tumefikia hatua hatuoni msaada....Kilio chetu ni kama ifuatavyo
•Kuna baadhi yetu tunaomba raisi utoe ruhusa na katibu wa Utumishi atoe maelekezo kwa mwajiri wetu ili turekebishiwe mishahara...Baadhi yetu tumeajiriwa na shirika tukitokea shule za halmashauri mbalimbali....mishahara ya huku na halmashauri ni tofauti...Hili shirika lipo mjini...maisha yapo juu...nyumba za kupanga n.k
Lakini wengine tuna miaka miwili...mwaka mmoja ingawa tupo shirika lakini bado tunalipwa mishahara ya halmsahauri yaani kwa scale za tgts badala ya ptss....Na kwa sasa tukiuliza jibu ni kuwa hawajapata ruhusa...
Juzi afisa utumishi wetu kampigia simu mkurugenzi mkuu wa utumishi akatwambia wale walioko vyuo vya elimu ya juu ndio wamerekebishiwa mwezi March 2017 na sisi tuendelee kuwa wavumilivu..Kwakweli tunaishi maisha ya shida na ukizingatia huo mshahara ndio serikali inakata hadi 15% za HESLB..Tunaomba na sisi turekebishiwe mishahara ili tufanye kazi kwa amani..
•Pili hili shirika walimu tunaoajiriwa kwa cheo cha afisa elimu msaidizi tangu mwaka 2014 tunakosa haki yetu ya kuingizwa kwenye mfumo kwa kitu tunaambiwa hakuna JOB CODES za hicho cheo katika shirika hili....Sasa tunajiuliza kama hawana hizo codes kwanini wanaajiri walimu wenye sifa Za kuwa na cheo hicho?.
Pia katika shirika hili watumishi walimu mambo mengi hayako sawa mfano kuna walimu hawajawahi panda vyeo hapa tangu mwaka 2010....Waziri Simbachawene hili analijua lakini hatuoni utatuzi...
Kwakweli haya mambo yanatukatisha tamaa hadi tunatamani kurudi shule za halmashauri maana shule za shirika licha ya kwamba tunalipwa mshahara mkubwa na mazingira mazuri ya kazi lakini tunaishia kulipwa mishahara ya halmashauri miaka nenda rudi na vikwazo vingi bila kuona mwanga wowote