utumishi wa umma huwa wanatoa majina kwenye web yao kwa wale waliochaguliwa,baada ya kutoa majina kwa nafasi zilizokuwa zimetangazwa huwa kuna watu ambao huwa wanakuwa wamefikisha vigezo vyao vya ufaulu na hawa huwa wanapigiwa simu kwa nafasi ambazo hutokea ambazo hazikutangazwa kablaWadau ,je utumishi humpigia simu kila aliechaguliwa kuingia kazini baada ya oral interview ?
Je,kama hupiga simu ,je hupiga kabla au baada ya matokeo ya oral?
Hua wanapiga simu kwa wale ambao wanapata kazi kwa kupitia database ,yaani walikua kwenye database yao kama wa akiba ndio wakapata kazi
Kama nilifanya interview na sikuwepo kwenye majina ya kupangiwa vituo vya kazi, inawezekana nikawa nimefeli au nimekosa nafasi. Nitafahamu vipi Kama nimewekwa kwenye kanzidata (database)?