Utumbo chukuchuku kwa chapati za maji

akilimalikisuse

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
266
Reaction score
139
Tafadhali wana jamvi,mwenye kujua namna ya kupoka chakula cha utumbo chukuchukuku na chapati za maji anisaidie,Nimetumia neno chukuchuku nikiwa na maana (isiwe na mafuta wala maviungo viungo mengi)
 
Unaosha vizuri sugulia Na ndimu kupunguza harufu kali ya utumbo.

Katakata vipande

Weka tangawizi Na saumu vilivotwanga pamoja Na chumvi.

Piilipili manga Na uzile.

Changanya ivo viungo vyote weka kwenye moto chemsha huku unakorogea visiungue.

Weka maji wastani uwe unaongezea ongezea hadi uwe laini.

Karibia dakika 10 kuepua weka ndimu.na pilipili ongeza Na chumvi kama itahitajika.

Epua enjoy .

Unaweza kuweka Na veggies upendazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…