Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,665
- 239,157
Taarifa zinazosambaa kwa kasi ya moto wa nyika zinaonyesha kwamba , yale maombi ya wana Kyela ya miaka yote ya kuomba kwa Mungu wao ili awezeshe kusambaratika kwa Chama cha Mapinduzi , hatimaye yamejibiwa .
Kamati ya siasa ya ccm Mkoa wa Mbeya , imewasimamisha na kupendekeza kuvuliwa uanachama madiwani MACHACHARI wanne wa chama hicho katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela , kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Madiwani hao ni Lameck Mwambafula (bujonde ) , Fyuda Msusi ( Katumba songwe) , Emmanuel Mwandambo ( Ndandalo ) na Furaha Mwasongela ( Mababu ).
Taarifa zinadokeza kwamba hawa ni miongoni mwa wale 19 wa ccm , walioshirikiana na wale 12 wa Chadema kumng' oa Mwenyekiti wa Halmashauri , ambaye pia amebatizwa jina jipya la " MCHWA " kutokana na uwezo wake wa kutafuna hela za umma , aitwaye Hunter Mwakifuna , diwani wa kata ya Ipinda .
Ikumbukwe kwamba pendekezo la kuwavua uanachama limepelekwa kwenye vikao vya juu ambavyo huongozwa na yule jamaa asiyetaka kuona Ng'ombe waliokatika mikia .
Tuendelee kusubiri .