UTU wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UTU wa Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Azimio Jipya, Apr 25, 2011.

 1. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Julius Kambarage Nyerere, kwa moyo wake wote, fikra zake zote, kauli na vitendo vyake alipigania na kutetea Utu wa Taifa la Tanzania.

  Utu wa Taifa ni heshima ya Taifa, Ni uzalendo wa taifa, Ni Uimara wa Taifa

  Utu wa Taifa unajengwa kuanzia mwananchi mmoja moja na mifumo yake yote ya jamii, Jk Nyerere alihaikikisha hilo, mifumo ya afya, kilimo, elimu, ulinzi siasa na jamii nzima kwa moyo wake wote alijitahidi kwa uwezo wake wote kuipelekea njia hiyo na maisha yake yeye mwenywe yaliwakilisha njia aliyokuwa anaipeleka Nchi …Kwenye kiwango cha juu cha UTU WA TAIFA!

  Thamani ya Utu wa mtu hainunuliki kwa gharama yeyote. Upewe nini ili kuuza utu wako? Ni mali kiasi gani mwanadamu anaweza kupewa ili Kuusaliti utu wake? Enzi hizo jibu lilikuwa wazi ... Leo Sijui!! Yaani upewe nini ilikuuza Utu wa Tiafa? Hili ni swala la kujadiliwa.

  Kuutetea Utu wetu hata ikibidi kukosa marupurupu kadhaa na na faida mbalimbali ni jambo la heshima na dhibitisho la uasilia wa Mwanadamu na heshima ya Taifa La Tanzania.

  Kujitoa muhanga kwa kiasi hiki si sifa ya Fisadi yeyote , Si sifa ya Kiongozi Mbabaishaji , si sifa ya kiongozi anayelenga Kujinufasha yeye na familia yake.


  Kati ya vyama vikubwa CCM, CHADEMA na CUF ni kipi kitaweza kubeba Mzigo Huo? Kipi kina muelekeo wa kutufikisha Kwenye kuuenzi na kuufufua Utu wa Taifa, amabao sasa uko mazikoni?


  Kama hakuna mtu au chama chenye uwezo wa Kutetea Utu wa Taifa na kuujenga utu wa Taifa ..Ni vuguvugu gani lifanyike kuikomboa Tanzania… Kiutu na Kimaadili?


  Leo ni nani anaweza kuchukua nafasi ya Mwal Nyerere katika kuendeelza harakati za ujenzi wa Utu wa taifa la Tanzania ?

  au

  Ni nani anaweza kuchukua nafasi ya Hayati Eduadi Morenge Sokoine katika harakati za ujenzi wa dhati wa Utu wa taifa letu?

  NI WEWE?

  Ni Mh Mkapa, Mh Mwinyi, Mh Kikwete, Dr Slaa, Mh Mbowe , Prof Lipumba … ? Au ni nani yeyote amabaye sijamtaja hapa?
   
 2. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nikazi sana ndugu yangu kwani hali hilivyo tz balaa. Kila siku najiuliza na kumwomba mungu tuweze pata kiongozi kama mwenda wazimu ambaye yupo teyari kuongoza tz kama enzi za mwalimu nyerere. Leo hii hata hvyo vyama vyaupinzani bado wengi waviongozi ni maslahi binafsi. Kunawachache ambao kweli wanafikra za mwalimu lakini hakuna wakuwasapoti.
  Nashauri kama vijana wakitz tukiamua kuungana na kuwanaumoja wetu, tupambane na sekta zote nazani nchi hii tutarudisha utu wetu. Lakini bado napata tabu kwani hata sisi vijana wengi wetu bado tunataka maisha ya haraka leo namaliza chuo nataka niwe na gari/nyumba na maisha ya juu kweli hapo tutafika?
  Tukipinga kwa kauli moja nazani vijana tunauwezo wakuibadilisha tz na kuwa mpya naomba tuachane na siasa tujikite katika kuelimisha jamii na kudai haki hata kama zitachelewa tukomae tu.
  Leo wanataka kuandaa katiba mpya hivi bado tunakubali tu mchakato unavyoendeshwa ambao hautabadilisha kitu kama tusipo kuwa macho hali itabaki hilehile.
  Naomba vijana watz tuliopo duniani kote tushikamane na kuakikisha tz inakuwa ni nchi ya maendeleo ya kweli na sio siasa ambazo zinasaidia familia chache tu.
  Leo angalia bungeni asilimia kubwa ni familia zilezile tangia enzi hizo. Angalia wizarani bado utakuta majina yaleyale tu, angalia kwenye mahakama/majeshi/ mavyuoni bado watu wanachaguana kutokana na kujuana bila kujali jamaa ni mbovu kwenye nafasi yake. Jamani naomba vijana tuache ushabiki wa kisiasa na tushikamane nakuakikisha tz inapaa na kufikia kipindi cha mwalimu.
  Hata kama mtanipinga lakini mm sijivunii kuwa na madini, mbuga za wanyama, milika na maporomoko wakati havitusaidii sisi wananchi wa hali ya chini.
  Leo hii migodi kibao inafunguliwa lakini ukiuliza kiasi gani cha madini kinazalisha na kusafirishwa kila siku hakuna ukweli wowote hapo. Miaka 50 sasa hakuna umeme tz wakuaminika bado tunategemea mvua jamani hivi utasema tunaserikali au?
  Tunaacha kupambana na mazalia ya mbu tunakomaa na kugawa vyandarua kweli hapo ni sawa? Nazani inabidi tz tubadilike jamani tuachane na kuoneana aibu hapa,vijijini wananchi wanafariki kwa magonjwa yanayotibika alafu tunasema mungu kapenda kweli mungu anatupenda sana sisi tufe lakini awapendi wazungu au wachina au wajapani? Embu tuachane na fikra za ajabu.
  Yani ninamambo mengi sana ya kusema lakini ngoja nikomae na kazi nikirudi tutapeana wito zaidi. Najua wapo vijana mawazo yao yatakuwa tofauti namimi na wataponda lakini ukweli ndo huo na pia tunakuja sasa hakuna kulala na kama bado mnafikili dunia ya leo kwamba kama mzazi wako ni kiongozi basi na wewe lazima huwe kiongozi hiyo haipo.

  Tanzania mpya inakuja, vijana tupambane na fikra mbovu.
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Rugambwa ..Tunafikaje huko? ..Nani atuongoze?
   
 4. e

  emma 26 Senior Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania ndo tulichobakiza kazi ni kulaumiana tu
   
 5. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tunaitaji Rais Dikteta na utawala dikteta katika kusimamia sheria ambazo tumejiwekea wenyewe.Kama sheria inasema usikojoe hapa basi iwe kweli,kama sheria inakataza ujenzi wowote pasipo kibali cha mamlaka husika basi kweli sheria iwe hivyo,kama hakuna ruksa kunywa pombe kuanzia asubuhi mpaka saa kumi jioni siku za kazi na iwe hivyo.Najua itakua udikteta lakini tutafika sehemu kama Taifa tujiona na kutambua faida za kuzingatia utwala wa sheria.
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  DSN;

  Nikisema yafuatayo upi utakuwa ni mtizamo wako?

  Ni kweli kuwa kutetea utu wako au wa familia au wa taifa lazima kujitoa muhanga kwa namna fulani kuweko.

  Kutetea utu wa familia yako ili binti au mke asidhalilishwe kijinsia mbele yako ...ni wajibu wa Baba yeyeyote mwenye utu na maadili yake.

  Nayasema haya kwani hata inapokuja kwenye kuutetea utu wa Taifa Baba wa nchi na waasaidizi wake hawana budi kujitoa muhanga, tena kwa dhati bila kubabaisha hata kidogo.

  Kuutetea utu wa taifa Raisi Kikwete

  Afanye alichofanya marehemu Edward Moringe Sokione wakati wa operewsheni ya wahujumu uchumi.

  Ni rahisi kabisa....

  Sasa hivi awakamate ..wote pale CCM wanaodaiwa kuhujumu utu wa taifa...

  Huwezi kumbembeleza Mtu anayeubaka uchumi wa nchi huku ukifikiri unaeleza utu wako.

  Awakamate na kuwaweka gerezani huku wakifunguliwa mashitaka....kwani hakuna uchunguzi wa kufanya vyote viko wazi kabisa.

  Awakamate huku wakiwa gerezani ....mali zote walizoiba ..zitaifishewe... Kuanzia fedha za kagoda, rada, EPA, richmond ..nk

  Nasema kuutetea utu wa mtu binafsi, familia na taifa sio lele mama...Lakini kuacha taifa likifedheka ni Kinyume na utu wa mwandamu ni dhambi kubwa... na si ajabu karibuni tukashindwa kutetea utu wa watoto wetu na wake zetu kwenye familia ...
   
 7. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Utu wa taifa na azimio la arusha vyote vina maana TAIFA LISILO NUNULIKA...

  Ni kiongozi gani wa Tanzania leo ..hanunuliki ..?
   
Loading...