Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,363
- 1,135
Julius Kambarage Nyerere, kwa moyo wake wote, fikra zake zote, kauli na vitendo vyake alipigania na kutetea Utu wa Taifa la Tanzania.
Utu wa Taifa ni heshima ya Taifa, Ni uzalendo wa taifa, Ni Uimara wa Taifa
Utu wa Taifa unajengwa kuanzia mwananchi mmoja moja na mifumo yake yote ya jamii, Jk Nyerere alihaikikisha hilo, mifumo ya afya, kilimo, elimu, ulinzi siasa na jamii nzima kwa moyo wake wote alijitahidi kwa uwezo wake wote kuipelekea njia hiyo na maisha yake yeye mwenywe yaliwakilisha njia aliyokuwa anaipeleka Nchi …Kwenye kiwango cha juu cha UTU WA TAIFA!
Thamani ya Utu wa mtu hainunuliki kwa gharama yeyote. Upewe nini ili kuuza utu wako? Ni mali kiasi gani mwanadamu anaweza kupewa ili Kuusaliti utu wake? Enzi hizo jibu lilikuwa wazi ... Leo Sijui!! Yaani upewe nini ilikuuza Utu wa Tiafa? Hili ni swala la kujadiliwa.
Kuutetea Utu wetu hata ikibidi kukosa marupurupu kadhaa na na faida mbalimbali ni jambo la heshima na dhibitisho la uasilia wa Mwanadamu na heshima ya Taifa La Tanzania.
Kujitoa muhanga kwa kiasi hiki si sifa ya Fisadi yeyote , Si sifa ya Kiongozi Mbabaishaji , si sifa ya kiongozi anayelenga Kujinufasha yeye na familia yake.
Kati ya vyama vikubwa CCM, CHADEMA na CUF ni kipi kitaweza kubeba Mzigo Huo? Kipi kina muelekeo wa kutufikisha Kwenye kuuenzi na kuufufua Utu wa Taifa, amabao sasa uko mazikoni?
Kama hakuna mtu au chama chenye uwezo wa Kutetea Utu wa Taifa na kuujenga utu wa Taifa ..Ni vuguvugu gani lifanyike kuikomboa Tanzania… Kiutu na Kimaadili?
Leo ni nani anaweza kuchukua nafasi ya Mwal Nyerere katika kuendeelza harakati za ujenzi wa Utu wa taifa la Tanzania ?
au
Ni nani anaweza kuchukua nafasi ya Hayati Eduadi Morenge Sokoine katika harakati za ujenzi wa dhati wa Utu wa taifa letu?
NI WEWE?
Ni Mh Mkapa, Mh Mwinyi, Mh Kikwete, Dr Slaa, Mh Mbowe , Prof Lipumba … ? Au ni nani yeyote amabaye sijamtaja hapa?