mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 917
- 1,997
Nikiwa Home nikiwaangalia watoto wangu naona kama utoto wao hauna kashikashi nyingi kama enzi zangu. Nikikumbuka enzi zile malezi yake kama jeshini vile..na taarifa nyingi tulikuwa tunafichwafichwa.
Mfano
(1) Akizaliwa mtoto Home, mnadanganywa mama ameenda kumnunua mtoto hospitali.
(2) Shuleni likipita gari la msalaba mwekundu, mwanafunzi mmoja akapiga yowe Mumianiiiii, nyonya damuuu, basi siku hiyo shule hamna masomo tena ni mbio kila kona.
(3) Kuna siku tulifungiwa maandazi kwenye gazeti la lugha la kiarabu mbaba mmoja akatutisha msile mtakuwa vichaa hiyo ni QURAN hiyo tukayatupa maandazi
(4) Mkitaka mpira wa miguu basi inabidi mkaokote Lylon kwenye maduka ya wahindi mtengene mpira ndio mcheze.
Lakini hawa Makamanda wetu wa Kidigitali Daah mambo yao soft sana, mpira wanataka uwanunulie dukani, hawajui hata Manati kazi yake nini, hata kuchomwa na miba za mbigiri miguu haziwachomi kutwa wamevaa viatu, hata mafunza miguuni hayawaingii.