Utofauti wake na Watawala wengine Afrika au Duniani

Utofauti wake na Watawala wengine Afrika au Duniani

Joined
Feb 22, 2013
Posts
14
Reaction score
9
MZEE MANDELA'S WISDOM

"Baada ya kuwa Rais, niliwataka baadhi ya walinzi wangu kwenda kutembea mjini.

Baada ya kutembea, tulienda kula chakula cha mchana kwenye mgahawa. Tulikaa katika moja ya mgahawa ulio katikati ya mji na kila mmoja wetu aliagiza alichotaka.

Baada ya kusubiri kidogo, mhudumu alituhudumia wakati huo nilibaini kuwa, kwenye meza iliyokuwa mbele yetu kulikuwa na mtu mmoja anayesubiri kuhudumiwa.

Alipohudumiwa, nilimwambia mmoja wa askari wangu: nenda ukamkaribishe huyo mtu ajiunge nasi. Askari huyo alifikisha mwaliko wangu.

Yule mtu akasimama, akachukua sahani na kukaa karibu yangu. Wakati wa kula, mikono yake ilikuwa ikitetemeka kila wakati na hakuinua kichwa chake wakati wa kula. Tulipomaliza, akanipungia mkono bila hata kunitazama, nikampa mkono na kuondoka!

Askari aliniambia:
"Madiba, mtu huyo lazima awe mgonjwa sana kwani mikono yake haikuacha kutetemeka wakati akiwa anakula"

"Hapana kabisa! Sababu ya kutetemeka kwake ni nyingine" - nilijibu.

Walinitazama kwa mshangao nikawaambia:

Mtu huyo alikuwa mlezi wa jela nililokuwa nimefungwa. Mara nyingi, baada ya mateso niliyofanyiwa, nililia na kuomba maji lakini alikuja kunidhalilisha, alinicheka na badala ya kunipa maji alikojoa juu ya kichwa changu. Hakuwa mgonjwa, aliogopa na kutetemeka labda akiogopa kwamba mimi, sasa kwa kuwa mimi ni rais wa Afrika Kusini, nitampeleka jela na kufanya vile vile alivyofanya nami, kumtesa na kumdhalilisha. Lakini sio mimi, tabia hiyo sio sehemu ya tabia yangu wala maadili yangu.

Akili zinazotafuta kulipiza kisasi huharibu taifa, wakati zile zinazotafuta upatanisho huunda Mataifa

Nelson Mandela
 
Back
Top Bottom