Jamar Said
Member
- Sep 2, 2015
- 19
- 35
Ni ukweli usiopingika kuwa Lowassa anajaza watu kwenye mikutano yake. Lakini katika siasa kinaangaliwa pia ubora wa mikusanyiko hiyo. Mikusanyiko ya Lowassa inaleta kumbukumbu za Mh Mrema mwaka 95, si kwamba Watanzania hawaelewi somo. Kuna watu aina mbili wafikao mkutanoni, kwa mfano: kuna wanaokwenda mkutanoni kumuangalia huyo Lowassa mwenyewe kwa macho yao na pia kuna wanaokwenda kuchambua sera za wagombea. Kwa sasa Lowassa hajawa na jipya la kuwaambia watanzania na kuwapa matumaini halisia.
Ukweli Lowassa, hata kama Watanzania wangekua hawajaamka na wakafanya makosa kumchagua, Lowassa kwenye moyo wake angelimuhitaji Magufuli amsaidie kuendesha Serikali ili kazi ya kweli ya kujenga nchi na watu wakaiona inafanyika inavyotakiwa iwe. Hata hivyo Watanzania wengi ambao ni wapiga kura vilevile hufikiria kama Lowassa, Wanamtazama Magufuli kuwa kwa sasa ndio mtu wa kwenda kunyoosha mambo.
Sasa kuna kikwazo gani cha Watanzania wenyewe kumchagua Dr John Pombe Magufuli kwa maana katangaza nia thabiti ya kuikomboa nchi ya Tanzania. Kuna ambao hawapendi kiongozi mwadilifu na mfuatiliaji, lakini kwa mtu wa kawaida kama mimi ninaeishi Tandahimba na kwa kuwa tuko wengi tunaomuona huyu Magufuli kuwa ndiye atakaekua mkombozi wa kweli kwa wanyonge wa nchi hii, basi kura yangu ni yeye. AMENI