Utitiri wa wachina kariakoo: Hongera JK kuleta wawekezaji...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utitiri wa wachina kariakoo: Hongera JK kuleta wawekezaji...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchemsho, Jul 19, 2011.

 1. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  serikali ya mkuu wa kaya imeufyata kabisa kutimua wavamizi wa kichina waliorudikana soko kuu la kariakoo wakipora Frame za wazawa kwa bei za kupaa, huku wakitumia frame hizo kuuza viatu na mitumba uchwra ambazo hata wafanyabishara wazawa wanamitaji na wamekuwa wakizifanya..JK fanya maamuzi magumu utimue Wachina kariakoo kwa kuwa wanadumaza sana wafanyabiashara wazalendo....hii ni taarifa tu.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,690
  Likes Received: 82,554
  Trophy Points: 280
  We subiri miaka 10 mpaka 15 ijayo hawa watakuwa wameiteka nyara Tanzania na jinsi population yao ilivyokuwa kubwa tutabaki tunalia na kusaga meno nchi imetekwa na Chinese. Wengine ukisema hivi wanakuona racist.
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa ana-implement strategies zake za kiswahiliswahili!!uwezo mdogo!
   
 4. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ha ha haaaaaa eti wawekezaji!!! wawekezaji wa kuuza karanga na maua ya plastic? Mi sijui tunaelekea wapi, aah niko tired ile mbaya, yaani nchi imevamiwa tunaibiwa mchana na usiku, tumekua shamba la bi kizee, tumejikalia watu wanaiba hata nguvu ya kuwafukuza hatuna lol!!!!!!!!!!!!!
   
 5. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mtavuna mlichokipanda November mwaka jana
   
 6. r

  rmb JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi ule muda aliotoa waziri wa hawa wachina wa kariakoo waondoke bado haujaisha?
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  subirini kwanza,
  hivi tukiwafukuza na wachina wakafukuza ndugu zetu kule nani atakula hasara?
   
 8. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ufaransa pana miaka ya 90 walianza kufukuza Waafrica kutoka kwao. Wakawakamata kibao na kuanza kuwatia kwenye ndege. Rais Bongo wa Gabon alitoa onyo kwa Ufaransa kuwa "kila M-Gabon mmoja akitua Gabon kutoka Ufaransa, yeye anarudisha Wafaransa 10".

  Wafaransa waliufyata na hadi leo hawawagusi Wagabon.
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  lazima tukubali dunia imebadilika
  mwenye kisu ndiye mla nyama
  mwenye akili ndiye atanusurika
  kama hutumii akili umekwisha,hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuia hili
   
 10. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hao ndugu zetu wanapata nini kule? Unadhani Wachina wanaruhusu uwekezaji wa kijinga
  kama tunavyofanya sisi? Wabongo walioko kule wanaganga njaa tu na kubadilisha mazingira
  lakini hakuna cha maana
   
 11. h

  housta Senior Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hao ndugu zetu kule wanaisaidiaje nchi yetu?Kwa lugha nyingine wana manufaa gani kwa taifa letu?Ni sisi tu tunawakombatia hawa watu.Nchi imekuwa ghala za bidhaa zenye viwango dhaifu na serikali imekaa tu kimya.Hakuna mtu anathubutu kufanya maamuzi.Tutaingia msituni,mark my words,tutaingia tu ili heshima iwepo.Kwa nini viongozi wasiwajibishwe?Nchi ipo kwenye crisis na Rais anakwenda SA kwenye birthday!Kwani ni lazima kusafiri?Kwa nini tunakuwa washabiki wa kisiasa na tunaweka maisha yetu kisiasa na siyo kibinadamu?Tuache upuuzi,lets ACT NOW!
   
 12. K

  Koba JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...haha haha eti bidhaa hafifu,wenyewe hata hizo hafifu hamzalishi sasa unataka watu watembee bila viatu,hizo TV,cellphone,computer mnazotumia bila huyo mchina hata hi JF usingeijua,acha wafanye biashara mpaka wazawa waanze kuzalisha, market forces will take care itself,na nani aliwaambia mkiwafukuza wachina ndio mtaendelea? na FYI watanzania kibao kule China wanasoma mengi tuu kuanzia medicine,Engineering,pharmacy etc kwa scholarship za hao hao wachina,na wengine wengi tuu wanafanya biashara..unafikiri hivyo vitu vyote kuanzia machinery,electronix etc made in china vinaletwa na wachina tuu? ni hao hao wabongo wenzako ndio waagizaji wakubwa wewe lala tuu na siasa zako uchwara..dunia imebadilika hakuna tena ujamaa wa kukulinda!
   
 13. K

  Koba JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..sio lazima kuandika,kama hujui bora ukae kimya,kukusaidia tuu kuna wanafunzi watanzania maelfu wanasoma vitu vya maana kwa pesa za wachina na wengine wengi tuu wanafanya biashara very legal,unafikiri macontainer maelfu yanayoingia from china kila mwezi pale bandarini ni ya waganga njaa,mnapiga kelele bidhaa fake lakini cha ajabu hakuna hata factory moja ya kutengeneza CD or any electronix equipment kama TV or computer hapo Dar es salaam...sanasana hata hivyo viwanda vyenu vya kupika mikate na sabuni vinafungwa sasa hakuna umeme,kufukuza wachina nakuhakikishia wengi wenu mtaishia kuishi life substandard..i doubt kama 99% ya wabongo mnaweza kununua anything made in Germany/Britain/US,bora mjitahidi na mshukuru hizo bajaji na fong fong or whatever maana BMW,Range or Lincoln will never happen,nakushauri waambie wenzako muingie mtaani kubadili katiba na mgawo wa umeme,rushwa kuliko picking a fight with chinese
   
Loading...