leipzig
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 2,766
- 1,714
Nashukuru mtoa uzi huu, imefika wakati wa kudhibiti kuwepo kwa mabaa mitaani. Unakuta baa iko mtaani inafunguliwa mapema tu inapiga muziki kuanzia mchana huo hadi usiku wa manane pamoja na hayo kuna matukio ya aibu yanayofanyika hata mbele ya watoto wadogo.
Isitoshe mitaani kuna wagojwa na hata watu wengine wasiopenda makelele wanahitaji kupumzika, wengine wanahitaji kujisomea lakini kutokana na vurugu na adha ya mabaa mtaani inakuwa kero kubwa kwao na huku hawana kauli.
Naomba serikali yetu ilione hili na kuiga uamuzi wa serikali ya Ruanda kupiga marufuku mabaa ya wazi mitaani badala yake zifunguliwe pub za ndani kwa ndani kama ilivyo katika sehemu nyingine hapa mjini kama Tabata, Sinza nk. Hii pia itasaidia kudhibiti watoto wadogo kujihusisha na ulevi na kulinda maadili ya watoto wadogo.