Uthubutu wa Rais Magufuli...

Maghufuli atabaki kuwa icon kubwa sana, time will tell, ana mapungufu yake ila ni raisi wa aina yake ,hawa hawa wanaomlaumu ndo watakuwa wa kwanza kumkumbuka jamaa,
Ipo siku utashuka tu kutoka kwenye gari la huyu mtu. Subiri awamu ya pili utaona.
 
Hoja yako inanikumbusha jukwaa la siasa kuanzia 2013 kurudi nyuma.

Uchambuzi wa siasa wa aina hii ulikuwa ni suala la kawaida wakati huo lakini sasa hoja kama hizi zimekuwa ni kama mnyama kakakuona!

Nikirudi kwenye hoja yako. Ni kweli taifa letu lina tatizo la uthubutu.

Hata huyu Rais Magufuli nimemsikia akiwaambia watendaji wake ni afadhari unathubutu na kutenda hata kama utakosea lakini unakuwa umetenda.


Kutokuwa na uthubutu nchini imekuwa kama tabia/haiba na utamaduni.

Watanzania wengi ni wapole sana. Upole na uthubutu haviendi pamoja.

Nadhani haiba inayoenda pamoja na uthubutu ni ruthless.

Ndio maana imefikia hatua baadhi ya watu wanadai Rais Magufuli hana Utanzania kwa sababu ni ruthless.

Watanzania wengi wanajua sana kuongea kuliko kutenda. Nahani hii imetokana na historia ya taifa letu.

Rais Magufuli ana mapungufu yake lakini uthubutu siyo moja ya mapungufu kwake.
 

Duh!

Mzee upo?
 

Wakati ukiandika haya nakukumbusha tu:

1. Lissu alipigwa risasi 16 na nyingine zaidi ya 20 zikimkosa
2. Ben Saanane kapotea
3.Azory Gwanda kapotea
4.Akwilina alikufa kwa risasi
5. Kamanda mawazo alikufa kwa mapanga
6. Roma mkatoliki alitekwa
7.Kada Chadema wa kata ya Hananasif aliokotwa amekufa coco beach
8. Msaidizi wa Membe alitekwa
9. Mo alitekwa

Nikija kwenye mada sasa:
  1. Uthubutu wa kutumia pesa za umma kufanya manunuzi bila kufuata sheria za manunuzi ya umma, lini tender ya bomdia ilitangazwa kama sheria ya manunuzi inavyotaka?
  2. Kwa nini ATCL aiweke chini ya ofisi yake ili isikaguliwe na CAG?
  3. Kwa nini atuondolee bunge live halafu LIve awe yeye Ikulu?
  4. Kwa nini atumie Jeshi kutwaa korosho za wananchi halafu asiwalipe pesa zao?
  5. Kwa nini atumie nguvu nyingi kuminya na kuwabana wapinzani wasitumie haki yao ya kikatiba kufanya siasa?
  6. Kwa nini atengeneze sheria kandamizi za vyama vva siasa, sheria ya takwimu, sheria ya habari n..k

Mleta mada, huo ndo uthubutu unaousema?
 
Uthubutu si lazima tuutazame kwa matokeo chanya pekee, hata matokeo hasi yanaweza kutokea kutokana na mtu kuwa na uthubutu, kudhamiria na kufanya lile alilokusidia.
Rev. ni vizuri kukusoma mara moja moja hivi.

"UTHUBUTU," kwa hakika Magufuli ni mtu wa kufanya mambo kwa 'uthubutu.' Ni mtu mwenye kuitumia dhana ya 'in your face' kisawasawa bila kujali matokeo yake yatakuwa vipi.

Ni kweli kiongozi anayetumia 'uthubutu' hasa katika mambo kadhaa wa kadhaa huweza kuleta mabadiliko makubwa na ya haraka, kwa sababu ule uchelevu unaoletwa na njia za majadiliano 'deliberations' huwa umeondolewa. Lakini hapo hapo kama 'uthubutu' unakuwa ni wa kimakosa, hapo ndipo husababisha majanga makubwa kwa nchi.

Uthubutu anaofanya Rais Magufuli unaogusa uvunjifu wa taratibu, sheria na hata Katiba ya nchi, huo ni 'uthubutu' mbaya kabisa, bila kujali matokeo ya 'uthubutu' huo. Nchi ni lazima iendeshwe katika misingi iliyojiwekea. Haiwezi kutifuliwa tu na 'mtu mmoja eti kwa sababu tu yeye anauthubutu. Hali hiyo huleta vurugu.

Nikiandika haya bila kuweka mifano sitaeleweka..
1. Uthubutu wa kujenga Stieglers' gorge. Ni uthubutu mzuri kwa mtizamo wangu na ninauunga mkono. Lakini anapolazimisha taratibu zisifuatwe wala kusikilizwa katika maswala ya mazingira, panakuwa na dosari. Wasikilize wenye maoni ya utaalam wao, na jitahidi kuelewa wanayosema na uyapime vizuri. Mradi kama huo wenye thamani kubwa kwa taifa hauwezi kuzuiwa na kampeni za kelele tu toka ndani na nje. Mwisho wa siku, mradi unajengwa lakini sio kwa mtindo wa "in your face" anaopenda sana kuutumia.

2. Ujenzi wa International Airport ya Chato. Ni nani anayejua chimbuko la maamzi hayo na jinsi mipango ya utekelezaji wake ulivyofanywa? Bunge walikuwa na taarifa. Walipitisha matumizi ya Tsh 39 billion. Hela hiyo ilipatikana toka wapi?
Kulikuwa na sababu yoyote ya lazima kujenga mradi mkubwa wa kiasi hicho katika eneo hilo? Kulifanyika upembuzi wowte wa kitaalam kuonyesha faidi itakayotokana na mradi huo?
Huu ni 'uthubutu' mbaya moja kwa moja.
Watu hapa wanasema Chato ni Tanzania pia, inahitaji miradi. Nasema sawa kabisa; lakini hapakuwa na miradi bora zaidi ya huo?
Tsh39 bilioni, uwekeze kwa nguvu za wanaChato. Wale wakulima, wavuvi, wachimba madini ...tena basi unahakikisha wananchi hawa miradi watakayosaidiwa kuifanya iwe darasa kwa maeneo mengine nchini. Kama ni kilimo wataalam wanamwagwa pale kutumia utaalam wao wote wa kilimo kuhakikisha kilimo cha hawa wananchi wa Chato kinakuwa ni cha mfano hasa. Miaka miwili mitatu, Chato inakuwa tofauti kabisa na eneo lingine lolote nchini katika maendeleo ya kilimo. Wananchi wakishajua kilimo bora inabaki tu kusimamia mwendelezo kilimo kiwe 'sustainable'. Baada ya hapo hata ujenzi wa International airport unaweza kuonekana ni wa maana.

Hii ni mifano miwili inatosha kuhusu hii dhana ya kufanya maamuzi kwa 'uthubutu'. Ipo mifano mingi sana sasa inayoweza kutolewa kutokana na uongozi wa 'uthubutu' wa rais Magufuli.
 

Nimekupa like I wish tungekua tunaweza kutoa likes nyingi lol
 
Nimekupa like I wish tungekua tunaweza kutoa likes nyingi lol

Ile kuvunjavunja nyumba za wananchi wa kimara na mbezi halafu hata hela za kujenga hizo barabara kumbe hana mleta mada anaona ni bonge la uthubutu!- ajabu sana!
Kuna uthubutu wa maana na uthubutu usio wa maana, kama huu wa kuvunja nyumba za watu na kuwatia umasikini wakati hata hela zenyewe za mradi huna siyo uthubutu ni kukurupuka!
 
Kizazi cha majanga. Kila kitu ni uvivu mbele. Watu waandika vitabu sembusi hizi sentensi mbili. Na mbaya zaidi unaweza kukuta ni mhitimu wa chuo kikuu ndiyo mwenye haya mawazo! Elimu yetu iko kuzimu
Nina mtizamo tofauti na wako kumhusu huyo jamaa anayetaka mashine inayo-type' maneno anayoongea.
Huyu jamaa amaona tatizo, kinachotakiwa ni kuweka akili katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, Uvumbuzi huanza hivyo.

Je mkuu, unajua kama kuna "mashine zinazotaipu maneno anayosema mtu'? Kama hazipo, je zikivumbuliwa kutakuwepo na watu watakaopenda kuzitumia?

Binafsi swali lake hilo mimi limenifikirisha sana, na kujaribu kupata jibu. Sijui jibu. Ni ajabu sana na teknolojia yote hii tuliyonayo sasa mashine hizi hazipo! Kuna sababu ya kutozivumbua, kwa sababu najua pesa nzuri ipo hapo kwa mvumbuzi!

Waziri wa Kaskazini, usiachie 'chance' hii.
Jamani sorry naomba kuuliza, hivi kuna machine za mtu kuongea zinyewe zika type unacho ongea?
 

Umemsoma vizuri Rev. lakini?

Mimi kama nimemuelewa vizuri, yeye kazungumzia uthubutu tu, bila kujali sana matokeo ya huo uthubutu!

Hebu msome vizuri tena...
 
Umemsoma vizuri Rev. lakini?

Mimi kama nimemuelewa vizuri, yeye kazungumzia uthubutu tu, bila kujali sana matokeo ya huo uthubutu!

Hebu msome vizuri tena...

..nadhani nimemsoma vizuri.

..na ameeleza uko uthubutu ambao matokeo yake ni mabaya.

..na mfano ni huo nilioutaja ktk bandiko langu uliloninukuu.

..uthubutu mwingine ni wa kununua ndege. So far shirika la ndege linajiendesha kwa hasara.
 

..labda ni uchanga wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

..hili neno "UTHUBUTU" halijajitosheleza kueleza alichotaka kueleza mtoa mada.

..Waingereza wangeweza kusema mhusika ni " BOLD."

..au huyu mhusika ni "RECKLESS."

Nyani Ngabu
 
Reverend, nilipotoa maoni mwanzo nilikuwa sijasoma bandiko lako lote hadi mwisho. Sasa nimelisoma lote.

Hapana, mengine si kweli kama hilo nililo'quote hapo juu.

Unakumbuka maamzi ya kuhamia vijijini? Unakumbuka elimu ya UPE; unakumbuka, hata ushiriki wa Tanzania katika ukombozi wa nchi zilizokuwa bado zinatawaliwa? Haya yote utayaita nini, kama sio 'uthubutu' ulioongozwa na kusimamiwa na kiongozi mwenye 'uthubutu' wa kushirikisha viongozi wenzake ndani ya chama na serikalini.

Haya yote yalifanyika katika 'taratibu za vikao.' Hayakuwa maamuzi ya 'uthubutu' tu wa mtu mmoja. Ndio maana pakawepo na 'a lasting legacy' ya maamuzi mazito kama hayo. Kiongozi alisimamia 'uthubutu' wa kufanya mambo kama taifa, sio 'uthubutu' wa mtu mmoja kuliburuza taifa zima.
Tena mengi ya haya yaliamuliwa ndani ya chama, na maamuzi hayo kushuka chini hadi kwa wananchi na kuyajadili katika vikao vyao huko huko vijijini.

Magufuli akidondoka leo, ni nini kitakachobaki alichokifanya kwa 'uthubutu' wake binafsi! Ufisadi, rushwa, nidhamu? kazini. Hayo ni mafanikio kweli? Kuna mfumo wowote wa kuyaendeleza haya hata Magufuli akiwa hayupo? Ile international airport itadumu kule Chato?
 
Nianze kwa kutoa Shukrani kwa michango na maoni tofauti ambayo imefanikisha lengo langu kuandika makala hii.

Natambua wazi hisia tofauti na hata mapokeo ambayo ama yameudhi au kufurahisha upande mmoja au mwingine.

Hivyo hamaki (reaction) ni kitu nilikitegemea na kukusudia.

Swali langu kwa wote; hitimisho langu linatoa mbiu kwa kila mmoja wetu kuwa na Uthubutu kudai haki, kusimama imara bila kuruhusu kunyanyaswa au kuwa wanyonge.

Je wote tukipata uimara na uthubutu huu, manyanyaso tuliyoshuhudia miaka 25 tangu tuachane na siasa za chama kimoja zitaendelea?

Ujeuri wa kimamlaka, kiburi na ubabe kutudharau kungeendelea?

Tuendelee kuitafakari dhana ya Uthubutu kwa kina kabla ya kufanya assessment ya kama aliyofanya Magufuli ni manufaa au uthubutu ulikuwa sahihi au la!

Leo tukipata kwa ujumla uthubutu wa kukataa kutawaliwa na CCM... tungekuwa tunaburuzwa?
Nyani,

People forget I could write in details to criticize Magufuli and list all his failures with such an ease and it will simply be a bitch rant similar to all that has already been said about him for last 20 plus years since he became a politician and now a president.

I chose to use a different prism to construct this piece, making it a thought provoking and it ain’t about Magufuli and his misdeeds nor praising him that he can get things his way...

One has to be Familiar with my writing and thought provoking style... it ain’t about him... it’s about us...!
 

💯%.

Now folks can see why some of us missed your presence!

Don’t be a stranger no more!
 
Uthubutu gani huo wakusubiri mpaka jeshi, polisi, mahakama, tiss, takukuru na bunge viwe upande wake.

Kipindi nchi inaliwa wakati wa mkapa yuko kimya, pia wakati kikwete yuko kimya, na sasa hivi kipindi chake yuko kimya, sana sana anaishia kupiga kelele nchi imetafunwa sana hii na huchukui hatua zozote, lakini wakina lisu na mbowe na wwngineyo kutwa kuwafungulia kesi mahakamani na kutaka kuwaua juu.

Ndugu jitahidi utapata hata ubalozi au ukuu wa wilaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…