CHIPESI NAMISUKU
Member
- Oct 7, 2019
- 51
- 157
Kuelimisha ni jambo jema, na shabaha ya kuelimishana ni kusaidiana ktk kupata maarifa mbalimbali ili maarifa hayo yatusaidie kup
ata mwanga wa kuondoa giza la ujinga lililotamalaki vichwani mwetu.
Katika tabia za wanadamu, usije kuona aibu kuitwa mjinga, maana mjinga yuko tayari kujifunza na kubadilika ila utakuwa sahihi ukichukia iwapo utaitwa mpumbavu maana mpumbavu yeye hayuko tayari kukubali kuwa hajui jambo flani, hata akielimishwa yeye huendelea kushupaa na kukakamaa maana akili yake haina uwezo wa kuruhusu maarifa mapya
Jana nimeona baadhi ya wanaharakati wa upinzani nchini na wanasiasa wachanga wakijaribu kupotosha kuhusu fomu aliyopewa Rais Magufuli kuhusu kugombea nafasi ya uongozi ktk vyombo vya dola.
Kwahiyo naomba tusaidiane kuhusu hili la uteuzi wa wagombea uongozi ktk vyombo vya dola ili mwishoni uweze kujifunza kitu kama uko tayari au uendelee kushupaa kama ndiyo tabia yako ya kushupaa.
CCM inaongozwa na kushughulikia masuala yote ya kiuongozi na kiutawala kwa mujibu wa ZANA zifuatazo,
i) Katiba ya CCM.
.
ii) Kanuni ya Uchaguzi ya CCM
.
iii) Kanuni ya Uongozi na Maadili ya CCM.
.
iv) Kanuni ya uteuzi wa wagombea wa uongozi ktk vyombo vya dola.
.
v) Kanuni ya wabunge na wawakilishi wa CCM.
.
vi) Kanuni za fedha na mali za chama na jumuiya zake
.
vii) Pamoja na sera za CCM (2010-2020)
.
viii) Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020 .
Naomba kwa leo nizungumzie zana namba (iv), kuna aina mbalimbali za uchaguzi na uteuzi unaofanyika ndani ya chama cha mapinduzi, lakini pia kuna uteuzi na uchaguzi unaofanyika kwa ajili ya kutimiza malengo mbalimbali ndani ya chama na nje ya chama.
Kuna uchaguzi unaofanyika ndani ya chama kwa ajili ya kupata viongozi wtakaohudumu ndani ya chama, mfano uchaguzi wa mwenyekiti wa wazazi, uvccm au mwenyekiti wa CCM Taifa, mwenyekiti wa CCM wilaya, mkoa au katibu wa CCM kata, tawi nk. Hao ni viongozi wanaochaguliwa kwa ajili ya kufanya kazi ya uongozi ndani ya chama.
Lakini pia kuna viongozi wanaoteuliwa ndani ya chama kwa ajili ya kufanya kazi ndani ya chama, mfano mzuri ni makatibu wa chama mkoa na wilaya, kuna wakurugenzi ndani ya chama, kuna nafasi nyingi ndani ya chama ambazo wanachama huteuliwa kikatiba kwa ajili ya kufanya kazi ndani ya chama mfano Katibu wa mahusiano ya kimataifa, Katibu wa itikadi na Uenezi, mkuu wa kitengo cha sheria, makatibu wa jumuiya za chama kama uvccm, wazazi nk
Baada ya kuangazia uchaguzi na uteuzi wa wanachama kuwa viongozi ndani ya chama, sasa turejee kwenye hoja kuu inayozungumzia uteuzi wa wagombea uongozi ktk vyombo vya dola. Huu ni uteuzi unaofanyika au uchaguzi unaofanyika ndani ya chama ambapo wanachaguliwa au kuteuliwa ndani ya chama huenda kufanya kazi serikalini (katika vyombo mbalimbali vya serikali au vyombo vya dola)
Mfano mwanachama anapochaguliwa ili akagombee udiwani, huyo anapelekwa ili akafanye kazi nje ya chama yaani serikalini, mwanachama anapoteuliwa au kuchaguliwa ili akafanye kazi bungeni huyo anakuwa ameteuliwa au kuchaguliwa ndani ya chama ila kazi anayoenda kuifanya iko nje ya chama, anaenda kufanya kazi ktk vyombo vya dola serikalini.
Kama hujui maana ya vyombo vya dola basi ni vyema uulize, maana inaonekana baadhi wanadhani vyombo vya dola ni jeshi la polisi, jeshi la ulinzi au usalama wa taifa pekee. Tambua kuwa vyombo vya dola ni dhana pana sana, hata bunge ni chombo cha dola, mahakama ni chombo cha dola na mamlaka nyingine za serikali zinazoisadia serikali kujiendesha ni vyombo vya dola, hata TAKUKURU ni chombo cha dola kinachoshughulika na rushwa nk
Hivyo basi, wagombea wa CCM ndani ya chama kama watia nia ktk udiwani, ubunge na urais wanaomba nafasi ili wakafanye kazi ktk vyombo vya dola, na kanuni inayotumika ndani ya CCM ni hiyo kanuni ya uteuzi wa wagombea uongozi ktk vyombo vya dola. Kwahiyo hata fomu ikiandikwa fomu ya uteuzi wa wagombea uongozi ktk vyombo vya dola na kutaja nafasi inayogombewa ktk hivyo vyombo vya dola, bado hakuna kinachopungua na hakuna kilichokiukwa kikanuni maana hapo inakua kwamba IWAPO A ni sawa na B, hivyo B pia ni sawa na A, ni suala la uelewa tu.
Kwahiyo kama kuna watu walikuwa wanapotosha kwa kutoelewa nadhani mtakuwa mmejifunza na kuelewa, na pia iwapo kuna watu wanapotosha kwa makusudi nadhani ni vyema kuacha upotoshaji huo maana kanuni hii imekuwepo tangu enzi na huwa inatumika ktk kila uchaguzi au uteuzi ndani ya chama kama anayechaguliwa au kuteuliwa anaenda kufanya kazi serikalini (Katika vyombo mbalimbali vya serikali).