PostGE2025 Uteuzi wa Wagombea CCM umeacha vinyongo, ipo siku wanaoumia watachoka kufunika kombe

PostGE2025 Uteuzi wa Wagombea CCM umeacha vinyongo, ipo siku wanaoumia watachoka kufunika kombe

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Nanunda

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
9
Reaction score
5
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 umepita, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilikamilisha kazi yake kwa kutangaza washindi wa Ubunge, Udiwani na Urais.

Upande wa maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya, Chama cha CCM Mkoa kimeshinda kwa kura katika maeneo mengi lakini bado kumekuwa na mijadala kuhusu makundi yaliyotokana na kupishana kwa Wanachama kabla ya uchaguzi, ambapo athari zake inawezekana zikaonekana baadaye.

Baadhi ya Kata za Mbeya kulikuwa na misuguano ya wazi iliyosababishwa na kile kilichoonekana kudaiwa kukosekana kwa “haki” wakati wa hatua za uteuzi wa Wagombea ndani ya chama.

Kulikuwa na Wanachama waliokuwa na matarajio ya majina fulani kupitishwa, yalipokatwa, hali ya sintofahamu ilitanda.

Moja ya tukio lililoonesha watu wana kinyongo au kutokubaliana na maamuzi ya chama ni maandamano yaliyotokea Kyela, ambapo baadhi ya Wanachama wa CCM walionyesha kutoridhishwa na maamuzi ya ndani ya chama, wakaamua kuandamana hadi Ofisi za CCM Mkoa wakipinga majina mapya ya Wagombea walioteuliwa.
52201.jpg


View: https://www.youtube.com/watch?reload=9&v=tnKkTgsDtwU
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Daud Yassin, Kupitia kikao maalum ilipotangaza uteuzi wa majina ya wagombea nafasi ya Udiwani katika kata 106 za Mkoa wa Iringa kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025.
Video: Focus TV Tanzania


Kata za Nsalaga, Mwakibete na nyingine za Jiji la Mbeya kulikuwa na makundi au mgawanyiko wa Wanachama kutokana na kutobaliana kwenye hoja kadhaa hasa ikiwemo kuhusu majina ya wanaostahili kuwa wagombea.

Wanachama walionesha wazi kupinga, wakiamini demokrasia haikufanya kazi inavyotakiwa, wakiamini majina yaliyopitishwa hayakuwa yale pendwa kwa Wananchi au wanachama kwa jumla.

Pamoja na hivyo ghafla wale waliokuwa wanapinga wakaamua kuwa kimya na wengine kutangaza kuwa wanavunja makundi na kuwaunga mkono waliopitishwa.

Swali la kujiuliza ni kuwa je, kinyongo chao ni kweli kimeisha au bado wamekihifadhi kwa matumizi ya baadaye?

Hii hali inatakiwa kuwa challenge kwa CCM kuhusu utaratibu wao wa kufanya uteuzi, kwani malalamiko mengi ya chinichini ni kuwa wanaamini ngazi za juu za chama zinawateulia watu ambao siyo chaguo lao.

Baadhi ya Viongozi wa CCM walioshinda kwenye nafasi ya Ubunge na Udiwani wameeleza changamoto walizokumbana nazo kwenye uungwaji wa mkono na Wagombea wenzao waliokatwa.
Screenshot 2025-12-19 004707.jpg
Aidha, wamesema wameanza kuchukua hatua za kuunganisha Wanachama na Watafanya mikutano ya shukrani, ziara za kuwatuliza waliokuwa na hasira, na kuhimiza umoja wa ndani ya chama.

Kauli zao nyingi zimejikita kwenye kuanza ukurasa mpya wa kufanya kazi na wananchi bila kutazama makundi yaliyowahi kutokea.

Upande wao Madiwani wa Kata ya Mwakibete na Nsalaga walinukuliwa wakisema hali ya uugwaji mkono ndani ya chama wakati wa kampeni iliimarika baada ya kupishana katika mchakato na hatimaye wakaungwa mkono na wenzao.

Wapo viongozi au wanachama ambao hawakutaka kuweka wazi utambulisho wao hadharani lakini wanakiri kuwa kulikuwa na msigano mkubwa wa ndani kwa ndani, na kueleza kuwa wametumia ule utamaduni wa CCM wa kufunika kombe tu lakini ndani ya mioyo yao wanaumia.

Huku kwa nje wanaonesha kama kila kitu kipo sawa lakini kiuhalisia hawajakubali hoja nyingi na maamuzi mengi ambayo Yanaon ekana kufanywa na Viongozi wa juu, hivyo ili isionekane wanapinga chama wale waliokandamizwa wameamua kunyamaza tuna kuonekana wanaunga mkono chama lakini kiuhalisia ndani ya moyo hali haipo hivyo.

Wananchi wanataka maendeleo
Mtazamo wa Wananchi, kilio kikubwa sasa ni kuona Viongozi waliopatikana kupitia uchaguzi wakifanya kazi inayotakiwa kwa maana ya kutimiza wajibu wao ikiwemo kutatua na kusaidia kero za Wananchi wao.

Uchaguzi wa ndani ya CCM kwa ngazi ya Jimbo la Mbeya Mjini nao ulikuwa na fitina za hapa na pale kiasi kwamba yule ambaye jina lake lilipitishwa kuwa Mgombea Ubunge, Patrick Mwalunenge alisusiwa na baadhi ya Wanachama wenzake japo baadaye nao walionekana kujitokeza hadharani na kumuunga mkono.

Mauaji ya Mtoto wa Mtiania
Wakati mchakato wa uteuzi wa ndani ukiendelea, ni wakati huo iliripotiwa tukio la Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu Mzumbe, Shyrose Mabula Mahande (21) kutekwa na baadaye kuuawa.

Alitekwa na watu wasiojulikana, baadaye mwili wake ukapatikana ukiwa umechomwa moto na kutupwa katika vibanda vya biashara Nane Nane, Mbeya.

Marehemu Shyrose (21) ni mtoto wa Dkt. Mabula Michael Mahande ambaye alikuwa mtia nia ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Mbeya Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Japokuwa haijawekwa wazi kama utekaji huo ulihusisha masuala ya siasa lakini Dkt. Mabula alisema watekaji waliwasiliana naye na kumueleza wanakwenda na mtoto wake Mbeya, alipouliza tatizo akajibiwa kuna watamueleza... haijawekwa wazi hadi sasa na Jeshi la Polisi linasema linaendelea kuchunguza.

Nilipozungunguka kufanya utafiti wa kuzungumza na Wadau mbalimbali wa ndani ya CCM nimebaini kuwa wengi wao hawakuwa tayari kuzungumza, wanasema wanaunga mkono waliochaguliwa bila kueleza kama yale yaliyowafanya wanung’unike kuhusu uteuzi wa ndani ya chama wameyaacha pia au wameamua kuyapotezea? Hawajibu

Nadhani hii ni nafasi nzuri kwa CCM kujitafakari au kutafakari mchakato wa uteuzi kwa kuwa kama demokrasia inaonekana kutopewa nafasi, inamaanisha ipo siku upepo utabadilika na wale wenye vinyongo na madukuduku hawatakuwa tayari kuendelea kukaa kimya.
 
CCM hata wote muuane na kumalizana huko ni sawa tu. Mashetani wakubwa nyinyi! 🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 
Back
Top Bottom