Uteuzi Wa Viongozi Wazee

wsdau sasa tunageuza mada inakwenda ndivyo sivyo,hapa tunataka hawa wazee ambao wamelitumikia taifa hili kwa muda mrefu na kupata uzoefu wakutosha ni wakati wao sasa kuingia ktk sekta binafsi ilikutumia ujuzi na mtaji walionao ktk kukuza uchumi na sio kuzeekea kwenye madaraka ambayo wamekuwa nayo miakanenda rudi.Na sio kunisukuma mimi ambaye ninacheti tu bila ujuzi wala mtaji.hilisio suala la uccm wa nanihiiiii

Kuwa specific, ni nafasi gani unazoongele wewe hao wazee waziachie?
Kumbuka kuna nafasi ambazo huwachwa kwa mujibu wa sheria ambapo mtu akifikisha miaka 60 hustaafu kazi. Lakini kuna nafasi zingine haziko kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo tusiwe tunajadili hoja bila ya kuwa na lengo, unaposema vijana washike hizo nafasi unamaanisha ni vijana gani?
Je, ni nafasi gani hasa ambazo wewe unaziona kwamba zimekaliwa na wazee kinyume na sheria? Kama zipo zianike hapa.
 
Hii ya wazee kuendelea kupeana uzoefu wa kazi sasa inaendelea kupata kasi.Hata angalia wajumbe wa NEC ya sisiem ya jana

lowassa,makamba,chenge,mwambi,membe,kapuya,gachuma,kinana,mwanri,wassira,komba,sumaye,mahanga,kingunge,mwakyusa,makalla,msome,lukuvi,chiligati,wangwe.

Maanake hii uzoefu wataendelea kupata wenye uzoefu.Hapa hamna mwenye umri chini ya miaka 50
 
Hapa tanzania kuna kitu kinaitwa recyclining of ledership. naomba niwieni radhi kwani nitataja majina hapa.
Kwanza vikiria gavana wa BoT aliyestaafu yaani Rashid sasa ni CEO tanesco baada ya kujaribu Akiba Commercial bank na benki nyingine pia Voda; Mattaka David alikuwa CEO wa PPF akaachwa sasa ameibuliwa amekuwa recycled kuwa CEO wa kufufua ATCL iliyouawa na sisi wenyewe kwa upambuavu wetu kudhani Afrika Kusini ndiyo mkombozi wetu. Aliyekuwa amestaafu PSRC mzee Mbowe aliteuliwa eti kuongoza TTCL ambayo kwa ujinga wetu tena tuliikabidhi wazungu waiue kama ambavyo tulifanya kwa Tanesco. sasa kuja kwa Msekwa tena si jambo la kushangaza kwa sababu sisi ni watu wa kurecycle mambo. kama alikuwa mkubwa kule akazeeka anweza kuwa kijana sehemu nyingine. Haya yanatoke wakati wanafahamu fika wakati wao wanchukua nchi walikuwa vijana lakini sasa wanataka wafie ofisini. Tunasonga mbele kwenda wapi kama si kujongea kaburi na maangamizo?
 
wazee wengi kwenye chama, ndio inayoleta mawazo ya kizee kwenye serikali.
kwakuanzia tu ....huyo JK na karamagi sio vijana! kijana wa nchi gani ana mia 57?! give us a break! watanzania mlidanganywa kikwete kijana na nyie mkadanganyika. sishangai sana lakini kwa vile sisiem hiyo hiyo imemchagua khadija kopa kuwa miongoni mwa NEC kwa mchango gani atakaotoa!! tunaongozwa na chama ovyo kabisa!

tunataka reform ndani ya serikali. na hii inawezekana. imewezekana china itakuwa tanzania ambapo siasa huru ni pevu zaidi?

wafanyakazi wote wenye umri wa zaidi ya miaka 55 tunaomba wastaafishwe, ili nafasi ziwe wazi kwa vijana wanaomaliza masomo
 
Hii ndio sababu ya kutokuwa na jipya Tanzania, bado mambo ni yale yale ya mwaka 47! Uongozi unazunguka miongoni mwa wateule wachache miaka nenda miaka rudi.


yanahitajika mabadiliko makubwa ktk teuzi na kuwaandaa viongozi...
 
Back
Top Bottom