Moja ya stumbling block ya kiuchumi tuliyonayo katika nchi yetu ni makazi holela.
Wataalamu wanasema hatua ya kwanza ya maendeleo katika mji ni kupanga mji. Maana yake ni kuwa ukipanga mji unamrahisishia mwananchi kupata huduma kwa wepesi ukiongelea logistics lakini pia kwa gharama nafuu.
ukipanga mji gharama za maisha za mtu mmoja mmoja zinakuwa ndogo hivyo vipato vilevile wanavyopata vitamudu mahitaji mengi zaidi na hivyo kwanza wao kama wao wananchi watanunua zaidi na hiyo ni kutengeneza ajira zaidi na kodi zaidi.
ukipanga mji unairahishia serikali kutoa huduma kwa wananchi kwa gharama nafuu na kuiraisishia serikali kuwafikia wananchi ili kuwadai kutimiza wajibu wao.
haya ndiyo yanayopelekea wataalamu kusema hatua ya kwanza ya maendeleo katika mji ni kupanga mji.
mfano
makazi ambayo yamepangwa kuweka maji ni rahisi na serikali inaweka mabomba ya mtaa kila nyumba bomba lina pita mbele yake na wananchi wanavuta kidogo tu kwa gharama nafuu lakini makazi holela kwanza yamekaa mbali na kila mtu kivywake au yamebanana sana kiasi hakuna nafasi ya kupitisha mabomba ya maji kuwafikia wananchi kwa karibu. Mtu kuweka maji katika nyumba yake ni gharama kubwa kuvuta maji kutoka mbali. Umeme hivyohivyo watu wa makazi holela gharama kubwa.
Huduma za hpspitali kwenye makazi holela shida maana hakuna anayetathmini wingi wa watu kujua idadi hii kwa pamoja inahitaji huduma hii. Makazi holela mengi watu wamekaa mbalimbali kutokana na kukosa udhibiti na utaratibu wa ujenzi hivyo mkazi mapya mengi hayana huduma hizi.
usafiri wa umma ni shida, watu wanatumia usafiri wa pikipiki, mfano masikini huyu analipa 1500 kwenye pikipiki kufikia kituo cha daladala na 1500 nyingine kutoka kituo cha daladala kurudi nyumbani. familia ya watu 5, baba, mama na watoto 3 wakitoka na kurudi kwenye pikipiki wanatumia 15,000 kwa siku (330,000 kwa siku 22 kwa mwezi) lakini kama makazi yangekuwa yamepangwa na daladala hizi zinafika mahali wanapokaa gharama ya kufikia vituo vya daladala ni sifuri. kazi za wachumi katika nchi ni kuhakikisha wananchi hawa hawapotezi hiyo 330,000 kwa mwezi katika usafiri bali wapate usafiri kwa bei nafuu na fedha hii ikafanye shughuli nyingine za maendeleo katika maisha yao. Leo hii Mtu akienda kupanga maeneo ya karibu 330,00 yote inaishia kwenye kodi ya kulipa nyumba na akisema akanunue kiwanja cha bei nafuu ajenge akae kwake fedha hii inaishia kwenye usafiri.
rafiki yangu huyu anasema kutokana na makazi mapya watu kukaa mbalimbal anasema mbu ni tatizo kubwa maana wamezungukwa na vichaka. anasema anatumia gharama kubwa katika huduma za afya maana kila mwezi wako hospitali wakiugua malaria.
rafiki yangu huyu anasema gharama ya maji ni kubwa maana hakuna huduma ya maji bali maji wanauziwa kwa kusombewa kwenye magari.
Hivi ni nani wa kutizama matatizo haya katika nji yetu na kuibuka na mipango ya kuondoa matatizo haya?
Hakuna mwingine bali Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi.
Lakini Je wizara hii inaona jukumu lake? jukumu hili kuona lina umuhimu gani katika jamii na wafanye nini kusaidia jamii?
Jamaa wamesinzia hawafanyi lolote na wananchi wanahangaika! miji inazidi kukua kwa kasi ikizidi kuvugika, wao wako kwenye biashara eti ukachukue hati kuhalalisha makazi yako hayo holela ili ulipe kodi. Kwao jukumu lao wanaloliona ni kumfanya mwananchi alipe kodi na hawaoni wajibu wao kwa Mwananchi.
Leo hii mtu tuliyemkabidhi jukumu hili na likamshinda maana katibu mkuu wa wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi ndiye mtendaji mkuu katika wizara hiyo, eti tunamkabidhi jukumu la kutazama mambo yote ya kifedha na kiuchumi.
Nijambo linaloshangaza kuona bado katika nchi yetu tunaendesha kwa dhana, mtu mnamkabidhi kiwanda aendeshe anakifilisi lakini bado mnampeleka kuendesha jambo kubwa zaidi kwa kutazama ana vyeti gani?
Ki msingi utendaji na vyeti ni vitu viwili tofauti. Kuna watu wana vyeti vizuri sana ni maprofesa lakini hawawezi kufanya hata jambo dogo kabisa kwa mafanikio.
kwa wale watu walioko kwenye system wapimwe kwa kile walichokifanya na sio kutazama ni daktari wa nini au profesa wa nini.
na utendaji sio ngonjera za kwenye majukwaa maana wengine wanatumia vyombo vya habari kupiga kelele ndio waonekane watendaji bali tutazame tumemkabidhi jambo hili tukiwa hatua gani na baada ya mda katufikisha wapi?