Uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri

Uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri

Mie namshauri wala asihangaike kubadilisha baraza, yeye kama yuko Uswiss akae huko huko asirudi hadi October 2015, Sio siri Kikwete tumekuchoka, umetuharibia nchi na utaiacha nchi pabaya sana
 
Mie namshauri wala asihangaike kubadilisha baraza, yeye kama yuko Uswiss akae huko huko asirudi hadi October 2014, Sio siri Kikwete tumekuchoka, umetuharibia nchi na utaiacha nchi pabaya sana

Kwa mwaka huo labda atakua kazaliwa Yesu mwingine tuanze kuhesabu upya teh.
 
Huu uvonjwa wa kansa. Kinachoendelea ni kumfariji mgonjwa kwa tembe asipate mawazo ya kufa.
 
Tuliambiwa pia Mawaziri wamekatazwa kutoka nje ya Dar es Salaam until further notes. Sina hakika kama hizo further notes tayari au bado.
 
Kubadili baraza la mawaziri huku imebaki miezi tu baraza livunjwe sio sawa hata kidogo kwani kutaleta matumizi yasiyokuwa na tija, wapo mawaziri itabidi wahame nyumba na wengine watalazimika kuhamia mahotelini hasa wale wapya. wapo mawaziri huhama na madereva makatibu muhtasi na hata wapika chai hii italeta mlolongo mkubwa wa uhamisho.

Mfano umhamishe magufuli ujenzi umpeleke wizara ya afya atahitaji kujifunza upya mazingira ya kazi na itamchukua muda kuweza kuzikabili changamoto za kazi katika hiyo ofisi mpya. mpaka sasa mafaili aliyoyaacha prof.tibaijuka haieleweki nani anayashughulikia kwani alipugwa juu kwa juu na hatujaona makabidhiano yoyote na hatujui kama bado anasign hati za viwanja au la.

Pia kuwafukuza watu kwa kizingizio cha kuwajibika sio sahihi sana, utamuwajibishaje Muhongo kwa tatizo lilokuwepo kwa miaka zaidi ya ishirini wakati yeye kawepo pale miazi tu, hii inawezekana ikawa hila za wapiga dili kuwapambanisha mawaziri wageni ili hadi wanagutuka tayari dili linakuwa limeshapita.

Tusifanye maamuzi ya pilato kumhukumu mtu asiyekuwa na hatia kwa kufuata makelele ya watu, tukikubali kusikiliza makelele ya akina sendeka sugu lema kangi itafika sehemu hatutaelewa ni nini hasa tunataka kufanya.


Tanzania kama nchi tunapaswa kuwa na dira na tujue shabaha yetu inalenga wapi tusiwe watu wa matukio, mfano tulisema nchi yetu hadi kufikia 2015 30% ya watanzania wawe na umeme yeye hadi sasa kafikisha 37% hayo hatuyaoni tu kweli? kuna watu kwa miaka mitano ya kuwatumikia wananchi wametoa madawati ishirini na beseni moja la kunawia, Prof.Muhongo kakaa ofisini miaka miwili tu nguzo za umeme zimetapakaa kila kona.
 
Ndugu wana JF kuna tetesi kuwa Rais JMK atatangaza baraza jipya la Mawaziri. Toka Jana nasikia mawaziri wamekatazwa kutoka nje ya DSM. Ilikuwa ikifika leo saa 10:00 jioni JMK angekuwa ameshatangaza baraza lake jipya, lakini mpaka sasa kimya. Kama kuna mwenye taarifa zaidi atujuze.
 
Ndani ya CCM hakuna msafi hata aliyezaliwa leo siwanajiita ukoo wa panya hata mtoto ni mwizi!
 
Hahahaaa! Watu wanajua kucheza na akili za watu. Yaani kila siku zinaibuka taarifa za Baraza jipya la Mawaziri, lakini inakuwa kimya kabisa. Kusema kweli suala la Escrow limekuwa gumu kwa mkuu wa kaya kwa sababu kuwa 'wana kibao' wamo ndani ya mgawo wa pesa.
Ova
 
Akitangaza ni hasara tu kwa taifa,hao watakao temwa lazima walipwe kiinua mgongo na hao wapya pia lazima pia walipwe muda wao ukiisha,jamaa naona anatafuta kuwapoza wadanganyika
 
Kama baba riz atatangaza baraza lingine la mawazili na yeye atangaze kujiuzuru kwa sababu yeye ndokichocheo cha escrow,
 
Akitangaza ni hasara tu kwa taifa,hao watakao temwa lazima walipwe kiinua mgongo na hao wapya pia lazima pia walipwe muda wao ukiisha,jamaa naona anatafuta kuwapoza wadanganyika

Mizigo juu ya mizigo
 
Back
Top Bottom