Uteuzi vigogo sekta binafsi gumzo

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,795
21,392
Wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiwateua wakuu wa bodi za taasisi za umma, wanazuoni wamesema hatua ya kuhusisha watu kutoka sekta binafsi kuziongoza bodi hizo inatafsiri kwa vitendo dhamira yake ya kushirikiana na sekta hiyo.

Juzi, Rais Samia aliwateua wakuu wa bodi, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Filbert Mponzi, Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT).

Mwingine ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SSC Capital, Salum Hagan aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB).

Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni hao wameonyesha mashaka ya kuwepo kwa mgongano wa maslahi kwa wakuu wa bodi hizo ambao pia ni viongozi wa maamuzi katika kampuni binafsi.

Akizungumza na Mwananchi juzi, Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk Timoth Lyanga alisema uteuzi wa viongozi hao unalenga kuiunganisha sekta binafsi na Serikali na uzoefu wao utatimiza matarajio ya mamlaka za uteuzi na wananchi kwa ujumla, kwa kustawisha taasisi za umma.

Alipoulizwa iwapo kutakuwa na mgongano wa maslahi kama walivyoshuku wanazuoni wengine, Dk Lyanga alisema ni vigumu kutokea kwa kuwa watafanya kazi kwa taratibu na miongozo ya utumishi.

“Sawa yeye anaweza kuwa na maslahi na jambo fulani, lakini utaratibu wa kitaasisi una watu wanaohakikisha kila kitu kinafanyika kisheria,” alisema.

Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya wote, lengo ni kuijenga kila mtu kutoka eneo lolote apewe nafasi ya kufanya hivyo kwa maslahi ya umma. Mtazamo huo unaungwa mkono na Mhadhiri kutoka Chuo cha Mipango, Dk Domitilla Bashemera aliyesema uwezo wa Serikali pekee hautoshi kutimiza malengo yake, inahitaji changamoto mpya, ndiyo maana sekta binafsi ni muhimu kuhusishwa.

Alieleza sekta binafsi inakwenda kuziba mashimo ambayo Serikali pengine isingeyaona, akisisitiza kuwa: “Hii ina maana kubwa na inajenga ushirikiano katika majukumu ya kitaifa”.

Alisisitiza ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika ustawi wa taasisi za umma, utaongeza tija ya kuanzishwa kwa taasisi hizo na hatimaye kuimarisha uchumi wa nchi.

Akizungumzia hilo, Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Wilhelm Ngasamiaku alisema: “Walioteuliwa wote ni vijana na wamefanya vizuri katika taasisi binafsi wanazoziongoza, nadhani Rais Samia anataka kutumia uwezo wao wa uongozi kuimarisha taasisi za umma,” alisema.

Hagan wa SSC Capital, aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya CPB, alisema wakati wote sekta binafsi imekuwa ikiomba kushirikiana na Serikali katika maeneo mbalimbali.

Alieleza dhamira ya mkuu huyo wa nchi ni kubadili mitazamo na utamaduni wa utendaji wa mazoea, kwa kuihusisha sekta binafsi kuboresha.

“Tumesikia mara kadhaa Rais Samia akisisitiza juu ya kuifungua nchi na kushirikiana katika kazi, ukiwa na watu wenye mitazamo inayofanana huwezi kuendelea, hivyo sekta binafsi inaingia kubadili mazoea na kuboresha utendaji kazi,” alisema.

Kuhusu majukumu yake mapya kama mkuu wa bodi ya CPB, alisema kwa kushirikiana na wenzake, atahakikisha wanatafuta soko sahihi litakalosaidia kuinua sekta ya kilimo. “Tumeona Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na mipango yake mizuri, tutamuunga mkono ili kuleta mapinduzi na tija kwa wakulima,” alisema.

Naye Mchumi kutoka UDSM, Dk Jehovaness Aikaeli alisema uenyekiti au ujumbe wa bodi sio kazi ya muda wote, huwa ni shughuli inayofanywa na watu ambao wakati mwingine wana kazi nyingine.

Alisema ni kwa sahihi Rais Samia kuwateua wasaidie maeneo ambayo wana uzoefu na taaluma nayo.

Wahofia mgongano wa maslahi

Tofauti na hoja za wengine, Mhadhiri wa Uchumi wa Siasa, Profesa Joseph Mbwiliza kutoka Chuo Kikuu cha St Agustine tawi la Mbeya, alisema haoni sababu ya kuwahusisha viongozi kutoka sekta binafsi katika bodi za taasisi za umma, kwa kile alichokieleza kuwa kuna hatari ya mgongano wa maslahi.

“Ikitokea taasisi ya umma inagongana maslahi na taasisi yake binafsi, kutakuwa na hatari ya Serikali kupoteza kwa sababu haitakuwa tayari kuisababishia hasara kampuni inayomlisha siku zote,” alisema.

Alipendekeza wastaafu waliowahi kuzitumikia taasisi hizo za umma kwa mafanikio, ndio wapewe nafasi ya kusimamia bodi, akisisitiza hawapaswi kuwa watumishi katika kampuni nyingine zenye uwezekano wa kugongana kimaslahi.

“Ni kweli Tanzania yetu sote na tunahitaji ushiriki wa sekta zote katika kila jambo, lakini tuangalie tija na maslahi yake,” alisema.

Profesa Mbwiliza, ambaye pia ni Mkuu wa chuo hicho, alitaka kutengenezwe sera na miongozo itakayoeleza namna nzuri ya kupatikana kwa wakuu wa bodi za taasisi za umma.

Alikwenda mbali zaidi akieleza, kama wamekosekana wazoefu wa kisekta katika taasisi za umma zinazohitaji bodi, watumiwe hata dayaspora, kwani wapo wabobevu nje ya Tanzania.

Wakumbuka mfumo wa zamani

Mtaalamu wa Utafiti wa Uchumi, Profesa Haji Semboja alikosoa mfumo unaotumika kuwapata wakuu wa bodi na mamlaka nyingine, akisema wanapaswa kuomba na sio kuteuliwa.

Kitendo cha kuteuliwa, alisema kinawafanya wafanye kazi kwa sababu wamepewa nafasi hizo na sio kwa nia thabiti kama ambavyo wangeziomba.

“Nafasi zitangazwe, watu waombe, wapatikane wataalamu wenye ujuzi na sekta watakazoziongoza ndiyo wapewe, kinyume na hapo suala la maendeleo hatutalipata,” alisema.

Profesa Semboja, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alieleza kuwa mfumo wa kuteuana ulifanyika enzi za Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere kwa kuwa idadi ya wataalamu ilikuwa ndogo.

Alieleza kusikitishwa na utaratibu wa Tanzania katika karne hii, akisema wataalamu wenye ujuzi wa sekta husika wapo lukuki, kwa nini hawapewi nafasi ya kuomba ili watumikie kwa dhamira za maombi yao.

“Zile mbinu za kwamba fulani yupo kwenye mtandao kila siku hao hao, kunatufanya tubaki kuwa maskini ukilinganisha na nchi nyingine zenye rasilimali kama zetu,” alisema.

Alieleza maeneo ambayo Tanzania inakwama kwa maendeleo ni Serikali au siasa kuingilia moja kwa moja mfumo wa utawala wa uchumi.

Ili nchi iendelee, alibainisha inahitaji mfumo kamili na sera za kisasa, zilizoandaliwa kitaalamu, sheria zitakazozitafsiri sera hizo, muundo wa taasisi na kuwa na rasilimali watu wanaoendesha taasisi kisheria na wanaopatikana kisheria pia.

Alisema mfumo unatakiwa kueleza watu gani wawekwe kwenye eneo gani na hata upatikanaji wao unapaswa kuwa kwa mujibu wa sheria zilizoanzisha taasisi husika.

“Tunafahamu mamlaka za uteuzi zinafanya shughuli hiyo kisheria, maana hata Katiba inaipa wajibu huo, lakini umefika wakati tubadilishe hii mifumo ya kizamani,” alisisitiza.

MWANANCHI
 
Tunakoelekea nchi inahitaji maombi.
Kwa nini? Mbona mambo yanakwenda vizuri sana?

Rais anafanya vizuri tena kuwabadilisha nyie mlio na akili mgando kuwa sekta binafsi ni wizi.

Mnatakiwa kujua kuwa sektq binafsi ndo engine ya maendeleo kwa nchi yeyote na kikubwa zaidi kwa akili zenu wajamaaa mnahitaji watu wenye mindset za kuchakarika ili mfanye kazi na kudeliver vizuri
 
Anacofanya Mama ni nzuri sana, sio unateua maprofesa, madokta kutoka vyuo vikuu kuongoza bodi unakuta mtu hata hajawahi kumiliki duka.
 
Tanzania hakuna kabisa kitu kinaitwa CAREER DEVELOPMENT Wala CORPORATE LADDER.

Watu Ni wa KUOKOTA OKOTA tu from NO WHERE.

Mtoto wa FULANI

KADA WA CHAMA.

Aanmsifia Sana RAIS kwenye Media.

MSANII anafahamika.

Hizo TAASISI utafikiri zimeanza JANA.

Watumishi wamefanya kazi Kwa UAMINIFU Kwa Muda mrefu ,halafu anakuja KUOKOTWA mtu tu ndio anawekwa hapo.

Halafu tutarajie MAENDELEO.

Labda Kwa MIUJIZA
 
Gumzo lipi sasa
 
Huyu profesa ameongea jambo la msingi kabisa
Huyo Prof Semboja amekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya NMB Bank kwa miaka zaidi ya kumi na tano, More than 15 years

Ametoka NMB sasa anapiga kelele, Alishavuna mamilioni Prof Semboja NMB mpaka alipostaafu na nafasi kuchukuliwa na yule commission mstaafu wa TRA hapo NMB Bank

Akae kimya
 
Back
Top Bottom