Idd Ninga JF-Expert Member Joined Nov 18, 2012 Posts 5,539 Reaction score 4,854 Aug 8, 2018 #1 HATUNAE MAJUTO. 1.Kila nafsi duniani Taingia kaburini Sote yupo safarini Twapita kwenye dunia. 2.Imendikwa vitabuni Siyo tungo za kubuni Kifo kipo karibuni Hakuna wakubakia. 3.Ila Mumba wa mbinguni Kwake twende kutubuni Toba iwe ndo dhumuni Tena tufanye kwa nia. 4.Ulazwe pema peponi Twahisi tupo ndotoni Siku yetu hatuoni Nani atatangulia. 5.Majonzi pia huzuni Na machozi mashavuni Umefika hatimani Kuwayo kwenye dunia. 6.Kuonana tena lini Tutakutia machoni Tulikupenda fwadini Ila umetangulia. 7.Twaisoma talqini Na dua nyingi za dini Mauti hayana kani Sote tutayapitia. 8.Hata uwe himayani Mbali kama Marikani Kifo hakina utani Huko kitakuchukua. 8.Ni huzuni kwenye fani Mashabiki mtaani Wakwombea Athumani Majuto me tangulia. 9.Uhai huna thamani Tujiandae jamani Kifo kwetu darasani Mengi pakujifunzia. 10.Hijalishi ni angani Nchi kavu na porini Mlimani baharini Kifo kitatufikia. 11.Na pesa kiasi gani Uwe nacho mfukoni Mbele yake masikini Kifo hatokuelewa. 12.Burudani jukwaani Hata kule runingani Ulikuwa ni makini Sana ki kuitendea. 13.Ilikuwa burudani Tamu iso na kifani Ni kweli siyo utani Nyota imeshapotea. 14.Wa kuliziba ni Nani Pengo lako pa nchini Sote tuna kaa chini Huku twakombea Dua. 15.Futuhi sa hatarini Kufutika runingani Iwapi yako thamani Serikali kulindia. 16.Wala hukwenda chuoni Ni uwezo wa manani Na ubunifu kichwani Mola alokujalia. 17.Wa kukuenzi ndi Nani Mbona bado tumuoni Ulipokua kazini Mzaha hukufanyia. 18.Hata filamu za dini Tuliona majumbani Leo taicheza Nani Nawe umeshapotea. 19.Nyingi Dua kwa manani Uwe wanja wa peponi Chumba chako mwanandani Rabi apate jalia. 20.Amini rabi amini Taqabal rahmani Waja wako waumini Ipokee yetu dua. SHAIRI -HATUNAE MAJUTO. MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha. +255624010160. iddyallyninga@gmail.com
HATUNAE MAJUTO. 1.Kila nafsi duniani Taingia kaburini Sote yupo safarini Twapita kwenye dunia. 2.Imendikwa vitabuni Siyo tungo za kubuni Kifo kipo karibuni Hakuna wakubakia. 3.Ila Mumba wa mbinguni Kwake twende kutubuni Toba iwe ndo dhumuni Tena tufanye kwa nia. 4.Ulazwe pema peponi Twahisi tupo ndotoni Siku yetu hatuoni Nani atatangulia. 5.Majonzi pia huzuni Na machozi mashavuni Umefika hatimani Kuwayo kwenye dunia. 6.Kuonana tena lini Tutakutia machoni Tulikupenda fwadini Ila umetangulia. 7.Twaisoma talqini Na dua nyingi za dini Mauti hayana kani Sote tutayapitia. 8.Hata uwe himayani Mbali kama Marikani Kifo hakina utani Huko kitakuchukua. 8.Ni huzuni kwenye fani Mashabiki mtaani Wakwombea Athumani Majuto me tangulia. 9.Uhai huna thamani Tujiandae jamani Kifo kwetu darasani Mengi pakujifunzia. 10.Hijalishi ni angani Nchi kavu na porini Mlimani baharini Kifo kitatufikia. 11.Na pesa kiasi gani Uwe nacho mfukoni Mbele yake masikini Kifo hatokuelewa. 12.Burudani jukwaani Hata kule runingani Ulikuwa ni makini Sana ki kuitendea. 13.Ilikuwa burudani Tamu iso na kifani Ni kweli siyo utani Nyota imeshapotea. 14.Wa kuliziba ni Nani Pengo lako pa nchini Sote tuna kaa chini Huku twakombea Dua. 15.Futuhi sa hatarini Kufutika runingani Iwapi yako thamani Serikali kulindia. 16.Wala hukwenda chuoni Ni uwezo wa manani Na ubunifu kichwani Mola alokujalia. 17.Wa kukuenzi ndi Nani Mbona bado tumuoni Ulipokua kazini Mzaha hukufanyia. 18.Hata filamu za dini Tuliona majumbani Leo taicheza Nani Nawe umeshapotea. 19.Nyingi Dua kwa manani Uwe wanja wa peponi Chumba chako mwanandani Rabi apate jalia. 20.Amini rabi amini Taqabal rahmani Waja wako waumini Ipokee yetu dua. SHAIRI -HATUNAE MAJUTO. MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha. +255624010160. iddyallyninga@gmail.com
Basi Nenda JF-Expert Member Joined Jul 29, 2017 Posts 20,796 Reaction score 48,044 Aug 8, 2018 #2 Steve nakuona umeandaa kabisa ka speech kako
A Arams Senior Member Joined Jun 14, 2015 Posts 133 Reaction score 195 Aug 8, 2018 #3 Kufa kufaana, Hongera sana kwa utunzi
Uduvi JF-Expert Member Joined Sep 3, 2012 Posts 738 Reaction score 521 Aug 8, 2018 #4 Steve nyerere Mzee wa kuiba rambirambi namuona ananyapia nyapia
deogratias hezekiel Member Joined Jan 21, 2018 Posts 14 Reaction score 6 Aug 8, 2018 #5 Imependeza sana kwa wosia km huu
Man Ching Member Joined Jul 17, 2018 Posts 62 Reaction score 57 Aug 8, 2018 #6 Aya sasa wazee wakupiga niwakati wakuongeza Gari na Nyumba