Sera nzuri. Tatizo hadi sasa hakuna sheria ambayo inaendana na sera hiyo. Kuna Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto lakini hakuna Wizara ambayo inahusuka na Wazee. Vilitolewa vitambulisho vya wazee ili pindi wauguapo wapate matibabu bila bughudha. Vitambulisho hivi hakuna mahali vinatambulika. Nenda Hospitalini kwenye dirisha la Wazee. Ndani ya chumba kuna meza tu, daktari wa Wazee hayupo! Nenda vituo vya Polisi. Kuna dawati la Wanawake na Watoto lakini hakuna dawati la Wazee. Sera ya Wazee, ile ya Serikali, pasipo kuwa na nguvu za kisheria inapwaya sana.