Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, amani iwe kwenu.
Bila shaka Uchaguzi umemalizika. Naamini pia Rais amemaliza kupanga safu yake ya Uongozi ngazi ya serikali. Naamini pia atakabidhiwa chama Julai 23 ili aweze kukisimamia chama kiweze kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015-2020.
Uzi huu ni mahsusi kwa ajili ya kuweka utekelezaji wa kile alichoahidi Rais wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Tutaangaza pia na Ilani ya CCM ili ifikapo mwaka 2020, tuweze kumpima Rais wetu kwa mizania iliyo sawa.
1. AHADI; - Elimu Bure hadi Kidato cha Nne
UTEKELEZAJI; - Muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwake, Rais alifuta ada na michango yote ya shule za
Msingi na Sekondari na kwa sasa watoto wetu wanasoma Bure.
2. AHADI; - Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Standard Gauge
UTEKELEZAJI; - Shilingi Trilioni Moja imetengwa kwa mwaka wa fedha 2016/17 kama kianzio
3. AHADI; - Uanzishwaji wa Mahakama ya Majizi na Mafisadi
UTEKELEZAJI. - Jumla ya Shilingi Bilioni 2.5 zimetengwa kwa ajili ya Mahakama hiyo. Majengo
yamepatikana, wafanyakazi wa Mahakama hiyo wamepatikana
4. AHADI; - Milioni 50 kwa Kila Kijiji
UTEKELEZAJI; - Fedha hizo zimetengwa kwenye Bajeti ya 2016/17. Vijana wanahamasishwa kuunda
Vikundi ili wapatiwe mafunzo ya Ujasiriamali ili wanufaike na fedha hizo
5. AHADI; - Kuondoa kodi za Hovyo zinazowakandamiza wanyonge
UTEKELEZAJI; - Kwenye Bajeti ya 2016/17, kodi za hovyo zimefyekwa hasa kwenye mazao ya Biashara
6. AHADI; - Umeme wa kutosha na wa Bei nafuu
UTEKELEZAJI. - Gharama za Ankara za umeme zimepunguzwa. Pia Service Charge imeondolewa
7. Ahadi: - Kuhakikisha wanafunzi hawakai chini....
Utekelezaji: - Madawati ya kutosha yametengenezwa na ahadi hii imetekelezwa kwa zaisi ya Asilimia 90
Wadau. Huu ni mwanzo tu na nitaendelea kuweka updates kwa kila ahadi itakavyotekelezwa. Kwa yale ambayo sijayaainisha humu, nawaomba wadau mnikumbushe nani nita update mara kwa mara.