Goodrich
JF-Expert Member
- Jan 29, 2012
- 2,091
- 1,179
Kuna matangazo ya kipindi kitakachorushwa na ITV kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM.
Nimeamini kabisa ya kuwa hakuna cha kujivunia ambacho CCM na serikali yake imefanya tangu kuingia madarakani.
Maana katika matangazo hayo tu, wanaongelea miradi ya TASAF, mapambano ya Rushwa, na mengineyo ambayo ni ya utendaji wa kawaida kabisa wa kila siku wa serikali.
Ingetarajiwa waongelee mambo kama jinsi gani wameboresha sekta ya umeme, mtandao wa barabara, jinsi gani wameinua elimu ya msingi, sekondari nk, sekta ya afya, ajira, upitiaji mikataba ya madini na mambo kama hayo yenye muelekeo wa ki maendeleo.
Au basi kama ni ilani as it is, waingolee kama ilivyowekwa wazi na JK katika ahadi zake ikiwamo :
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam hadi mikoa ya Kanda ya Ziwa - Nzega, Tabora.
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini.
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria Igunga.
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Shinyanga.
5. Kumaliza migogoro ya ardhi nchini Dodoma.
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini.
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma.
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi Kagera.
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi Kagera.
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini.
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini.
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda Kagera.
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme Kagera.
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu Kagera.
15. Hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua albino Mbeya.
16. Kununua meli kubwa kuliko mv Bukoba Kagera.
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali.
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika Mwanza.
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalumu chenye vifaa kupambana na wahalifu Mwanza.
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani Geita.
21. Kulinda Muungano kwa nguvu zote Pemba.
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa Morogoro.
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini.
24. Kujenga bandari Kasanga Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo Songea.
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira Mbeya.
27. Kuzuia hatari ya Kisiwa cha Pangani kuzama Tanga.
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini Iringa.
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same hadi Kisiwani Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam-Same mkoani Kilimanjaro.
30. Kumaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Same - Same mjini.
31. Kuboresha barabara za Igunga-Tabora.
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu mkubwa wa walimu - Kisesa Magu.
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya mjini.
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) - Hydom Manyara.
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa Musoma.
36. Kulinda haki za walemavu Makete.
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami, urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini.
38. Kujenga barabara Musoma-Mto wa Mbu Arusha Arusha.
39. Kuanzisha Jimbo la Ulyankulu- Shinyanga mjini.
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma-Kaliua, Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha-Moshi - Arusha mjini.
42. Kuboresha barabara ya Hande
ni, Kondoa hadi Singida Dodoma.
43. Kuwafidia wanakijiji ngombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 Longido.
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji Shinyanga.
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha Arusha mjini.
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma.
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido Longido.
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti Ngorongoro.
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara.
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini.
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima mwaka 2010-2015 - Babati vijijini.
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha Iringa.
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika Iringa.
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania Iringa. 55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi Ifunda.
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, Mkoa wa Mara.
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa.
58. Ahadi kuisaidia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii Kibandamaiti, Mjini Zanzibar.
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada Kibandamaiti.
61. Serikali kujenga upya Bandari ya Mbamba Bay Ruvuma.
62. Ununuzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 Mbamba Bay, Ruvuma.
63. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) Ruvuma.
64. Mtwara kuwa mji wa viwanda Mtwara.
65.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu Kibaha.
66.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa Kibaha.
67. Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda Kibaha.
Tofauti na hapo wafanye kazi kwanza !