Utekaji wa mtoto na huduma za kipolisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utekaji wa mtoto na huduma za kipolisi

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mtazamaji, May 15, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nimesikia summary ya mageziti kisa kimoja kinachofanya nijiulize umakini,uharaka, uwajibikaji wa utendaji wa polisi na watu wanaotakiwa kulinda usalama wa raia

  In sumary ya kisa ni hivi mtoto alitekwa moshi na kupelekwa uganda. wazazi wakatakiwa watoe pesa kama kikombozi.

  Kwa mujibu wa wazazi walikwenda polisi. Majibu ya kituo cha kwanza ilikuwa hiyo issue ni kubwa mno inahitaji watu wa makao makuu ????

  Wazazi wakaenda kwa DC jibu walilopewa ni kuwa hayo ni masuala ya kiusalama/kipolisi. ???????????

  wazazi wakaamua kuorganise resorucez zao wenyewe na kuchangiwa na ndugu na jamaa fwedha . wakaenda mpaka Uganda wakadeposit hela kwenye account kama walivyoagizwa na mtekaji waliyekuwa wanawasiliana naye mara kwa mara kwenye simu.

  Baaada ya muda wakaelekezwa waende kituo cha basi fulani na kondakata akawakabidhi mtoto wao.

  NB: Kondakta alisema kapewa huyo mtoto na mtu aliyemwambia kuwa atapokelewa na wazazi wake. so kondakta hana kosa. Na zaidi huyo mtoto kasema kawaacha wenzake watatu

  kwa mujibu wa gazeti majibu ya polisi wa tanzania wamesema wazazi wa mtoto walikuwa wana haraka sana????

  DUKU DUKU NA MAONI YANGU

  Je utendaji wa polisi hapa ndio huu wakutoa majibu mepesi mepesi kwa issue nzito? Yaani mtu una tatuzo kubwa badala kituo cha kwanza unachoripoti kichukue issue unaambiwa nenda kule au nenda kule. Kwa nn hicho kituo ulicholiripoti kisiwajibike kuripoti hiyo issue urgent inapotakiwa?

  Je kuna umuhimu wa kuwa na Ushirikiano wa Afrika mashariki ikiwa issue ndogo kama hii polisi wa TZ wameshindwa kuorganise resources zao na za waganda kuwakamata wahusika?

  Je Jeshi la Polisi limepewa haki ya kuwa uwezo wa kufanyia utafiti na uchunguzi kwenye makampuni yetu ya simu( Zain , Celtel, Tigo, TTCL). Mfano kujua mtu mwenye IMEI no fulani alibadilisha chip ya number 07xxxxx tarehe fulani na alipiga simu akiwa maeneo fulani kuwasiliana na jamaa XYZ. Nadahni hili ni rahisi sana na linaweza kukatama wahalifu kwa kasi kirahisi kwa kasi hata ambayo hata Jeshi litashangaa.

   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  polisi wa kwetu njaa tu..................kufanya kazi ambayo hatapata rushwa yoyote ndani yake haoni kama ina maana kwake. Polisi kwetu wamekaa ki maslahi zaidi. aibu
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani hapo ndo utajua police wetu wanafaa au awafai yani awataki kuumiza vichwa kabisa aswa kama ishu yenyewe aina rushwa watakupa kila sababu wanazozijua mwisho wanaweza kukuambia hilo si swala la kipolisi linaitaji makomandoo na makomandoo wote wamekewenda mazoezini hivyo subirini warudi.
  ebufikiria ishu kama hiyo watekaji wanakula pesa kilaini usalama wa taifa wako wapi? yani inauma kweli na watekaji wakishajua udhaifu wa vyombo vya usalama vitashamiri
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yaani hata hayo majibu aliyotoa DC kumwambia mzazi wa mtoto hiyo ni issue ya kiusalama. kwani katika baadhi ya majukumu na wajibu wa DC hakuna issue ya ulinzi na usalama. Nadhani angekuwa mtoto wa kigogo fulani au mtu mwenye jina response ingekuwa tofauti.
   
 5. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  pamoja na mambo mengine,sidhani km issue hiyo iliwashinda polisi,kuna utaratibu maalum wa kufuata kwani tayari mtoto huyo alikuwa nchi nyingine. Tukio km hili mpokea taarifa akipata taarifa km hiyo ni lzm OCD ajulishwe na baadae PCO n RPC wanapewa taarifa ambapo kati ya hao yaani RCO au RPC anamjulisha DCI ambako ndiko kuna kitengo cha Polisi wa kimataifa (INTERPOL) ambao huwasiliana na wenzao wa nchi husika na kwa kutumia teknologia ya simu baada ya kuwapatia namba ya simu inayotumika ktk mawasiliano huweza kuwapata kiurahisi wahalifu na hata hapa kwetu mfumo huu umekuwa ukitumiwa sana na kukamata wahusika wa matukio mengi ya uhalifu hasa baada ya polisi kupewa uwezo wa mamlaka ya ku access au kuingilia mawasiliano ya mtu wanayemtilia shaka. nadhani ikwa maoni yangu,wazazi wa mwathirika walikuwa na haraka ya kukomboa mtoto wao kwani damu ni nzito kuliko maji. kitu kingine ni kukosekana kwa huduma nzuri kwa mteja na ndiko kunapelekea pia wadau wengi kutokuwa na imani na jeshi letu la polisi. Naomba kuwasilisha hoja.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani na wewe
  Ukweli Polisi issue iliwashinda sababu aliyefanikisha kukombolewa mtoto ni mzazi mwenyewe. Hata kama kungekuwa kuna mlolongo wa watu 10 wa kujulishwa hiyo issue swali la kujiuliza inachukua siku ngapi kutoka kituoni hadi kwa OCD na inachukua masaa mangapi ofisi ya OCD kumjulisha PCO.

  KWa wenzetu naamini kuna sheria kuwa a issue fulani urgent inabidi iwe imemfikia bosi fulani labda baada ya masaaa matatu. Kusema mzazi wa mtoto alikuwa na haraka ni kukosea kabisa. Ukweli ni kuwa Polisi wako slow. Otheriwse useme issue ya utekaji kipolisi haimo katika mambo Critical ???.
   
 7. K

  Kilian Senior Member

  #7
  May 15, 2010
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndiyo serikali yenu yenye sera za maisha bora kwa kila mtanzania!!!!!!! Tuendelee tu kuichagua!!!!!!. DC ni nani kama sio serikali? nani bosi wa usalama wa taifa kama sio serikali? Hivi tunaogopa nini kujaribu serikali nyingine mwaka huu? kwanini hatuko tayari kujaribu kitu kipya hata kama hatujui watafanya nini?

  Watanzania TUMENYANYSWA VYAKUTOSHA, TUMEONEWA VYAKUTOSHA NA TUMEDHARAULIWA VYAKUTOSHA NA WALE TULIODHANI NI WATETEZI WETU. TUAMKENI SASA TUJARIBU KITU KIPYA, SERIKALI YA CHAMA KINGINE.


  Mungu aturehemu.
   
 8. M

  Mkono JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo ndiyo Tanzania zaidi ya uijuavyo! Said Mwema anavyo penda ujiko na wenzake kwa hili wako kimya kama vile hakuna kilichotokea
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Uharamia wa kuteka watoto waibuka


  Wazazi wadaiwa kulipa fedha nyingi kuwakomboa

  Utapeli wa kutisha umeingia mkoani Kilimanjaro, ambapo mtu mmoja (jina tunalihifadhi) ameiba mtoto wa kiume anayesoma darasa la pili, mwenye umri wa miaka minane na kumtoroshea jijini Kampala, Uganda.
  Mwanafunzi huyo jina linahifadhiwa alikuwa anasoma katika shule ya msingi Korongoni Manispaa ya Moshi.
  Baada ya kumtoroshea Uganda, mtu huyo aliwadai wazazi wa mtoto huyo dola za Marekani 1,000 ili wamrejeshe mtoto huyo.
  Wakizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa kuelezea utapeli huo na namna walivyompata mtoto wao, baba wa mtoto huyo, mkazi wa Oysterbay na mfanyabiashara wa soko la Mbuyuni mjini hapa, alisema kuwa mwanaye alipotea tangu Aprili 18, mwaka huu.
  Mzazi huyo alisema siku ya tukio walirejea nyumbani kutoka shambani eneo la Punguani wilayani Moshi Vijijini majira ya saa moja jioni lakini hawakumkuta mtoto wao hivyo wakaanza kumtafuta.
  Alisema baada ya kumkosa kwa ndugu, jamaa na marafiki, walikwenda kituo kikuu cha Polisi mjini hapa na kutoa taarifa.
  Baada ya kutoa taarifa, waliambiwa kuwa zikipita saa 24 bila mtoto huyo kuonekana polisi wangeaza uchunguzi. Mzazi huyo alisema baada ya kupita siku 17, polisi waliwajulisha kuwa kuna mtoto amepatikana na kwamba alikuwa kituo cha polisi cha Majengo mjini hapa.
  Kwa mujibu wa baba mzazi huyo, walimuona mtoto husika, lakini hakuwa wa kwao.
  Alisema baada ya wiki moja kupita tangu waelezwe habari za mtoto aliyekuwa Majengo, wakala wa basi la Kampala Coach namba UAL 248H, alidai kuwa alipigiwa simu na mtu mmoja kutoka Uganda ambaye alimwelekeza awasiliane nao ili awape mawasiliano kwa lengo la kuwasiliana na mtu aliyemchukua mtoto wao.
  Alisema ndugu waliwasiliana na mtu huyo kwa namba 01405915501 ambaye alidai kuwa yuko Uganda na kwamba anahitaji kiasi hicho cha fedha ndipo amuachie mtoto huyo na akawapa muda wa siku tatu kuwasilisha fedha hizo vinginevyo atamuuza mtoto huyo.
  Mzazi huyo alisema kuwa alirudi polisi na kuwaomba msaada, lakini walimwambia kuwa hawawezi kumsadia kwani hawana uwezo wa kusafirisha polisi hadi nje ya nchi na kwamba kibali cha kusafirisha polisi husika ni lazima kitoka makao mkuu Dar es Salaam.
  Alisema majibu hayo hayakumridhisha na kuamua kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Musa Samizi, ambaye aliwajibu kuwa yeye ni mwanasiasa na suala hilo ni la kipolisi zaidi na kuwashauri warudi polisi ili kupata msaada.
  Alisema baada ya kurudi polisi waliwaomba wawape barua ili watakapokuwa Uganda wasipate matatizo yoyote hivyo, polisi wakawapa barua.
  Alisema kuwa waliwasiliana na mtu huyo na kumuomba apunguze kiwango, na kuwakubalia wampe dola 400 na baada ya kukubaliana, aliwapa masharti ya kuzibadili fedha hizo kutoka Shilingi ya Tanzania na kuwa Dola.
  Alisema walianza mchakato wa kutafuta pasi za kusafiria na kwamba wafanyabiashara wenzake walimchangia Sh. million 1.5 kwa ajili ya nauli, malazi na kumlipa mtu huyo.
  Alisema walianza safari Mei 12, mwaka huu, yeye na mtu mmoja aliyeteuliwa na wenzake jina tunahifadhi na kuanza safari hadi mji wa Busia mpakani mwa Kenya na Uganda.
  Mtu aliyechukua mtoto wake alikuwa amewapa maelekezo kwamba washuke hapo. “Baada ya kufika alituambia twende kwenye benki ya Stanbic eneo la Jinja na tuweke fedha tutampata mtoto. Tuliweka fedha kwenye akaunti namba 0140592455501 Mei 13, tulikaa kwa saa sita tukisubiri na tulianza kuwa na hofu kuwa tumepoteza fedha, lakini alitupigia akidai anatuona hapo benki,” alisema na kuongeza:
  “Alitupa namba ya ambaye atamleta mtoto.”
  Alisema baada ya muda simu haikupatikana tena, lakini baada ya muda walipokea simu kutoka kwa ndugu zao Moshi, ambao mtu huyo alikuwa akiwasiliana nao na kuwaambia wawaambie waende kituo cha daladala watamkuta mtoto wao na baada ya kufika daladala waliwasiliana na kondakta ambaye alimpeleka mtoto akiwa na mfuko wenye nguo zake.
  Mzazi huyo alisema walishindwa kuchukua hatua zozote kwa kuwa kondakta huyo alidai kuwa alipewa mtoto huyo amshushe kwenye kituo hicho apokelewe na wazazi wake.
  Akizungumzia tukio hilo, mtoto huyo alisema alichukuliwa na mtu huyo nyumbani kwao na kumwabia anakwenda kumnunulia mhindi, na kwamba alimsafirisha kwa gari na alimfikisha Uganda.
  Mtoto huyo alisimulia kuwa alikuwa anapewa kila kitu katika nyumba aliyokuwa anaishi na kwamba amewaacha wenzake watatu.
  Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa (RCO), Linus Sinzumwa, alisema kuwa wazazi wa mtoto huyo walishindwa kuwa na subira kwani waliambiwa wasubiri mawasiliano kati ya Polisi wa Tanzania na Polisi wa kimataifa (Interpol).
  Alisema baba wa mtoto alitoa taarifa Mei 4 na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.
  Sinzumwa alisema wameshapata namba ya mtu aliyemtorosha mtoto huyo, hivyo wanashirikiana na Interpol kumtia mbaroni.
  Polisi waliokwenda eneo la tukio kwa ajili ya kumchukua mtoto huyo na wazazi wake, wananchi waliwagomea na kuwafukuza kwa kusema kuwa walikosa msaada wa polisi na walijichangisha wenyewe na kufanikisha kupatikana kwa mtoto huyo.
  Hata hivyo wananchi wa eneo la Mbuyuni waliandamana kumpokea mtoto huyo na wazazi wake katika kituo cha mabasi mjini hapa na kuzunguka kwa maandamano hadi nyumbani kwao.
  Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wananchi walisema ni uzembe wa polisi kwani wangeonyesha jitihada wangeokoa fedha hizo na kumkamata aliyemtorosha mtoto huyo.  CHANZO: NIPASHE
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Police wa Tanzania wapo kwa malengo maalum. Mojawapo ni kulinda maslahi ya viongozi na kuhakikisha usalama wa familia zao na mali zao kwa kuwa wasipofanya hivyo watakosa kazi. Nyingine ni masilahi binafsi na irresponsibilities. Kwamba mwananchi wa kawaida mimi atanisaidia nini?. Nina uhakika kuwa Polisi hao wangeambiwa kuna donge nono litatolewa akipatikana mtoto wangetumia mbinu zote mpaka wakawakamata wahalifu hao. Nchi za wenzetu polisi wanaona fahali zaidi kufanya kazi za wananchi, nchi yetu polisi wanaona fahari zaidi kufanya kazi za viongozi.
   
Loading...