Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Hivi karibuni nimejifunza kitu ambacho sikuwahi kukijua hapo kabla na na nilikuwa na boss wangu na mara nyingi alikuwa anasoma mawazo ya watu kwa kuangalia body language.
Awali nilijua ni mchawi aisee kumbe haya mambo yanafundishika.
Je mnajua mtu anayetazama juu kushoto anawaza nini?
Je anayetazama juu kulia naye mnajua anawaza nini?
Ngoja niwaelezee kuhusu hii siri ya body language.
Mtu anayetazama juu kushoto anajaribu kukumbuka picha ya kitu alichowahi kukiona wakati fulani anajaribu kuvuta taswira ya kitu hicho akilini mwake ili kuvuta kumbukumbu jinsi kitu hicho kilivyokuwa.
Je anayetazama juu kulia naye mnajua anawaza nini?
Mtu anayetazama juu kulia anajaribu kujenga picha ya kitu anachoelezwa ili kukipa sura ya jinsi kinavyokuwa kulingana na maelezo anayopewa au aliyopewa au simulizi tu kama hadithi za kufikirika pale tunapojaribu kuzipa sura.
Kwa mfano mwanaume anapohisi kusalitiwa na mkewe huwa na utazamaji huo pale anapojaribu kujenga picha ya jinsi mkewe anavyofanya akiwa kitandani na huyo bwanake.
Kama mwanamke akigombana na mumewe kwasababu ya kumtuhumu kumsaliti kisha mwanaume akawa kimya halafu akawa na utazamaji huo ni wazi baada ya hapo ugomvi ukawa mbaya zaidi kwani mwanaume akijenga picha zake kichwani za kuona kitendo cha kusalitiwa live akilini mwake hata kama si kweli akili itamwambia ni kweli na hapo kitakachofuata ni ngumu kusimulia.
Mwanamke akiona utazamaji huo kutoka kwa mumewe aondoke hapo kwa muda.
Mtu anayetazama kushoto anajaribu kukumbuka jambo fulani.
Mtu ambaye labda anahojiwa kuhusu jambo fulani pale anapojaribu kukumbuka huwa na utazamaji huo.
Wapelezi huweza kujua mtu anachoongea ni kweli au anadanganya kutokana na utazamaji wake.
Mtu anayetazama kulia anakuwa anajaribu kutengeneza sentensi hapo anakuwa anatengeneza maelezo kwasababu ya kudanganya kwa kuwa hakujiandaa na swali. Au anataka kuficha jambo na hapo ndipo tunasema kwamba maelezo yana nusu uongo nusu ukweli.
Je mtu anayetazama chini kulia mnajua kinachotembea akilini mwake?
Mtu anayetazama chini kulia anajaribu kukumbuka hisia alizozipata wakati fulani zinaweza kuwa za huzuni au za furaha hususan za kuridhishwa kimapenzi.
Je mtu anayetazama chini kushoto?
Mtu anayetazama chini kushoto anakuwa anamjadala mzito kichwani mwake. Inategemea ni mjadala gani kwani sura itatoa majibu
Huo utazamaji unafanya kazi kwa wanawake na wanaume.
Lakini kwa wale mashoto hufanya kazi kinyume chake.
Yaani inafanya kazi vise versa
Hii sasa ni kwa wanawake. Hivi mnajua mwanaume anayekutaka kimapenzi au anayekutamani jinsi anavyouangalia mwili wako anawasilisha hisia zake juu yako.
Utazamaji wake unakupa ujumbe maridhawa.
Je unawezaje kujua ujumbe anaokupa?
Ask me......
Nitarudi......