Utawala wa awamu ya 5 utafanikiwa?

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,305
2,562
Mpaka kufikia sasa tumeona kila dalili kuwa utawala huu hausikilizi ushauri wowote kutoka kwa mtu/watu au kikundi cha watu wanaotofautiana naye kimtazamo.Analolifikiria mheshimiwa rais na utawala wake ndilo litakalofanyika,end of discussion. Uzoefu unaonyesha kuwa nchi nyingi au makampuni mengi yaliyopata mafanikio yalikumbatia a sense of diversity kwamba watu wanaotoka katika different ethnic, religious, political and class backgrounds wana kitu kizuri wanachoweza kukileta kwa manufaa ya nchi/kampuni husika. Diversity brings best decision making and finally best solution to most complex challenges kwavile watu wanaotoka katika certain group wanaweza kuleta uzoefu wao wa utatuzi wa changamoto mbalimbali kutoka huko.

Uzoefu unaonyesha kuwa mawazo ya kundi moja katika namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali mara nyingine huishia kushindwa, wazo moja ni muhimu lishindanishwe na lingine ili hatimaye lipatikane wazo bora zaidi kwaajili ya manufaa ya wengi, na si kulazimisha wazo.

Yanayotokea chini ya utawala wa awamu ya 5 ni mfano halisi wa utawala ambao hautaki mawazo na mipango yake ipate changamoto kutoka makundi mengine ya kisiasa yanayotofautiana kimtizamo na huu utawala. And so far most of their ideas are impractical, they can never be useful in the real world, only in the fantasy world! Utaanzishaje viwanda wakati huo huo ukifanya kila njia kuwanyang'anya wananchi fedha kupitia kodi holela?

Wananchi hawa unaowanyang'anya fedha kupitia mlolongo mrefu wa kodi (wakienda kununua bidhaa dukani kuna kodi,kutoa pesa kwa njia ya simu kuna kodi,nyumba za kupangisha zina kodi,vinywaji kodi,nk) ndio Wateja watarajiwa wa bidhaa zitakazozalishwa na hivyo viwanda, je wataweza kumudu kununua? Bado pia kuna changamoto kubwa katika sera za fedha za nchi hii ambazo zinapelekea benki nyingi nchini kutoza riba kubwa kwa wakopaji, je hivyo viwanda vitaanzishwa katika mazingira gani hadi kuweza kuzalisha bidhaa za bei nafuu ambayo wananchi wenye kipato cha kawaida waweze kumudu?

Labda kama vitaendeshwa kwa kutumia ruzuku (grants) kutoka serikalini na hii ina maana ni fedha za walipa kodi ndizo zitakazoviweka viwanda hivi hai kama serikali itaamua viendeshwe nje ya mifumo na taratibu za kifedha na kiuchumi tulivyojiwekea, this might mean more taxes for the survival of these industries.
 
Back
Top Bottom