Utaukosa urais kwa sababu ya wapambe

Utaukosa urais kwa sababu ya wapambe

NYAMALINGO

Member
Joined
Jun 14, 2015
Posts
32
Reaction score
38
Ndugu watanzania wenzangu,Hakuna asiyefahamu kuwa nchi yetu inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi october tarehe 25,Na kwamba tutapata fursa ya kila mmoja wetu kumchagua mgombea au chama anachoona anafaa/kinafaa.Siku zote palipo na uchaguzi popote pale duniani,Kuna wagombea na wapiga kura.

Katika muktadha huu,Wagombea wanakuwa kama mwanafunzi na wapiga kura wanakuwa kama walimu wa masomo mbalimbali.

Kama kawaida,mwalimu anapomaliza kuwafundisha wanafunzi wake na ili aweze kufanya tathmini ya uelewa wa wanafunzi wake,anawauliza maswali,anatoa test na mwisho anawapa mtihani.

Hii imekuwa ni tofauti kwetu watanzania,kwani kunawapambe wa watia nia fulani ambao kila mtia nia wa kambi yao anapoulizwa maswali na watanzania,wao wanachukulia kuwa mtia nia wao anachafuliwa,anadhalilishwa,anatukanwa na hata kufikiri kuwa anaonewa.

Watia nia hawa kwa kiwango kikubwa wanafikiri kuwa kwa kufanya hivyo wanamsaidia mgombea wao,Kumbe wanamdidimiza mgombea wao bila ya wao kujua.

Wapambe hawa ni vyema wakatafakari na kutambua kuwa hata kama mgombea wao atapata watanzania wanaomuunga mkono 20,000 kila mkoa,bado watahitaji kura za ziada kutoka kwa watanzania ili mgombea wao ashinde.HILI HAWALIFAHAMU KABISA,Wao ni matusi tu kwa kwenda mbele!!.

Wapambe hawa wakumbuke kuwa wanapokuwa wanawatukana na kuwakejeli watanzania wanaouliza maswali juu ya mgombea wao,Wanakuwa wanataka kujua ukweli wa mambo juu ya kile wanachokisikia kutoka vyanzo mbalimbali na mwisho wa siku wajue ukweli wa jambo hilo,Lakini wanapokuwa wanatukanwa au kukejeliwa,Watanzania hawa huchukua maswali hayo na kuyapeleka kwenye jamii ambayo ndo ina wapiga kura wengi kuliko wapambe hao.

Naomba watanzania wenzangu tujikumbushe historia ya mwaka 1995 kwenye uchaguzi mkuu.Mzee mrema alikuwa ni mgombea aliyeonekana kukubalika zaidi kuliko wagombea wengine.

Lakini,baada ya mdahalo uliofanyika kilimanjaro hotel na wagombea wote kujieleza na kuulizwa maswali mbalimbali na kujibu,Benjamin mkapa alionekana kuwa yeye ndiye anawafaa watanzania.

Uchaguzi wa mwaka 2010,katibu mkuu wa ccm mzee makamba alipiga marufuku wagombea ubunge wanaotokana na ccm wasishiriki midahalo kupitia kipindi cha shaban kisu cha mchakato majimboni..TBC.Kila mtanzania anafahamu kilichotokea;"CHADEMA walipata ongezeko la wabunge kwa zaidi ya asilimia 400.

Hapo mwanzo nimesema kuwa,hata kama wapambe hawa watapata wapiga kura 20,000 kila mkoa,bado idadi hiyo hazitatosha kumpeleka ikulu mgombea wao.

Ninawaomba wapambe wa mgombea huyu wajaribu kufanya tathmini kupitia kwa watu wao waliopo mikoani ili kujua ni kwa namna gani mgombea wao anavyokubalika katika jamii.

Ninaamini watadanganywa kuwa "mambo ni mazuri tu",Lakini wakifanya ziara ya kushitukiza mikoani,watakuta hali ni tofauti.

Hii inatokana na wapambe hawa kujiaminisha kuwa mgombea wao anafaa na hata pale yanapoulizwa maswali yanayotaka majibu,wapambe wanatukana na kukejeli.

NAWASILISHA
 
Back
Top Bottom