Ndg wadau nina masikitiko makubwa kuhusu vyuo vikuu vinavyopandisha ada kiholela, hilo limetokea mwaka huu wa masomo 2016/17 katika chuo cha Stella Maris Mtwara University Collage, kwamba wamepandisha ada (administrative fee kutoka 132000/- hadi 320000/- hili ni ongezeko Tsh 200000/- kubwa linalostajabisha wanafunzi wa chuo hicho hawakupewa taarifa ya ongezeko la kiasi hicho cha fedha mapema, taarifa ilitolewa tarehe 24/09/2016 siku moja baada ya chuo kufunguliwa (23/09/2016).... Je kutokana na sheria za vyuo vikuu kuhusu ongezeko la ada sheria inasemaje? Naomba msaada wenu wadau
by Mwl Kitoi