Utaratibu wa wafanyabiashara kuhifadhi sukari umeanza baada ya serikali kuzuia uingiza wa sukari?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Hili ni swali ninalojiuliza maana inawezekana wafanyabiashara hawa hufanya hivi kila mwaka kutokana na viwanda vya sukari kufungwa kipindi hiki kwa ajili ya matengenezo.

Tunachopaswa kujua//kuona ni nyaraka za manunuzi zinazoonyesha tarehe ya ununuzi wa tani hizo za sukari ili kama manunuzi yalifanyika kabla ya agizo la serikali la kupiga marufuku uingiza wa sukari kutoka nje, basi tusiwalaumu hawa wafanyabiashara bali tuilaumu serikali.

Nafikiri hata TRA wanaweza kuwa na data/nyaraka za mauziano ya sukari kati ya wenye viwanda na wafanyabiashara hawa kwa madhumi ya utozaji wa kodi hivyo wanaweza kusaidia uchunguzi.
 
Nimejiuliza maswali haya, je nivibaya mtu akiweka mzigo wake stoo ambao hajapewa ruzuku na serikali? je vp mabilionea na mamilionea ambao wametajwa kuwa wanafedha ndani na nje ya nchi wakati wengine hawana hata uhakika wa kula? je hela zao zinaweza kugawiwa kwa mafukara? je kama mtu alinunua bidhaa bei ghali analazimishwa kuuza bei ndogo?
 
Huko sio kuweka store, ni kuficha mzigo usitumike wakati kunauhitaji. ni sawa Tanzania kuwe na njaa na wewe umeficha tabi 4000 za mahindi. Lazima uitwe shetani.
 
Pesa ukiificha lazima utakuwa umeificha bank.. Na Bank wanaitumia kukopesha watu. Kuna tofauti kubwa sana kuficha fedha na kuficha bidhaa.
 
Leseni ya.biashara no mkataba kati ya mfanyabiashara na serikali kuwa utatoa Huduma kulingana na masharti na sheria ya biashara. Moja ya sheria iliyopo ni kuhujunu uchumi kwa kusababisha uhaba Wa bidhaa ili wananchi wapate shida kuchochea dola ianguke. Bidhaa haipo sokoni, kibali cha kuagiza umepewa na serikali, wewe uhifadhi ghalani mpaka lini na lengo lako nini?
 
Acha tu waisome namba.

Wafanya biashara ndio wamekua wakiua demokrasia hapa nchini kila mwaka wakifadhili ccm ili iendelee kukaa madarakani waendelee kutuibia.
 
Acha tu waisome namba.

Wafanya biashara ndio wamekua wakiua demokrasia hapa nchini kila mwaka wakifadhili ccm ili iendelee kukaa madarakani waendelee kutuibia.
Hahahahahaaaàa. Vipi kuhusu fisadi Lowasa na genge lake akina Rostam Aziz, Yusuph Manji na wengineo? Hao si wafanyabiashara?
 
Salary Slip siku zote unapingana na serikali hata kama maamuzi iliyochukua ni sahihi. Kwa sisi tunaokujua hatuhangaiki na wewe
 
Inasikitisha sana ,chama kinachojinasibu kinauwezo Wa kuitoa ccm madarakani na kuongoza nchi (chadema) kinashindwa kuzuia wafanyabiashara kuficha sukari Arusha.

Sasa wananchi chini ya chadema Arusha wanateseka kwa kukosa sukari.!!!
 
Tatizo sio kuhifadhi, tatizo ni hali iliyopo.

Watu wanakanyagana kwenye foleni kwa kupigania sukari kidogo iliyopo wewe unahifadhi maelfu ya tani kwenye Ghala.....kweli.
 
Inasikitisha sana ,chama kinachojinasibu kinauwezo Wa kuitoa ccm madarakani na kuongoza nchi (chadema) kinashindwa kuzuia wafanyabiashara kuficha sukari Arusha.

Sasa wananchi chini ya chadema Arusha wanateseka kwa kukosa sukari.!!!
Zero brain huyu!!
 
Hivi kama Mwenye ghala la kuhifadhi sukari anasubiri Wateja waje,halafu hawaoni au wakija wanachukua mzigo kidogo yeye afanyeje?achukue kipaza Saudi awaite?
 
Kikombe cha chai kinawatoa jasho Ccm,sukari ni ishu,sembuse kununua mitambo kwa ajili ya Tanzania ya viwanda,hebu lete uji wa chumvi tunywe
 
Back
Top Bottom