Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 33
- 46
Jana tarehe 17 Februari 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora kupitia kesi ya Amina Mwaluko dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilibatilisha utaratibu wa baadhi ya watu wakiwemo maafisa wa mahakama, na maafisa sheria wa sekta za umma kupewa uwakili bila kuhitimu Astashahada katika Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) (Almaarufu Mawakili wa Vitu Maalum). Kesi hiyo imesikilizwa na kuamriwa na jopo la majaji watatu akiwemo Jaji Daktari Mambi, Jaji Daktari Mango na Jaji Daktari Mirindo.
Utaratibu huo ulilenga kuwaruhusu maafisa wa taasisi za serikali (Umma) kuapishwa kuwa mawakili na Jaji Mkuu endapo wametimiza miaka kumi na kuendelea katika majukumu hayo ya kisheria. Katika Uamuzi huo Mahakama Kuu imeeleza kwamba Sheria iliyoruhusu utaratibu huo ni Batili, zipo kinyume na KATIBA, zinakiuka Haki ya Usawa, ni za Kibaguzi kwa maana inataka wanaoapishwa kuwa watumishi wa umma tu wenye uzoefu wa miaka 10 katika sheria na kuwaacha watumishi wa taasisi binafsi wenye vigezo sawa.
Hivyo Mahakama imeamua kwamba vifungu hivyo ni batili kuanzia tarehe ya uamuzi huo (17/02/2026) kwa kuwa vinakiuka ibara ya 12 na 13(1), (2) na (4) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho.
Hatahivyo, katika uamuzi huo, Mahakama imesema kwa wale waliokwisha kuwa mawakili chini ya Sheria hiyo wataendelea kutambulika kama mawakili halali. Ikumbukwe Disemba 2025 takribani mawakili 388 waliapishwa chini ya utaratibu huo ambao Mahakama Kuu imeamua kuwa ni batili na ni uvunjifu wa Katiba.
Aidha, katika jopo la Majaji watatu waliosikiliza shauri hilo, Jaji Mambi yeye amechukuwa mtazamo tofauti kwa kuandika Uamuzi kinzani (Dissenting Opinion) akieleza mtazamo wake na kufafanua sababu kadhaa akifananua kwamba Sheria ile haipo kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.